Monday, August 12, 2013

Mama Mkwe Part 1......

Leo nataka niongelee kuhusu MAMA MKWE nataka niguse upande wa wanawake ambao ndio sugu na ndio tatizo katika ndoa nyingi na haswa hizi changa, ndoa nyingi zinakuwa na migogoro na mama wakwe kwakuwa wanawake wengi huingia kwenye ndoa wakiwa tayari wanajuwa kwamba siku zote mama wakwe ni wabaya na kwamba siku zote watakuwa upande wa watoto wao wa kiume na sio upande wako.

Kwa asilimia kubwa hii sio kweli ila sisi tunaoolewa ndio huwa tunaleta chokochoko zinazofanya sasa tugombane na mama wakwe, japo jamani kuna mama wakwe wengine wanagubu utakuta msichana wa watu anampenda kweli mama mkwe wake lakini mama mkwe hapendeki gubu mtindo mmoja.

Mnapooana mnakuwa kitu na mwili mmoja inamaana familia ya mumeo ni yako na familia yako mumeo ni yake, mapenzi uliyokuzwa nayo kwenu ndio hayo ukayapeleke kwa mumeo na mumeo hivyohivyo, mama yako kwa jinsi ulivyokuwa unampenda na kumuhudumia ndio hivyohivyo unavyotakiwa kumuhudumia mama mkwe wako na kumpenda.

Kuwa naye free jamani mimi nasikitika wakati naolewa mama mkwe wangu alikuwa ameshatangulia mbele za haki lakini laiti ningemkuta najuwa tungependana mume wangu mwenyewe angeomba poo maana mume wangu ananiambiaga katika wanawake waliolewa kwao kama mama yake angekuwepo leo basi angenipenda sana kwanini kwasababu mume wangu anaona jinsi ninavyoishi na ndugu zake ndio maana anaamini hivyo.

Turudi kwa mama mkwe, ndio najuwa yule mama ndio umemkuta tu ulivyokuwa mkubwa na kuolewa unajiuliza utaanzaje kumpenda kama mama yako, jamani hebu fikiria yule mama mkwe wako alivyojuwa anamimba ya mumeo aliitunza miezi tisa tena kipindi hicho kulikuwa hamna kudeka na hospital na mambo ya uzazi ya kisasa kama ya leo utakuta mama wa watu miezi tisa alivyombeba mumeo alipata tabu sana sio tu ya kiafya hata na baba mkweo labda kailea mwenyewe mimba ya mumeo, labda hakuweza kujifungulia hospital kwasababu ya tabu ya usafiri akajifungulia nyumbani, huku anafanya kazi zake za kumuingizia kipato huku anamnyonyesha na kumlea mumeo..

Kama tunavyojuwa sisi tuliozaa watoto wa kiume ndio hivyohivyo mama mkwe wako hakulala siku saba za mwanzo akimuangalia kwa makini mumeo kitovu kisidondoke kwenye uume wake akashindwa kukupa raha za kitanda alianza kulala vizuri baada ya kitovu kudondoka vyema...leo tena shoga umeolewa ndio unamletea dharau mama yako kisa wewe ndio ubavu wa mwanae inahusu...

Unajitutumua mtoto wa kike ukisikia mama mkwe anakuja nyumbani unavuta mdogo kama unalamba mbilimbi cha kwanza unaanza kuuliza atakaa muda gani huna haya, badala wewe ukijuwa mama mkwe anakuja ndio ujishauwe tena uhakikishe unampikia vizuri na kumvisha vizuri yani akija kwako asitamani kuondoka na ndio baraka zinakuja ndani ya ndoa yako na nyumba yako tena wewe mama mkwe wako unatakiwa umdekee na kumpenda mwanaye akose la kuongea baya juu yako kwake hata kama umemlaza bila chakula cha usiku ashindwe kukusemea..eboooo

Na ikifika muda anapotaka kuondoka mtoto wa kike juwa kumfungashia mama mkwe wako sio umbebeshe nyanya na vitunguu la hasha mpe matenge jamani kariakoo siku hizi matenge yapo ya kila aina bei rahisi nunu hata matatu manne mpe mama mkwe wako unadhani ukimtumikia vizuri atapata la kukutafuta hapana jamani.

Na kwawale ambao mama wakwe zenu hawapo mikoani wapo mjini pia unaweza ukawa unampelekea zawadi yani katika mshahara wako au faida zako za kila mwezi uweke na fungu la mama mkwe mpe raha mama mkwe wako usimzoee ikapitiliza lakini mzoee kama mama yako mtoe out dinnder, dance mnunulie vitu vizuri..jamani sisi sote tunapenda na kuwapenda watu wanaojuwa kututunza vizuri hata kama wanamatatizo yao tunayavumilia kwakuwa anajuwa jinsi ya kukutunza, ndio hivyohivyo mama mkwe wako atakupenda na kukuvumilia ukijuwa kumtunza na kumpenda vizuri..

NA UTU UZIMA WOTE ULIO NAO HUJUI KULA NA KIPOFU...

0 comments:

Post a Comment