Monday, August 5, 2013

Tafakari

Ulitoa mimba. Mimba zaidi ya moja. Hukuona kama ni big deal. Sasa jambo hilo linakusumbua, linakukosesha amani, ukilala unasikia sauti ya mtoto analia. Umekata tamaa maana hujui la kufanya wala wa kumwendea. Pengine umeolewa na unawatoto lakini huna furaha nao ukikumbua yule uliyemkatisha maisha. Pengine hujapata mtoto tena. Unaona kama Mungu amekulaani sababu ya mimba ulizotoa. Huoni pa kushika, mbele giza nyuma giza.
Mchana wa leo nakuambia LIPO TUMAINI! Bwana Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu zote! Hakubakiza nyingine! Wewe unalopaswa kufanya ni kumpa maisha yako, mkabidhi ayatawale. Tubu kwa makosa yote uliyofanya, na kumkiri Yesu kama Bwana na mwakozi wa maisha yako. Yeye anasamehe kabisa na hatakumbuka tena. Anza maisha mapya na Yesu naye atakuponya na majeraha yote ya nyuma.
EZE. 18:21-23, 31-32 
Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi.

Source: Women of Christ