Thursday, April 28, 2016

Tuongeemahusiano - Visa Vya Mume wa Ndoa

Monday, April 18, 2016

Tuongeemahusiano

Vikwazo katika ndoa, nilitembelewa na rafiki yangu ofisini tukawa tunaongelea vikwazo vya ndoa moja ya vipindi vyangu youtube, je wewe una vikwazo vinavyokufanya usioe ama usiolewe?? ni Vipi???

Monday, April 11, 2016

INSTAGRAM...

Wapendwa najua nimekua kimya sana ni kwasababu sasa napost sana Instagram, kwa wewe ambae una acc unaweza ukanifollow @tuongeemahusiano  na huko utafurahia post nyingi sana za mahusiano kama ulivyokua unafurahia hapa, lakini pia hapa utafurahia sana za kwanjia ya video ambazo nitakua nazipost mara kwa mara.

Ahsanteni

TuongeemahusianoBWANA YESU Asifiwe, wapendwa nawakaribisha katika youtube channel yetuwww.youtube.com/rosemarymizizi mpate kujifunza mengi ya kuhusu Imani na Mahusiano, kila wiki tunaweka kipindi kipya ili upate kujifunza zaidi ila pia tutawawekea hapa link ya kipindi kipya tutachokua tunaweka kwa urahisi kwako....Karibuni sana

Wednesday, May 27, 2015

AM BACK.....

 AM BACK BABY..... yeeeeuuwww nawasalimu wote kwa jina la MUNGU wetu aliye juu, natumaini wewe na familia yako nyumbani ni wazima na MUNGU wetu amezidi kua mwaminifu kwenu na kuendelea kuwapa baraka zake tele juu yenu, mimi na familia yangu hatujambo tunamshukuru kwakua amekua na anaendelea kua mwema tunazidi kumuona akitutendea miujiza mikubwa sana kwetu, na kila ninavyoendelea kumshangaa MUNGU ananiambia bado sijamaliza na wewe maana nikimaliza na wewe kila mtu atajua ya kwamba mimi ni MUNGU wako
Nimekua busy sana na projects nyingi zangu zitakazokuja, nakuombea uhai na afya njema ufurahie pamoja nasi japo nina mambo mengi sana naendelea kufanya nje na hapa sasa nimerudi kuendelea na hii baraka yangu ambayo MUNGU alinipa kabla

Sunday, February 15, 2015

jamani moyo unaniuma mimi kila nikifikiria natamani kulia......

yani hizi mali hizi siku hizi au ilikua tokea zamani..jamani mpaka namuonea huruma huyu dada huyu dada walizaliwa watatu kwao wasichana wawili na mvulana mmoja

mama yao alifariki na baba yake kuona yupo peke yake kwenye nyumba kubwa akaamua kurudi kijijini kwao kumalizia uzee akawaachia watoto wake nyumba yake kuwa ni urithi kwao nyumba ni kubwa na inauwanja mkubwa tu

mwanzoni wakaa vizuri sana huyu kaka ameoa anakaa hapohapo na mkewe na watoto wake wanne, hao wasichana mmoja kazalia nyumbani tu mtoto mmoja na mwengine pia kazalia nyumbani watoto wawili

huyu kaka majirani wanasema anapenda sana mambo ya kishirikina haswa kuwafanyia ndigu zake ili awadhurumu mali na ukiangalia ni watoto wakike ambao ni wanaishi tu uswahilini na maisha ya uswazi labda hawajui hata maana ya haki za mwanamke na kama kuna watu wanaotetea wanawake kisheria

basi katika wale wasichana wawili mmoja akaamua kuhama na kwenda kupanga mbali lakini upande wake wa nyumba bado ulikuwepo tu, kwahiyo kwenye nyumba akabaki yule msichana mdogo na kaka yake pamoja na familia yake

mdada wa watu huyu alikua hana kazi nyengine zaidi ya kuajiriwa salon, lakini watu walikua wanashangaa yeye ndiye alikua analisha familia yote hiyo kubwa kaka yake hafanyi anabaki tu kuendeleza kujenga nyumba vyumba ili apangishe ikawa hivyo kwa muda mrefu mtaani wakaanza kusema kamfanyia mdogo wake chuma ulete siunajua waswahili tena

basi maisha miaka nenda rudi ndio hivyo kwao watu nje wanasikitika tu na kuongea chini kwa chini mashoga wa shisti wakimueleza anaona wanamsema majungu anaenda kukusemea kwa kaka yake unachambwa kwanzia na kaka mtu mpaka mtoto wao siunajua tena maisha yetu ya uswazi mabibo kwahiyo watu wakawa wanapotezea na kuongea chini kwa chini

ghafla huyu msichana akaumwa sana bila kaka yake kuonyesha mahangaiko yoyote ya mdogo wake ili apone mpaka yule dada yake mkubwa ndio kuacha chumba chake huko alipokua kapanga kuja kumuuguza mdogo wake mpaka alipokata roho

basi msiba ukafanyika watu wakazika maisha yakasonga sasa miezi mitano sasa tokea mdogo wao afe, yule dada aliamua kubaki pale ili amlee yule mtoto mdogo ambaye yupo la kwanza aliyefiwa na mama yake

basi yule kaka mtu hata shs mia hampi yule mtoto, maisha yao wenyewe ya kawaida kinachouma watu mama yake ndiye alikua akiilisha familia ya kaka yake leo hayupo mtoto wake wamemtupa wamemuachia huyo dada yao ambaye na yeye maisha yake ya kawaida sana, ndiye anayekaa naye hata kumsaidia chakula maharage matupu hamna yule dada wa watu akienda kubangaiza huko akipata ndio wale akikosa walale..

halafu juu ya hapo yule kaka akampigia baba wa mtoto njoo umchukuwe mwanao anapata tabu huku anateswa sana baba wa watu kuja mputa kumchukua mwane kwenda naye kwa ndugu zake ila ndugu zake wakamsihi amrudishe kwa huyo mama kwani kwa kumuangalia tu mwili mtoto anaonekana kanenepa na kupendeza kuliko hata mama yake mzazi alivyokua hai...yule mtoto akauridishwa

ndio dada mtu kumuuliza yule baba kwanini umemrudisha mwanao na ulisema huku anapata tabu ndio kuhadithia A mpaka Z yule dada aliumia sana yule kaka alipoondoka ndio kutoka kwenda kumgongea kaka yake kwanini lakini unanitia ubaya hatakama humtaki huyu mtoto ama mimi usinipakazie ubaya na watu wanaoniheshimu

shoga naambiwa mwanamke akanununiwa na nyumba nzima kuanzia baba mpaka watoto wanakaa uwanja mmoja watoto wa baba mmoja mama mmoja lakini hawaongeleshani wala kuombana moto, hata akitaka kibao cha mbuzi anapanda kwetu kwa jirani ama majirani wengine anaomba anakuna anapika

nyumba yule kaka nje kaweka maji lakini huyu dada haruhusiwi kuchota anachota mtaa wa pili huko ya kulipia na akichota kwa kaka yake anatakiwa kulipia kama mtu mwengine

sasa ukaanza ugomvi huyu kaka anamfukuza dada yake kwenye ile nyumba ya marehemu aichukue yeye apangishe, ndio balaa lilipoanza dada yake anamuuliza kwanini upangishe wakati nipo hapa kumlea na kuhakikisha huyu mtoto anapata haki zake alizoacha mama yake

shoga yule kaka asianze kumpiga dadake yani kama kalogwa hivi huyu kaka kampiga sana mpaka akaanza kumkaba sijui alikua anataka kumuaa kamkaba sana kooni basi familia ya huyu kaka inashangilia tu mtoto wake wa kike yupo form two sijui anashangilia muue kabisa baba muue kabisa kakabwa msichana wa watu kujipindua huku na kule ndio kuweza kuporonyoka na kukimbia

kufika juu sasa kwa majirani hoi barazani kwa mama mmoja hivi rafiki yake analia kachafuka akiongea mdomoni anatoka damu ndio huku na kule kumsafisha na kuhadithia kilichotokea

wengine wakamshauri nenda polisi wengine anza kwa mjumbe wakaamua kwenda kwa mjumbe kwahiyo sasa kesi ipo kwa mjumbe...nyumbani kule paka na panya hata salamu hakuna

kisa nini mali ama??? na siye watoto ama ndugu tunaoshadadia leo kwa mwenzio kesho kwako yani kale katoto ningekuwepo karibu ningekazaba mabao maana nimeama uswahilini ila kama kawaida mama shughuli lazima nipigiwe kupewa umbea na yaliyojiri mtaani kama mama mwenye nyumba...

******END*******

Tuesday, February 10, 2015

Weeeee ndoa hizi jamani mpaka huruma ila na sisi wanawake tulioolewa tumezidi acha yatukute saazingine.....

WANAWAKE TULIO KWENYE NDOA KWANINI TUNAPENDA SANA KURELAX NA KUJIONA KWAMBA KWASABABU TUMESHAOLEWA BASI TUMESHAFIKA HAKUNA KUACHIKA

 YANI UNAJIBWETEKA KILA IDARA SIO KWA WATOTO, SIO KWA MUMEO NA SIO KWA NYUMBA NZIMA

YANI MAJUKUMU YAKO YOTE KWAKUA UNAMSICHANA WA KAZI UNAMUACHIA MSICHANA NDIO AYAFANYE KWA KISINGIZIO UNAWAHI KAZINI NA UKIRUDI UNAKUA UMECHOKA JAMANI HII TABIA KILA SIKU NAIPIGA MARUFUKU

HUYU MAMA NA YEYE ALIKUA HIVYO KILA KITU ALIKUA ANAMUACHIA MSICHANA WA KAZI AFANYE, MPAKA KUTANDIKA KITANDA ANACHOLALIA NA MUMEWE!!!!

KWELI JAMANI WANAWAKE CHUMBANI KWAKO MSICHANA WA KAZI AKUTANDIKIE KITANDA, AKUDEKIE UKINIAMBIA KUKUWEKEA MAJI KWAKUA MAJI HAYATOKI NA ANACHOTA MCHANA UKIWA KAZINI NITAELEWA LAKINI SIO KUTANDIKIWA WALA KUFANYIWA USAFI

SHUKA UMELALIA NA MUMEO MMEPEANA USIKU MASHAHAWA MENGINE YAKABAKI KITANDANI KWAKUA HUJUI KUMFUTA VIZURI AU WEWE ZIMEDONDOKA KWAKO BAHATI MBAYA UNAACHA SHUKA MTOTO WA WATU ANAKUJA ANATANDIKA ANASHIKA HAYO MASHUKA NI AIBU

BASI HUYU BABA KUMBE ALIKUA ANACHUNGUZA KILA KITU KINACHOENDELEA PALE NYUMBANI NA KUGUNDUA KWAMBA DADA NDIO KAGEUKA MAMA MAANA KILA KITU ANAFANYA YEYE MAMA HANA MUDA

YULE BABA AKAANZA KUVUTIWA NA YULE MSICHANA NA HIVI MTOTO WA WATU ALIKUA ANATABIA NZURI NA MCHAPA KAZI BABA AKAANZA KULA CHINI KWA CHINI MTOTO NAYE HAKUKATAA AKALIKUBALI DYUDYU LA MAMA AKAWA ANAHANGAIKA NALO KWA MAHABA NA NDIO UMKUTE KAFUNDWA WEEE UTAOMBA POOO

IKAENDELEA HIVYO MPAKA MSICHANA WA KAZI KABEBA MIMBA IKAKUA MAMA KUCHANGANYIKIWA MIMBA YA NANI NIAMBIE AMA NIKUFUKUZE BABA AKAMWAMBIA WALA USIMFUKUZE HIYO MIMBA NI YANGU

MAMA WA WATU KUPATA PRESHA NA KUKIMBIZWA HOSPITAL SIKU MBILI JANA NDIO KURUDI NA BABA KUMUELEZA KILA KITU MKEWE ALIVYOKUA ANAONA MPAKA AKAAMUA SAA KWAKUA NILIOA NIPATE MSAIDIZI NA MKE WANGU ANIFANYIE HIVYO VITU NIRINGE NA MIMI NINA MKE MATOKEO YAKE ANANIFANYIA DADA BASI NIKAAMUA NA DADA AWE MKE WANGU

KWAHIYO MTAKUA WOTE WAWILI HAPA WAKE ZANGU, YULE DADA HAKUAMINI AKAWA KAMA KACHANGANYIKIWA AKALIA SANA WATU WAKAMSHAURI AONDOKE TU AKAPUMZIKE AKABEBA KILA KITU CHAKE NA WANAE NA KUONDOKA AKAMUACHIA MSICHANA WA KAZI NYUMBA

TUENDELEE TU KUBWETEKA WASICHANA WAKAZI WATUNYOOSHE

 ****END*****