Tuesday, August 27, 2013

ULIMI..

ULIMI ni nyama laini sana ambayo huungua na kupoozwa kwa haraka sana, ulimi usipousafisha vizuri hufanya mdomo kutoa harufu mbaya sana, ulimi ni wa heshima na unatakiwa kutunzwa sana ndio maana ukafichwa ndani ya mdomo huonekana pale panapotakiwa tu..ulimi wapendwa ndio hubeba maisha yetu, hubeba mahusiano yetu na hubeba ndoa zetu ulimi wako unaongeaje wewe, unaiambia nini jamii, unaambia nini watoto wako, unamwambia nini mume/mke wako ndoa nyingi zimevunjika na hazina raha kwasababu ya ulimi wetu, mumeo/mkeo anapokosa unaanza kupayuka matusi na maneno ya kashfa, au tena mama mkwe na ma wifi ukiwaamlia mbona wanajuta kumjua hata huyo ndugu yao..lakini ukijuwa kutumia ulimi wako vizuri utapata baraka katika ndoa yako watu wa nje wakiiona watatamani wawe kama wewe, ndoa zilizo dumu zaidi ya miaka 20 usidhani wao yaliwanyookea tu hapana bali walijuwa kugombana na kuongea kwapamoja vizuri, ULIMI unachachua na kulainisha kwa wakati mmoja jua kuchuja maneno yako ukiwa unaongea na mumeo/mpenzi wako ili uwe na amani na upendo wa kweli utawale maisha yenu.

Neno

1. Tuombe kwa ajili ya utii wa wake kwa waume zao. Kama wewe ni mke omba Mungu akuwezeshe kumtii mume wako hata kama ni ngumu. Omba neema ya Mungu na uwezo wa kuweza kumtii mume wako. Kama hujaolewa omba uweze kumtii mumeo siku ukiolewa. Mume muombee mke wako aweze kuwa mtii kwako.

1 PET. 3:1-2 
"Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu."

EFE. 5:22-23 
"Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili."

Source: Woman of Christ

Mwanamke sikia hii

Kila mmoja anafahamu kuwa biblia inawataka wanawake wawatii na kuwaheshimu waume zao, ila wengi hawajui mambo gani yanaonyesha haumuheshimu na athari za kutomuheshimu ni nini. Kumuheshimu mume kunaanzia ndani ya moyo na nje ni matokeo tu. Haijalishi mumeo ameokoka au la, unakipato kumzidi au la, mkorofi, mlevi au vyovyote. Maadamu ni mume wako yakupasa kumtii na kumheshimu katika Bwana.
Unapokuwa unambeza na kumdharau mumeo ndani ya moyo wako na kumuona hana faida ni sawa na kumfanyia akiwa anaona maana katika ulimwengu wa roho unampa shetani nafasi. Huwezi kumuombea mtu unayemdharau ndani ya moyo wako. Mambo mengine yanayoonyesha huna utii kwa mumeo ni kutomshirikisha mipango yako na kufanya mambo bila kujali yeye anasema nini, tangu unachangia kitchen party hana habari, umepata kadi bado kimya halafu asubuhi unamwambia "leo naenda kwenye kitchen party", hiyo haifai kabisa. Mumeo anapaswa kujua ratiba zako zote ziwe za kikazi, kanisani, kijamii, binafsi n.k na kwa pamoja mnakubaliana jinsi ua kufanya.
Kutokuwajali ndugu zake hasa wazazi wake. Wanawake wengi wanaonyesha upendo kwa mume ila hawawajali ndugu wa mume, hii kwa mume anaona ni kutokumheshimu. Mheshimu mume kwa kuwajali na kuwapenda ndugu zake bila kuangalia wao wanakutendea nini. Jambo lingine kubwa la kumuonyesha heshima ni kuwa tayari pale anapokuhitaji kimahaba na sio kila siku unatoa visingizio. Mume ambaye mkewe kila siku anatoa visingizio au haonyeshi ushirikiano anajiona kutoheshimika na mkewe. Mume hujisikia kuheshimika pale mkewe anapokuwa tayari kufurahi naye bila kuona kama ni kazi wala kulazimishwa bali kwa moyo uliochangamka na sio kutumia jambo hilo kama silaha ya kumuadhibu au pale anapotaka kitu.
Athari za mume ambaye mkewe hamheshimu ni nyingi, zikiwemo kukosa ujasiri mbele za familia, kazini na hata kanisani. Hujiona hajakamilika na hawezi kufanya kazi zake kwa ujasiri. Pia huwa ni mtu aliyejaa hasira na asiye na furaha hasa akiwa pekeyake, wakati mwingine hujikuta anajiingiza kwenye emotional affair ili kujaribu kutimiziwa hitaji la heshima maana ni hitaji kubwa sana kwa mwanaume. Kama ni boss ofisini basi atakuwa mkali sana au mkali kwa watoto. 
Kumheshimu mume sio utumwa wala unyanyasaji bali ndio msingi wa ndoa imara na yenye baraka.

Source: Woman of Christ

Word..

Hii imewatokea wengi. Familia za kiafrika jambo la kukaa na ndugu ni la kawaida kabisa na wengi wetu kabla hatujaishi wenyewe tumeishi kwa ndugu. Sasa kuna jambo huwa linasumbua watu wengi, unakuta unaishi na mtu vizuri, unakaa naye kama mwanao means unamjali, unamtimizia mahitaji yote na vile vile akikosea unamkanya. Lakini unakuta mtu huyo hawi na furaha wala kuchangamka akiwa nawe, ila akiwa na watu wengine yupo more than happy. Anaweza kuwa mdogo wako, dada/ kaka yako, wifi, mkwe, mpwa, n.k.
Hali hii husababishwa na nini? Je ni kiburi au nidhamu ya woga? Na mtu wa aina hii unaishi naye vipi?

Source:Woman of Christ

Friday, August 23, 2013

Word

Wasichana wengi wa siku hizi wanapenda sana maisha super. Wanataka wampate kijana aliyejikamilisha au angalau awe na degree na gari. Utakuta msichana yupo kwenye mahusiano na mkaka na amekubali kuoana naye, baada ya muda kupita anakuja kijana msomi mwenye hela na gari anamtosa mchumba wake na haraka unasikia harusi. Wakaka wengi sana wamejeruhiwa kwa sababu ya kuachwa na wachumba zao kuolewa na wenye hela zaidi yao.
Hivi unawezaje kumuangalia mtu leo ukajua hatima ya maisha yake? Kama ulikuwa humpendi ni kwanini ulikubali ombi lake na ukawa naye na akakutambulisha kwa marafiki na baadhi ya ndugu? Kama unaona hujampenda mkaka na wala Mungu hajasema nawe kuwa ndiye, kwanini umkubalie? kumbe wewe unawapanga uone nani mambo safi zaidi ndio uolewe naye? Acha tabia hiyo maana hata ukiingia kwenye ndoa na mumeo akatetereka kiuchumi utakuwa rahisi sana kumsaliti kwa wenye mali.
Kama unatafuta kuolewa ili upate wa kukuvisha na kukupatia fedha please kuna better alternative ambayo ni kutafuta kazi na kuifanya kwa bidii. Ndoa sio gari, nyumba, fenicha, wala fedha.

Source:Woman of Christ

Wednesday, August 21, 2013

Ubinafsi...

Katika mahusiano haswa kwa wale ambao ni wachumba wanaoelekea kwenye ndoa ama kwa wale walio kwenye ndoa hakuna kitu kibaya kama ubinafsi, ubinafsi haurekebiki wala hauna tiba heri upewe umbea kuliko ubinafsi na ni mbaya ukipewa vyote viwili..mahusiano mengi hayadumu kwasababu ya ubinafsi mnapoamua kuwa pamoja kila kitu ni chenu wote sio chako wala chake matatizo yanaingia pale mnapogombana na hii sana ni kwa walio ndani ya ndoa utakuta tena mmegombana na mwenzako basi kama ulikuwa unataka kumfanyia jambo zuri humfanyii tena, labda ulitaka kumnunulia gari mkeo kisa mmegombana kakununia siku mbili tatu unagairi tena humnunulii au mke unataka kumnunulia mumeo suti mpya kisa amerudi usiku wa manane unagombana hata hutaki tena kumfanyia jema wala kumnunulia tena ulichotaka kumpa..hii ni mbaya sana na nikukomoana tukiishi maisha ya kukomoana na ubinafsi kisa ni chako hutaki kumpa mwenzako hatutafika..MUNGU alimuumba mwanaume kuwa kichwa cha familia mwanamke acha ubinafsi muweke mumeo mbele awe kichwa hata kama umempita kipato sio kila mtu ajuwe wewe ndio unaendesha familia muache baba awe baba, na unapoingia katika ndoa kwa mguu mmoja nje na mwengine ndani lazima utakuwa mbinafsi utaogopa kushirikiana na mwenzako ukijuwa kesho tukiachana je kitu changu hiki nitakipataje..jamani hayo sio maisha  lazima kila kitu unachotaka kufanya maishani ukifanye on your best ingia kwenye ndoa kwa miguu miwili hata kama wewe ndio unakipato kuliko mumeo mnapokuwa sehemu ya wazi muache mumeo awe mumeo mpe heshima yake kama wewe ndio unatakiwa kulipia kitu fulani mbele za watu kabla hamjashuka kwenye gari au kufika hiyo sehemu mpe mumeo hela alipe yeye mkifika inampa security na kujiona yeye ni mwanaume..na sio mkigombana unamnyali kwa watu mwanaume mwenyewe miye ndio nakuweka ndani nakuhudumia na kukupa kila kitu..leo MUNGU amekubariki mwanamke/mwanaume unavyo hivyo ulivyokuwa nazo anauwezo wa kugeuza shilingi upande wa pili akipewa mwenzako itakuwaje??? ataishije na wewe?? TAFAKARI

word

Kijana umemuona dada, ukampenda na ukamfuata kumueleza yako ya moyoni. Baada ya muda akakubali na mkawa kwenye mahusiano mkitaraji kufunga ndoa maana ulivyomfuata ulimwambia unataka kumuoa. Baada ya miezi kadhaa kimyaaa, hakuna simu, hakuna msg na ukitafutwa unasema upo busy. Dada wa watu anakuwa katikati haelewi ndoa ipo au haipo, haelewi kwanini umekata mawasiliano ghafla na wala hamjagombana.
Kama ulikuwa umewaweka pending wengi na umeshamchagua mmoja kwanini kuendelea kumfunga dada wa watu? Kama umeona yaliyomo hayamo kwa mtazamo wako kwanini usinwambie ukweli kuwa wewe nayeye basi? Na kwanini unamuahidi mtu kuwa utamuoa wakati moyoni unajua kabisa sio kweli au wapo wengi hivyo uhakika haupo? Unaishia kuumiza moyo wa dada wa watu maana yeye anakuwa amejitoa kweli kweli. Acha kuharibu maisha ya mtu usiye na mpango wa kumuoa, anawakataa wengine akijua yupo na wewe kumbe wewe umempanga unamthaminisha. Ukiona sio unapotea kimya kimya yeye anajua ana mtu anakuja kushangaa unaoa.
Huwezi kuwa na ndoa yenye furaha na baraka huku kwenye ujana wako ulikuwa mtu wa kuwaumiza tu wadada kwa kuwachumbia na kuwatosa. Kama huna uhakika wa kumuoa usimweleze kabisaa, hadi utakapopata uhakika yupi utamuoa.

Source: Woman of Christ

Word

Furaha haitafutwi kwa jirani. Moyo wa kuchangamka hautokani na mali. Amani haitokani na kukosa matatizo. Unapaswa kuwa na moyo wa shukrani (heart of gratitude) ili uweze kuwa na furaha, amani na moyo uliochangamka. Unaowaona wana furaha na moyo uliochangamka sio kwamba hawana matatizo au wanawatu wa kuwachangamsha la bali wana moyo wa shukrani kwa Mungu wao kwa kila kitu. Kila wakati wanayaona yanayowapasa kumshukuru na sio kuangalia wasivyonavyo.
Mtu mwenye moyo wa shukrani lazima atakuwa mwenye furaha, amezungukwa na marafiki, ana amani, mjasiri na anayejiamini, muwazi na rahisi kuwasiliana naye. Mtu asiye na moyo wa shukrani mara zote yupo mwenyewe, anahasirahasira, hana furaha, hajiamini, anaona kila aliyefanikiwa zaidi yake analazimika kumsaidia, sio muwazi.
Hata maombi pia yanaonyesha maana mwenye moyo wa shukrani maombi yake yamejaa sifa na shukrani kwa Mungu na yule asiye na shukrani maombi yake yamejaa laumu na manung'uniko.

Source: Woman of Christ

Tuesday, August 20, 2013

I WANT TO SAVE A LIFE...DO YOU??

Wapendwa MUNGU ni mwema na anatupenda sana, sisi tuliobarikiwa kuwa salama leo, wenye afya na tunahema na kufurahia maisha, lakini tukumbuke kuna wenzetu wanaumwa wapo mahospitalini bila msaada zaidi tu ya kumtegemea MUNGU, nimeguswa sana tokea asubuhi nikaongea narafiki yangu wa karibu ya kwamba ninawito ndani yangu ya kutoa damu ambayo itasaidia watu wanaokuja hospital wakihitaji damu, wagonjwa wengi katika mwaka wanahitaji damu, labda umeshaona ndugu yako, rafiki yako, jirani yako,mzazi wako,mume/mke wako au hata mtoto wako anahitaji damu na ukaweza msaidia ila kuna wale ambao wanahitaji misaada na wanategemea tu sisi ambao tunauwezo wa kutoa damu ndipo wapewe wao nakumbuka babu yangu kabla hajafariki mwezi wa tano aliumwa sana siku tumempeleka hospital alitapika karibia beseni zima la damu, tukiwa tumekaa reception muhimbili madaktari wakaamuru awekewe kwanza drip ya damu kabla hajapelekwa kulazwa maana asingeweza kufika chumbani kama angekuwa hajaongezewa damu nashukuru kwa damu zilizokuwepo siku hiyo mpaka akapewa japo siku tatu baadaye alifariki, ndio maana nikawaza i want to save a life japo kwa siku tatu tu huyu baba aweze kumwambia mkewe jinsi anavyompenda, huyu mama aweze kuwabariki watoto wake kabla hajafa..siku tatu ni masaa mengi sana ya kubadilisha mtu na dunia..ndio maana 21/9/2013 ni siku ambayo mimi, wewe na yule tutakayoenda damu salama kwenda kutoa damu ili ziwasaidie watu hata kwa siku tatu tu, tuendelee kula matembele kwa wingi na virutubisho vya kujaza damu zetu..tafadhali kama na wewe ni mmoja wa watu unaotaka kushiriki naomba unipetaarifa mapema nikuweke katika maandalizi ya siku hii 0717 019320...MUNGU awabariki sana

Monday, August 19, 2013

Kuelekea kupata mtoto...

Nataka niongee na wanawake ambao hawajazaa na wanawake ambao wanamimba, unajuwa wewe kama mwanamke ni mtu wa thamani sana duniani bila wewe dunia itakuwa tupu, ni wewe unaweza ukazaa watoto wenye baraka na ni wewe unaweza ukazaa watoto wenye laana kabla hujapata mimba pindi unapoanza kumjuwa mwanaume hakikisha mara kwa mara unaombea tumbo na uzao wako utafanyaje huwa napenda kuwashauri wanawake vyumbani mwao wasikose mafuta ya nazi ama ya olive oil utayaombea hayo mafuta kwa dini uliyonayo mimi huyaombea na kuyageuza kuwa damu ya yesu, basi kila utakapokuwa unaombea tumbo lako utajipaka na kuanza kuongea na MUNGU kuhusu uzao wako kama hujazaa utaomba MUNGU akubariki tumbo lako likapate kubeba mimba kwamba hatakama kuna wagumba kwenye ukoo wenu lakini wewe utazaa kataa hali na roho ya ugumba na ukazae tu na mume wako au na mwanaume MUNGU aliyekupangia kataa kuzaa na mume wa mtu kwani watoto wengi wa wame wa watu hawathaminiwi wanafichwa hawatambuliki na utakapokuwa umebeba mimba kila siku asubuhi paka tumbo lako na yale mafuta muombe MUNGU akulindie mtoto wako kila siku, mwanao akitoka afanane na baba yake au wewe mama yake, akawe mtoto wa baraka, mvunjie laana zote za ukoo kabla hajatoka, kataa mimba kuharibika, muombee akija duniani akapate kuwa baraka kwa watu na sio laana, muombee akawe na akili kabla hajaanza hata kuongea,usisahau kumuombea kuwa mcha MUNGU maana huo ndio wingi wa maarifa...TUJIFUNZE kuombea matumbo yetu dunia inaharibika na kubarikiwa kwasababu ya tumbo la MWANAMKE...

Kukataliwa -2

Soma kwanza sehemu ya kwanza.
Unapoweka thamani yako kwa wanadamu ni lazima utaona kukataliwa na kujikuta unaruhisu roho za kukataliwa kuingia kwako. Lazima utambue kuwa thamani yako inatoka kwa Mungu na si wanadamu wanakuonaje. Haijalishi nani anasema nini bali tafuta Mungu anasema nini. Acha kumlaumu Mungu na kujilaumu unayopitia, biblia imasema mapito ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humlinda na hayo yote.

Usiruhusu chuki, uchungu, hasira na wivu vipate nafasi ndani ya moyo wako. Soma neno la Mungu lijae ndani yako na maombi kwa wingi. Kataa roho ya kukataliwa isipate kibali ndani yako kwa kuondoa milango ambayo ni kutokusamehe, chuki, wivu, uchungu na kumlaumu Mungu. Usiangalie yule aliyekutendea mabaya na kukukataa kama vile yeye ndiye mwenye hatima ya maisha yako bali muangalie Mungu aliyeahidi kuwa nawe siku zote.
EBR. 13:5b-6 
"kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?"

Mambo ya kufanya kushinda kukataliwa
1. Mruhusu Roho mtakatifu akuonyeshe umeumizwa wapi na kwa kiasi gani kwa kukataliwa.
2. Samehe wale waliokuumiza
3. Tupilia mbali matunda ya kukataliwa: chuki, hasira, uasi, uchungu n.k.
4. Kubali kuwa Mungu amekukubali kupitia Yesu Kristo.
5. Jikubali

ZAB. 71:5-7, 13 
"Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima. Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi, Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu. Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya."

Soma pia Ebrania 4:16 Zaburi 23 1 Samwel 53:4

Source: Woman of Christ

Kukataliwa -1


Roho ya kukataliwa inawasumbua watu wengi. Wengi wanaosumbuka na kukataliwa inawezekana walikuwa na wazazi wasiojali, wazazi walitengana, wamelelewa na mzazi wa kambo, hawakuwa vizuri darasani, n.k. Kukataliwa kunaumiza sana na kunaua kabisa hali ya kujiamini na shetani huitumia sana kuharibu maisha ya watu. Shetani anawafanya watu wasahau kabisa juu ya upendo wa Mungu na kuendelea kuumia na kuteseka. 
EFE. 3:19 
"na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu."

Kukataliwa kunaleta vidonda kwenye hisia na visipotibiwa hukua na kuwa vidonda vya kiroho kama kutokusamehe, wivu, chuki, uchungu na kumlaumu Mungu. Vidonda hivi hufungua milango kwa roho chafu kukuingilia kupitia milango hiyo. Shetani anafurahia moyo wako ukijaa mawazo mabaya juu ya watu wengine unaowaona kwamba hawajakutendea mema.
Kukataliwa kunamfanya mtu kuwa na tabia zifuatazo:
1. Uasi
2. Unafiki (ukiwa mbele za watu fulani unabadilika ili ukubalike)
3. Kukataa wengine
4. Kila wakati kujihisi kuwa unakataliwa
5. Kuhitaji sana kukubaliwa na kila mtu
6. Kujihurumia
7. Kutokuwa tayari kukosolewa au kusahihishwa
8. Kutokuweza kupokea wala kuonyesha upendo.
9. Kumlaumu Mungu kwa hali uliyonayo
10. Kiburi
11. Ukiwa hata ukizungukwa na watu.
12. Kujiona huna thamani, wala tumaini
13. Wivu, chuki na husuda.

Wengine wanahisi kukataliwa wakati si kweli. Roho hii ya kukataliwa inakufanya uone kama kila ambaye hajafanya jambo fulani kukusaidia au kukufurahia basi anakukataa. Biblia inasema aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Pia kuna wanaojikataa wenyewe na kupelekea kujichukia. Hali hii hutokana na kushindwa kujisamee kwa kosa fulani ukilotenda siku za nyuma na likakuletea madhara makubwa.
Tutaendelea sehemu ya pili jinsi ya kukabiliana na hali hii.

Source: Woman of Christ

Friday, August 16, 2013

Word...

Mara nyingi sana tumesikia wanaume wanapopatikana wameisaliti ndoa visingizio huwa mke wangu mkorofi, mke wangu hanisikilizi, mke wangu hiki na mke wangu kile. Na mke hulaumiwa na kila mtu na hulazimishwa kumsamehe mume kwa kigezo ni kosa lake mwenyewe. Ndio tunajua kuwa mke anapaswa kumheshimu, kumsikiliza na kumhudumia mumewe lakini sidhani kwamba mke akishindwa kufanya hivi kwa kutoelewa, kiburi au uchungu basi ni sawa mume kutafuta mtu mwingine.
Maana mume anawajibika kumhudumia na kumtunza mkewe, wapo wanaume wengi tu hawatimizi hili hakini hatuoni wake zao wakitafuta watu nje wa kuwatimizia. Ikitokea hivyo basi mume anaambiwa mke hafai kusamehewa hata wanawake wanaosimamia mume lazima asamehewe anapokosea nao pia wanasimamia mke lazima aondoke. Je, mke anawajibika kwa tabia ya mumewe?
Wako wapi waume wanaowapenda wake zao hata pale ambapo mke anaonekana jeuri, maana mtu ambaye ni mgumu kupendeka ndiye anayehitaji upendo sana. Mume kwa upendo unaweza mbadilisha mke ndio maana biblia inasema waume wawapende wake zao, hapa bila kujali mke anafanya au hafanyi nini.

Source: Woman of Christ

Nimepata maswali mengi kuhusu wanaume kwanini wanaume wengi hawawezi kutulia na mwanamke mmoja ilianza hivi twende kwenye biblia MUNGU alimuumba mwanaume na katika ubavu wake wa kushoto akatoa ubavu mmoja na kumuumba mwanamke na akawaambia wafanye yote kwenye bustani lakini wasile matunda ya mti mmoja ambao walikatazwa, na kweli walifanya hivyo mpaka shetani alipokuja kumpotosha mwanamke na mwanamke naye akampotosha mwanaume wakatenda dhambi na ndipo matatizo yalipoanza hapo duniani na tokea siku hiyo mwanaume akawa mtumwa kwa mdhaifu sana mbele ya mwanamke iwe kwa mazuri ama mabaya mwanamke anauwezo wa kuulainisha moyo wa mwanaume na kumfanya afanye atakayo mwanamke, twende kwenye mahusiano tuongelee wanawake ambao wanatongozwa na mume wa mtu na wanajuwa kabisa ni mume wa mtu lakini bado anamkubali sio kwamba anapenda bali ni shetani anajitumia tena kwa mwanamke kuharibu ndia ya huyo mwanamke na ukiangalia mwanamme anavyomtongoza mwanamke atampa sababu mbaya kibao anazofanya mkewe ili aonewe huruma na kukubaliwa na mengi huwa niuongo lakini wanaume wameshajuwa jinsi ya kulainisha wanawake, na shetani pia atajiingiza kwa mwanamke kujitongozesha kwa mume wa mtu sio kwamba anapenda bali ameshikwa na shetani na yeye mwenyewe hajielewi..lakini kama leo tungesema hatutaki kutumiwa na shetani kuharibu ndoa za watu kweli wanaume wangejirekebisha lakini kwakuwa na sisi tunakubali kutumiwa katika mipango ya shetani kwa kutupa matatizo kibao ambayo tunajuwa tutatatuliwa na wame za watu tunajikuta tunajiingiza katika mpango wake wa kuharibu ndoa..maana shetani ameshajuwa sasa hivi mahali pa kushindana na MUNGU ni kwenye ndoa hapo ndio anapata wafuasi wengi maana watu sio wavumilivu tena, watu wanapenda maisha ya haraka ukikutana na viserengeti boys vinapendeza kwasababu ya mke wa mtu mmama mtu mzima utashangaa na ukikutana na msichana mdogo anamkatikia kiuno mbaba anayeweza kumzaa mara mbili utashangaa..ukimkuta kijana kaoa hana hata mwaka analala nje ya nyumba yake utashangaa ukikutana na mwanamke aliyeolewa anakumbatiwa na kukatiwa kiuno na mwanaume aliyeoa ambaye sio mume wake utashangaa..huu wote ni mpango wa shetani na wengi tumeingia, wameingia na bado wanaendelea kuingia bila kujijuwa...haijaanza jana wala haitaisha kesho MPAKA UTAKAPOJITAMBUA NA KUTAMBUA UMUHIMU WA HIYO NDOA ALIYOKUPA MUNGU NA UTAKAPOJITAMBUA THAMANI YAKO KAMA MSICHANA SIO KUTUMIWA HAPO TU NDIO DUNIA ITABADILIKA ZAIDI YA HAPO bado tupotupo sanaaaaa

Wednesday, August 14, 2013

Juwa ya kwamba...

Kila mtu anaingia kwenye ndoa kwa malengo ya kwamba ndoa yake idumu milele, wazae watoto na wafurahie kuwalea pamoja, ni furaha ya kila binadamu unapopata ndoa, tunapofika kwenye ndoa pale ndio balaa zinapoanza pindi ambapo mke anataka afanyiwe hivi na mwanaume anataka afanyiwe hivi tunaposhindwa kukutana katikati katika kukubaliana tuishi vipi ndio balaa zinapoanza, wanawake tunapoingia kwenye ndoa tunataka kupendwa, unithamini, utumie muda wako mwingi kuwa na mimi mwanamke anataka kumuhudumia mumewe muda wote wawe kwenye furaha mwanamke anaacha kila alichokuwa nachokibaya zamani akiolewa wanaume wa mwanzo wote wanapigwa chini akili yake ni kwa mumewe tu, mwanaume je yeye anaingia kwenye ndoa kwamba sasa ameshakuwa anataka kuwa namaisha yake awe na nyumba yake na mkewe, afuliwe, apikiwe, mpate watoto aheshimike kuitwa baba lakini je anakuwa ameachia wanawake wake wa nyuma au anakuwa amejipanga kwamba mpaka kufa ni mimi na mke wangu hapana, wanaume wengi ndoa ni step tu nyengine ya maisha sio kwamba ndio wamefungwa wasiwe na wanawake nje japo wanajuwa hairuhusiwi lakini wengi hawawezi..sasa pale mwanamke unapokuja kugundua mumeo ana mwanamke nje ndipo unapoanza kuchanganyikiwa, kukosa amani ya kukaa kwenye ndoa, mapenzi kwa mumeo yanapungua unajikuta huwezi kumuhudumia tena vyema mwanaume unamaumivu wengine mpaka wanakonda na kuumwa hadi kulazwa, wengine wanaona haifai kama kaniona wa nini na mimi nitamuona wakazi gani unaamua kuacha ndoa yako na kuondoka, huku labda ukiwa na mwanao ndoa unaiacha kwa maumivu na majuto laiti ningejuwa asingenioa..kama huyu ndio atakuwa mwanaume wako wa mwisho basi hata mimi nakushauri uondoke lakini kama bado baadae utataka kuwa na mwanaume mpaka utakapokutana na mwanaume ambaye kweli yupo tayari kukaa chini na mwanamke mmoja na kumtumikia basi wanaume wote wapo kama mumeo unayemuacha utamkimbia tena na tena na tena utakimbia mara ngapi?????? hakuna aliyesema ndoa ni rahisi toka enzi za biblia ndoa ni ngumu,majaribu,mapito na kukata tamaa lakini ukimruhusu aliyekupa ndoa aisimamie hata ukipita magumu gani atakuonyesha jinsi ya kutokea maana yeye sindiye aliyemuumba mumeo na mkeo basi anajuwa jinsi gani yakumuweka sawa..TAFAKARI HILI UNAPOFIKIRIA KUOLEWA AU KUOA MAANA KUNAWANAUME PIA AMBAO NDOA ZAO ZINAWAKA MOTO WAKE ZAO HAWAKAMATIKI...

Word...

Nani kakuambia kuwa sababu tu mtu anaimba praise madhabahuni basi hawezi kuwa HIV+?
Nani kasema kuwa sababu tu mtu ameokoka tangu shule ya msingi basi hawezi kuwa hiv+?
Kuhubiri, kuvaa nguo ndefu, kuomba kwa machozi mengi, kuvaa tai, kuokoka hakumuondolei mtu possibility ya kuwa HIV+.

Vijana wengi siku hizi tena wanaosema wameokoka wanashiriki tendo la ndoa kwa kigezo kuwa wamekubaliana kuoana hivyo haina tatizo. Wamezoelea dhambi kiasi kwamba dhamiri zao haziwasuti na wanaendelea na huduma. Hofu ya Mungu imewaondoka kabisa. Muogope Mungu, kimbia dhambi, ishi maisha matakatifu hata kama watu watakucheka na kukuona mshamba. Tafuta kumpendeza Mungu na sio wanadamu.

Source:Woman of Christ

Makubwa...


MWANAFUNZI wa kidato cha pili jina kapuni (16), amejikuta akiozeshwa na wazazi wake kwa mwanaume aliyetambulika kwa jina la Kaizilege Jabiri (31) ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, Risasi Mchanganyiko linakupa habari.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu jijini Dar nyumbani kwao Mlandizi, Bagamoyo, Pwani ambako mwanaume huyo alifunga ndoa na binti huyo na kurejea naye nyumbani kwake, Ubungo Kisiwani, Dar huku baadhi ya watu wakihofia uhai wa ndoa hiyo.
Baada ya kuanza maisha ya ndoa kama mke na mume, Agosti 6, mwaka huu taarifa zikafika kwenye Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo maafande walisema hiyo haiwezekani.
“Polisi walipopata habari walisema hakuna ndoa hapo, wakajipanga kwenda kuvamia nyumbani kwa wanandoa hao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliongeza kuwa, nje ya nyumba hiyo walimkuta msichana huyo anapika huku kaka yake akiwa kajipumzisha ndani akisubiri lishe hiyo.
Kaizilege alipobanwa alikiri kuwa mwanafunzi huyo ni mkewe walifunga ndoa ya Kiislamu, Mlandizi. Kwa kuwa kisheria ni kosa kuoa mwanafunzi aliye chini ya miaka 18 alilazimika kupelekwa Kituo cha Polisi, Magomeni, Dar.
Kwa upande wake mwanafunzi huyo alikiri kuolewa na kaka yake. Alisema yeye ni mwanafunzi, yuko kidato cha pili Mlandizi. Alisema hakuwa na maamuzi  ya kuikataa ndoa hiyo kwani uwezo huo ni wa wazazi wake.
Denti huyo alizidi kuweka wazi kwamba, chanzo kikubwa cha kuozeshwa kwake ni kutokana na ugumu wa maisha ulioko katika familia hali iliyomsukuma baba yake mzazi kumshawishi aolewe na kaka yake.
Alisema kuwa aliambiwa atakapoolewa, mumewe  huyo angeendelea kumsomesha jambo ambalo halikufanyika.
‘’Mimi nilikubali niolewe ili baadaye nipelekwe shule kwani wazazi wangu hawana pesa za kunisomesha na mimi siwezi kukataa kwa sababu wazazi ndiyo wameamua,’’ alisema.

VYANZO VYA HABARI
Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya ndugu, dini ya wawili hao inaruhusu kumuoa mtoto wa mama’ke mkubwa  endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka 18 haki ambayo kwa mwanafunzi huyo haipo.
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na msemaji wa dawati la jinsia Wilaya ya Kinondoni, Dar, Inspekta Prisca Komba ambapo mhusika mmoja alisema:
‘’Kwa mujibu wa sheria na taratibu za utamaduni wetu si ruhusa kuoa mtoto wa mama mkubwa tena akiwa bado mwanafunzi, mimi naona ni kuvunja sheria na ni lazima huyu bwana afunguliwe jalada la uchunguzi.”
Kaizilege amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa Kumbukumbu MAG/RB/9015/2013, mara uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


Tuesday, August 13, 2013

Thamani yako kwake...

Thamani yako kwa mpenzi wako unaijua siongelei na nyie wenye wapenzi wame za watu au wake za watu  kwakuwa huyo sio wako ni wa mwanamke na mwanaume  mwengine, ila wewe mwenye mumeo, mkeo au mpenzi ambaye sio wa kukopa unaijuwa thamani yako kwake, unapokuwa naye anakuaje, anakuitaje na anakuchukuliaje..anakupenda,anakuthamini, anataka kila mtu ajuwe wewe ni nani kwake au mkitoka kwenda sehemu anakaa tu kimya hata marafiki zake au watu wanaomjuwa wakimuona hakutambulishi kwa heshima..kama yupo hivyo hilo ni TATIZO lifanyie kazi lazima ujuwe thamani yako kwa mpenzi wako mimi mume wangu ananiita MALKIA na anamapenzi ya ajabu kwangu yani nikiwa naye sehemu mpaka mimi mwenyewe naona aibu kila mtu anayemjuwa atatambulishwa huyu ndio mke wangu, malkia wangu mama wa watoto wangu wawili hata tukiwa bar kuna bar ya jirani na kwangu kila mwanamke anamsifia na kumshangaa mume wangu ila sasa hivi walishamzoea utasikia tu huyo huyo kaoa bwana hakuna mwanaume aliyeoa mtaani zaidi yake maana yeye kutwa mkewe... je wewe unajuwa thamani yako kwa mumeo/mkeo/mpenzi wako...kila mwanadamu anamapungufu yake lakini ni vitu vizuri na vidogo kama hivi vinakufanya uzidi kumpenda na kutaka kuendelea kuwa na kusihi naye...

ARUSHA,ARUSHA,ARUSHA...

Wakowapi mashoga zangu wa Arusha jamani narudi tena kufunda arusha niliwaahidi nitarudi natimiza ahadi yangu nitakuja mwezi wa kumi MUNGU akipenda nitawajuza hotel na tarehe siku zijazo kwa jinsi nilivyowasoma siku zile wanawake wa Arusha bado mnakazi sana kuna mambo mengi sana bado mnayahitaji sasa basi wakati huu nikija nitafaya tofauti wanawake wote mnaohitaji kufundwa nitawafunda private ndio tutakutana hotel fulani chumbani miye na somo yangu tutakuwepo kuwapa darasa tutakaa siku tano kwa ajili yenu hii ni ya kiutu uzima zaidi utafurahi..nachukuwa order za watu wanaokuja kufundwa kwanzia sasa na ninakupangia siku yako na muda kama kawaida yetu kiingilio ni 30000/= na bidhaa zote tunazotumia kufundia zitakuwepo hii sio ya kukosa kwa kuweka nafasi yako nipigie 0717 019320 natumaini hata wa Moshi pia na sehemu za jirani mtaweza kuhudhuria, usimuache wifi yako, shoga yako na yule jirani yako......

Karibuni sana 

Monday, August 12, 2013

MWANAMKE: nataka niongee na wanawake ambao wapo kwenye mahusiano ambayo yanaelekea kwenye ndoa na pia wanawake ambao wapo kwenye ndoa jamani aihusu kabisa wewe kumwambia mwanaume wako mambo ya nyumbani kwenu ambayo unaona hayana faida ya yeye kuyajua, yani kunawanawake hawana siri kila kitu cha kuhusu maisha yake wanamwambia mwanaume mengine ni aibu kabisa mwenyewe unasema oohhh namwambia ili akija kusikia asidhani nimemficha jamani hebu chuja ya kumwambia mwanaume kwasababu kama hujui wanaume wanatumia mabaya na mapungufu yako na familia yako kama fimbo ya kukuchapia wewe baadae ndani ya ndoa nitakupa mfano " mpenzi yani hapa ninahasira baba jana karudi saa nane za usiku akaanza kugombana na mama akampiga kweli" atakwambia pole basi utajibembelezesha yataisha sasa amekuoa wewe ikafika siku na yeye akarudi saa nane za usiku mara tena wewe ndio umevimba na kununua kwa hasira unamuuliza na kutaka kugombana akakujibu "unanisema mimi narudi saa nane za usiku mbona wewe baba yako anarudi saa nane za usiku ulishawahi kusikia mama yako anagombana na kumtukana bora mimi narudi nalala sianzishi ugomvi na kukupiga"...nadhani mmenielewa hayo na mengine mengi ambayo tunawaambia wanaume chuja ya kumwambia mwanaume asitafute fimbo ya kukuchapia..

Mama mkwe Part 2....

Jamani hapa nataka tuongelee mama wakwe wenye gubu na masimango yani jamani kuna mama wakwe wengine hata uwapende vipi hawapendeki yani wao kero tu muda wote.

Kwanza kabisa japo namatatizo yake na masimango yake wakati mwengine japo unahamu ya kumtukana, kumfanyia madharau ninakusihi kwanza, usijaribu hata siku moja kufanya hivyo na unatakiwa kwanza kumuheshimu kama mama yako na pia kumchukulia msalaba wake wa mapungufu yake.

Unachoweza kufanya wewe ni kukaa kimya na kumuhudumia vyema mmueo usimpe nafasi ya kuwa asilimia 100% kwa mama yake anatakiwa awe 50% tu japo ndio anampenda sana mama yake lakini mapenzi zaidi yanatakiwa kuwa kwako kwani wewe ndio mtu ambaye upo naye zaidi baada ya kumuacha mama yake.

Mama wakwe wengi wanakuwa na roho mbaya kwasababu wanahisi kwamba pindi mtoto wake akioa basi huduma na attention kwake tena ndio hamna yote anapeleka kwa mkewe ndio maana anatumia ubabe kupata attention kwa mwanae.

Wanawake wengi wanapokosea ni kuwadharau mama zao wakwe wa aina hii unapomdharau mama wa mumeo usitegemee mumeo atakupenda wewe zaidi, tena mama mkwe wako atakusingizia maneno kibao kwa mumeo mara tena ndio mnaanza kugombana mwanaume hashikiki tena kurudi nyumbani na vituko vingine kibao, na usimpelekee mumeo matatizo ya mama yake hawapendi hao viumbe yani wewe ndio utaonekana huna adabu na umpendi mama yake.

Anapokuja nyumbani kwako akusonye, akutukane,akusingizie vibaya, hata akuteme mate usinyanyue mdomo wako kumtusi wewe miaka inaenda tu ukihudumia mumeo na watoto na nyumba yako itafika sehemu tu mwenyewe atakaa sawa maana wakiona watoto wao wanatunzwa vizuri ile chuki hugeuka kuwa upendo na kuanza kukuamini na kukupenda.

Kwani hukusikia kuna msemo unaosema anayekudharau siku moja atakusalimia kwa heshima???? hata mama mkwe wako naye ni mmoja wao.


MWANAMKE: katika maisha wewe unanyota na baraka za kumuwashia au kumzimia mwanaume mwanga wake wa kuonekana katika dunia,hii haswa ni katika ndoa pindi mnapokaa zaidi ya mwaka pamoja katika nyumba moja na maisha yenu kuwa kitu kimoja, je hujawahi kumjua mtu ambaye alikuwa na maisha mazuri,kazi nzuri na hela mwanaume alikuwa ng'aring'ari lakini ghafla alivyomuoa msichana fulani nyota yake ikazima, akawa wa hovyo kabisa, kazi kafukuzwa, kama ni biashara haina faida mpaka anafunga, magari na nyumba anauza..na je umeshawahi kumuona mwanaume wa kawaida tu alikuwa anajimudu yeye tu lakini baada ya kumuoa msichana fulani sasa hivi anang'aa, anahela ana nyumba na magari..umeshawahi kuona vitu hivi..tambua wewe mwanamke ndio kiini kikuu katika maisha yako na mumeo uwezo wote unao wewe huku ukiomba kwa MUNGU azidi kuwasaidia...unapokuwa tayari kwa kuwa mke wa mtu muombe MUNGU akuandae ukawe nyota itakayong'aa na kila mtu akiiona apate kutambua uwepo wako katika maisha ya mumeo na kama wewe ni mke wa mtu na hukutambua umuhimu wa nyota yako basi muombe MUNGU akakung'arishe upya leo ukapate kuonekana.

Mama Mkwe Part 1......

Leo nataka niongelee kuhusu MAMA MKWE nataka niguse upande wa wanawake ambao ndio sugu na ndio tatizo katika ndoa nyingi na haswa hizi changa, ndoa nyingi zinakuwa na migogoro na mama wakwe kwakuwa wanawake wengi huingia kwenye ndoa wakiwa tayari wanajuwa kwamba siku zote mama wakwe ni wabaya na kwamba siku zote watakuwa upande wa watoto wao wa kiume na sio upande wako.

Kwa asilimia kubwa hii sio kweli ila sisi tunaoolewa ndio huwa tunaleta chokochoko zinazofanya sasa tugombane na mama wakwe, japo jamani kuna mama wakwe wengine wanagubu utakuta msichana wa watu anampenda kweli mama mkwe wake lakini mama mkwe hapendeki gubu mtindo mmoja.

Mnapooana mnakuwa kitu na mwili mmoja inamaana familia ya mumeo ni yako na familia yako mumeo ni yake, mapenzi uliyokuzwa nayo kwenu ndio hayo ukayapeleke kwa mumeo na mumeo hivyohivyo, mama yako kwa jinsi ulivyokuwa unampenda na kumuhudumia ndio hivyohivyo unavyotakiwa kumuhudumia mama mkwe wako na kumpenda.

Kuwa naye free jamani mimi nasikitika wakati naolewa mama mkwe wangu alikuwa ameshatangulia mbele za haki lakini laiti ningemkuta najuwa tungependana mume wangu mwenyewe angeomba poo maana mume wangu ananiambiaga katika wanawake waliolewa kwao kama mama yake angekuwepo leo basi angenipenda sana kwanini kwasababu mume wangu anaona jinsi ninavyoishi na ndugu zake ndio maana anaamini hivyo.

Turudi kwa mama mkwe, ndio najuwa yule mama ndio umemkuta tu ulivyokuwa mkubwa na kuolewa unajiuliza utaanzaje kumpenda kama mama yako, jamani hebu fikiria yule mama mkwe wako alivyojuwa anamimba ya mumeo aliitunza miezi tisa tena kipindi hicho kulikuwa hamna kudeka na hospital na mambo ya uzazi ya kisasa kama ya leo utakuta mama wa watu miezi tisa alivyombeba mumeo alipata tabu sana sio tu ya kiafya hata na baba mkweo labda kailea mwenyewe mimba ya mumeo, labda hakuweza kujifungulia hospital kwasababu ya tabu ya usafiri akajifungulia nyumbani, huku anafanya kazi zake za kumuingizia kipato huku anamnyonyesha na kumlea mumeo..

Kama tunavyojuwa sisi tuliozaa watoto wa kiume ndio hivyohivyo mama mkwe wako hakulala siku saba za mwanzo akimuangalia kwa makini mumeo kitovu kisidondoke kwenye uume wake akashindwa kukupa raha za kitanda alianza kulala vizuri baada ya kitovu kudondoka vyema...leo tena shoga umeolewa ndio unamletea dharau mama yako kisa wewe ndio ubavu wa mwanae inahusu...

Unajitutumua mtoto wa kike ukisikia mama mkwe anakuja nyumbani unavuta mdogo kama unalamba mbilimbi cha kwanza unaanza kuuliza atakaa muda gani huna haya, badala wewe ukijuwa mama mkwe anakuja ndio ujishauwe tena uhakikishe unampikia vizuri na kumvisha vizuri yani akija kwako asitamani kuondoka na ndio baraka zinakuja ndani ya ndoa yako na nyumba yako tena wewe mama mkwe wako unatakiwa umdekee na kumpenda mwanaye akose la kuongea baya juu yako kwake hata kama umemlaza bila chakula cha usiku ashindwe kukusemea..eboooo

Na ikifika muda anapotaka kuondoka mtoto wa kike juwa kumfungashia mama mkwe wako sio umbebeshe nyanya na vitunguu la hasha mpe matenge jamani kariakoo siku hizi matenge yapo ya kila aina bei rahisi nunu hata matatu manne mpe mama mkwe wako unadhani ukimtumikia vizuri atapata la kukutafuta hapana jamani.

Na kwawale ambao mama wakwe zenu hawapo mikoani wapo mjini pia unaweza ukawa unampelekea zawadi yani katika mshahara wako au faida zako za kila mwezi uweke na fungu la mama mkwe mpe raha mama mkwe wako usimzoee ikapitiliza lakini mzoee kama mama yako mtoe out dinnder, dance mnunulie vitu vizuri..jamani sisi sote tunapenda na kuwapenda watu wanaojuwa kututunza vizuri hata kama wanamatatizo yao tunayavumilia kwakuwa anajuwa jinsi ya kukutunza, ndio hivyohivyo mama mkwe wako atakupenda na kukuvumilia ukijuwa kumtunza na kumpenda vizuri..

NA UTU UZIMA WOTE ULIO NAO HUJUI KULA NA KIPOFU...

Sunday, August 11, 2013

Tumejikongoja kidogo..

 Jumanne nilituma post kuhusu huyu baba anayeomba masaada wa fedha ili aweze kupata ticket na passport kwa ajili ya kwenda India kumtibia mwanae ashura ambaye ana cancer ya ngozi...

Kwa uwezo tuliokuwa nao mimi na marafiki zangu wengine tuliweza kujichangisha kwenye group yetu ya wanawake ya Reserve ikiongozwa na admin wetu shoga yangu kidawa Lamkeku tukaenda zetu mpaka mkuranga huko kupeleka hela kwa kina Ashura.

 Hali ya Ashura kwakweli ni mbaya vidonda vinatoa harufu na kuanza kuoza, ila bado naamini MUNGU yupo upande wake watakamilisha na kumsafirisha huyu mtoto akatibiwe...na wewe kama umeguswa na ugonjwa huu please rejea post yangu ya nyuma ya msaada kuna number ya simu ya baba yake ashura umtumie kidogo ulichokuwa nacho MUNGU atazidi kukubariki...

Tuesday, August 6, 2013

Mwanamke unapofikiria kuolewa...

Kuna umri ukifika mwanamke unataka kuolewa, uwe na watoto na mji wako lakini kabla hujapata hivi unajitunzaje kama mwanamke anayetaka mume, na unampataje huyo mwanaume wa kukuoa, ama wewe ndio wale wanaokuwa na wanaume watatu au zaidi wakiangalia yupi ataoa unakula huku na huko, au wewe ndio yule mwanamke unayekuwa na mahusiano na mume wa mtu wakati unangojea wako,au ni wewe mwanamke uliyemuachisha mume mwanamke mwenzako ukisubiri kuolewa wewe...wengi wetu ndoa zetu hazitufikii kwa sababu ya majanga kama haya, tunajiachia sana kuchezewa na wanaume mpaka nyota yetu na baraka za kuwa wake zinafifia, wakati unasubiri kuwa mke mwema wa fulani jifunze kumuomba MUNGU akupe mume wa ubavu wako wa kutoka kwake ni sala tu ndio itakupa wewe mume na ndoa yenye matunda mema na kama una mwanaume mmoja muombee mwanaume wako kama kweli ni mumeo akuoe na kama sio badi MUNGU amuweke pembeni asimzibie njia mumeo aliyenjiani kuja kwako..Mwanamke kataa kuchezewa na kuchakazwa na wanaume wewe ni mtu wa thamani sana.

MSAADA PLEASE.....

 baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT,

kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.


“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765, ili kumpeleka India kwa matibabu

MUNGU WA MBINGUNI AWAGUSE.. KUTOA NI MOYO.. TOA CHOCHOTE ULICHONACHO..... KITAMSAIDIA SNA HUYU BABA.. HATA TUKISEMA TUOE ELFU MOJA MOJA, JAMAN ITAMSAIDIA.... UWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII NAHISI KUCHANGANYIKIWA

Word...

Baadhi ya wasichana wanapoona maisha ni magumu, kila analojitahidi kufanya halifanikiwi, hakuna pa kukimbilia wala msaada wanaona lililobaki ni kuolewa. Wanafikiri kuolewa kutawaondolea matatizo waliyonayo, watapata mahali pa kuishi, mtu wa kumtunza, atafanya analotaka na kila alilokuwa analitamani atalipata. Wanaingia kwenye ndoa kukimbia matatizo waliyonayo, wanaingia kwenye ndoa wakimuona mume kama mzazi wa kumtunza. Wanapokuta hali sio kama walivyotarajia ndoa inaishia kuwa ndoano na msalaba usiobebeka.
Usione maisha ya ndoa ya fulani ukayapenda ukajua nawe itakuwa hivyo. Usitumie mfano wa fulani nawe kufanya jambo. Hujui mtu huyo amepitia na anapitia nini. Mungu pekee ndiye kimbilio na msaada, zaburi 46:1-2. Usifanye uamuzi mkubwa kama kuolewa sababu ya matatizo yanayokuzunguka, hiyo sio sababu kabisa ya kuingia kwenye ndoa. Matatizo yapo kwa wenye ndoa na wasio na ndoa na msaada wa wote ni Mungu. Jifunze kumtegemea Mungu 100% kabla hujaingia kwenye ndoa.

Source: Women of Christ

Monday, August 5, 2013

Zivunje....

Leo nataka tuongelee laana za kurithi..wengi tukifikia hapa tunajisahau kabisa haswa kwenye mambo ya ndoa na uzazi, wakati unataka kuolewa je unakuwa umevunja laana za ulipotoka?? na ulipo je umevunja laana za wazazi na mababu ambazo zimekuwa kwenye damu yako??? unajikuta mtu umepata mume unaolewa halafu mama yako hajawahi kuolewa na babu yako alioa wake watano wewe inakuweka wapi sawa unajihisi mwenyewe unabahati lakini je kwanini watu wako nyuma hawakufurahia maisha ya ndoa????au wewe mama yako alikuwa na baba yako akaachika akapata mwanaume mwengine akaolewa na kwa huyo baba alikuwa mke wa pili na wewe mtoto wake umepata mume unataka kuolewa umevunja laana???? au unaolewa na mwanaume ambaye amelelewa na mama tu kwakuwa wazazi wake waliachana kwa sababu ya umalaya, au uchawi je umevunja laana?????... ndoa nyingi zinakuwa hazidumu sio tu kwa umalaya pia laana sasa kwenu nyie hamna hulka ya kudumu kwenye ndoa, mama yako ndoa hana, kaka zako wameachika, dada zako hawana ndoa wewe utaipataje na kudumu kwenye ndoa???? mama yako alikuzaa wewe tu, mama yako mkubwa hajawahi kuzaa mjomba wako anawatoto wawili tu wewe unaingia kwenye kwenye ndoa una mwaka wa tatu hujazaa umevunja laana?? kwenu hakuna hata mtu aliyedumu kwenye ndoa leo wewe umeolewa umezaa watoto je umewavunjia laana katika maisha yao maana MUNGU alisema nitakulaani wewe na uzazi wako wote!!!jamani tunavunja laana..mama yako alipata mimba akifanya umalaya humjui baba yako umalaya ukakusomesha mpaka hapo ulipofikia na wewe unatafuta mume je umevunja laana??? matatizo mengi sana tuliyonayo katika maisha yetu ni kwa sababu ya laana tulizo ridhi kutoka wa mababu na wazazi wetu tujifunze kuvunja laana ili tusihi kwa raha na kuweza kudumu katika ndoa pia tuheshimike kwa jamii...

Itakusaidia...

MWANAMKE katika mahusiano yako usiogope mpenzi/mume wako kuwa na hawara, wala usitumie muda wako kuanza kumchambua mwanamme,kumfwatafwata na kutaka kujifanya kama wewe ndio mama yake umcontrol maisha yake wanaume hawapendi mwanamke wa aina hii..kaa tulia tunza penzi lenu, jiheshimu,mpende beba mapungufu yake kama msalaba wako, mpendezeshe, jifunze kumridhisha kila idara kwa kiasi...mfanye mwanaume wako ajuwe hawezi kuishi bila wewe, awe anakuhitaji kama hajakuoa akuoe na kama amekuoa ashindwe kukuacha..hapo ndipo atakusifu na watu wote watajuwa wewe ni mke uliyetoka kwa MUNGU...kila mara jitahidi kumpenda kama hujawahi kupenda tena yani awe na furaha akiwa na wewe na kutaka kila mtu ajuwe umuhimu wako kwake....hayo mambo ya hawara na kufumaniana ni ya mpito tu mwisho wa siku ni wewe na yeye na mapenzi yenu umeweza kutunza kiapo ulichoweka siku ya ndoa, umeweza kumtunza mume na watu wakaona kweli ametunzika, watoto wenu mnawalea kwa maadili ya MUNGU, wewe mwenyewe unajiheshimu kama mke wa fulani????????....TAFAKARI

Tafakari

Ulitoa mimba. Mimba zaidi ya moja. Hukuona kama ni big deal. Sasa jambo hilo linakusumbua, linakukosesha amani, ukilala unasikia sauti ya mtoto analia. Umekata tamaa maana hujui la kufanya wala wa kumwendea. Pengine umeolewa na unawatoto lakini huna furaha nao ukikumbua yule uliyemkatisha maisha. Pengine hujapata mtoto tena. Unaona kama Mungu amekulaani sababu ya mimba ulizotoa. Huoni pa kushika, mbele giza nyuma giza.
Mchana wa leo nakuambia LIPO TUMAINI! Bwana Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu zote! Hakubakiza nyingine! Wewe unalopaswa kufanya ni kumpa maisha yako, mkabidhi ayatawale. Tubu kwa makosa yote uliyofanya, na kumkiri Yesu kama Bwana na mwakozi wa maisha yako. Yeye anasamehe kabisa na hatakumbuka tena. Anza maisha mapya na Yesu naye atakuponya na majeraha yote ya nyuma.
EZE. 18:21-23, 31-32 
Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi.

Source: Women of Christ

Thursday, August 1, 2013

wanawake...

Leo nataka niongee na wanawake wanaotoa nyuma, jamani kutoa nyuma ni maamuzi ya mtu na starehe zako, wanawake wengi wanaponzwa na wanaume kuwapa nyuma na wao bila kufikiria wanadhani kumpa mwanaume nyuma ndio nitamuweka mkononi nani kakukwambia mwanaume anawekwa mkononi, matokeo yake wanawake wanaharibika mwanamke utamkuta mzuri akivaa anapendeza kumbe hana bikra ya mbele wala ya nyuma, sitetei kutoa nyuma lakini bora utoe nyuma lakini upo kwenye ndoa kuliko utoe nyuma hujaolewa matokeo yake ukiachika unapata tu aibu na wanaume wanahadithiaga unajipatia tu aibu...MWANAMKE usidanganyike ukatoa nyuma kama kukunyonya akunyonye tu lakini sio aingize dude lake humo..na kama wewe ni mwanamke na umeshaliwa sana nyuma na huipendi hali hiyo na imekuletea madhara kuna dawa imesaidia kukaza mbele inaweza pia ikakusaidia kukukaza nyuma nipigie 0717019320....

Nimeitoa sehemu...


Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.. Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????

Mtenda akitendwa.....

   WANAUME bwana yani mtendwa akitendwa....yani mwanaume yeye ndio atoke nje ya ndoa ukitoka wewe unauliwa huyu baba amemuua mke wake baada ya kujuwa mkewe anamahusiano nje ya ndoa yao kisha na yeye kujiua wameacha mtoto wa miaka 3 .....R.I.P