Wednesday, August 21, 2013

word

Kijana umemuona dada, ukampenda na ukamfuata kumueleza yako ya moyoni. Baada ya muda akakubali na mkawa kwenye mahusiano mkitaraji kufunga ndoa maana ulivyomfuata ulimwambia unataka kumuoa. Baada ya miezi kadhaa kimyaaa, hakuna simu, hakuna msg na ukitafutwa unasema upo busy. Dada wa watu anakuwa katikati haelewi ndoa ipo au haipo, haelewi kwanini umekata mawasiliano ghafla na wala hamjagombana.
Kama ulikuwa umewaweka pending wengi na umeshamchagua mmoja kwanini kuendelea kumfunga dada wa watu? Kama umeona yaliyomo hayamo kwa mtazamo wako kwanini usinwambie ukweli kuwa wewe nayeye basi? Na kwanini unamuahidi mtu kuwa utamuoa wakati moyoni unajua kabisa sio kweli au wapo wengi hivyo uhakika haupo? Unaishia kuumiza moyo wa dada wa watu maana yeye anakuwa amejitoa kweli kweli. Acha kuharibu maisha ya mtu usiye na mpango wa kumuoa, anawakataa wengine akijua yupo na wewe kumbe wewe umempanga unamthaminisha. Ukiona sio unapotea kimya kimya yeye anajua ana mtu anakuja kushangaa unaoa.
Huwezi kuwa na ndoa yenye furaha na baraka huku kwenye ujana wako ulikuwa mtu wa kuwaumiza tu wadada kwa kuwachumbia na kuwatosa. Kama huna uhakika wa kumuoa usimweleze kabisaa, hadi utakapopata uhakika yupi utamuoa.

Source: Woman of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment