Friday, August 16, 2013

Word...

Mara nyingi sana tumesikia wanaume wanapopatikana wameisaliti ndoa visingizio huwa mke wangu mkorofi, mke wangu hanisikilizi, mke wangu hiki na mke wangu kile. Na mke hulaumiwa na kila mtu na hulazimishwa kumsamehe mume kwa kigezo ni kosa lake mwenyewe. Ndio tunajua kuwa mke anapaswa kumheshimu, kumsikiliza na kumhudumia mumewe lakini sidhani kwamba mke akishindwa kufanya hivi kwa kutoelewa, kiburi au uchungu basi ni sawa mume kutafuta mtu mwingine.
Maana mume anawajibika kumhudumia na kumtunza mkewe, wapo wanaume wengi tu hawatimizi hili hakini hatuoni wake zao wakitafuta watu nje wa kuwatimizia. Ikitokea hivyo basi mume anaambiwa mke hafai kusamehewa hata wanawake wanaosimamia mume lazima asamehewe anapokosea nao pia wanasimamia mke lazima aondoke. Je, mke anawajibika kwa tabia ya mumewe?
Wako wapi waume wanaowapenda wake zao hata pale ambapo mke anaonekana jeuri, maana mtu ambaye ni mgumu kupendeka ndiye anayehitaji upendo sana. Mume kwa upendo unaweza mbadilisha mke ndio maana biblia inasema waume wawapende wake zao, hapa bila kujali mke anafanya au hafanyi nini.

Source: Woman of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment