Jamani hapa nataka tuongelee mama wakwe wenye gubu na masimango yani jamani kuna mama wakwe wengine hata uwapende vipi hawapendeki yani wao kero tu muda wote.
Kwanza kabisa japo namatatizo yake na masimango yake wakati mwengine japo unahamu ya kumtukana, kumfanyia madharau ninakusihi kwanza, usijaribu hata siku moja kufanya hivyo na unatakiwa kwanza kumuheshimu kama mama yako na pia kumchukulia msalaba wake wa mapungufu yake.
Unachoweza kufanya wewe ni kukaa kimya na kumuhudumia vyema mmueo usimpe nafasi ya kuwa asilimia 100% kwa mama yake anatakiwa awe 50% tu japo ndio anampenda sana mama yake lakini mapenzi zaidi yanatakiwa kuwa kwako kwani wewe ndio mtu ambaye upo naye zaidi baada ya kumuacha mama yake.
Mama wakwe wengi wanakuwa na roho mbaya kwasababu wanahisi kwamba pindi mtoto wake akioa basi huduma na attention kwake tena ndio hamna yote anapeleka kwa mkewe ndio maana anatumia ubabe kupata attention kwa mwanae.
Wanawake wengi wanapokosea ni kuwadharau mama zao wakwe wa aina hii unapomdharau mama wa mumeo usitegemee mumeo atakupenda wewe zaidi, tena mama mkwe wako atakusingizia maneno kibao kwa mumeo mara tena ndio mnaanza kugombana mwanaume hashikiki tena kurudi nyumbani na vituko vingine kibao, na usimpelekee mumeo matatizo ya mama yake hawapendi hao viumbe yani wewe ndio utaonekana huna adabu na umpendi mama yake.
Anapokuja nyumbani kwako akusonye, akutukane,akusingizie vibaya, hata akuteme mate usinyanyue mdomo wako kumtusi wewe miaka inaenda tu ukihudumia mumeo na watoto na nyumba yako itafika sehemu tu mwenyewe atakaa sawa maana wakiona watoto wao wanatunzwa vizuri ile chuki hugeuka kuwa upendo na kuanza kukuamini na kukupenda.
Kwani hukusikia kuna msemo unaosema anayekudharau siku moja atakusalimia kwa heshima???? hata mama mkwe wako naye ni mmoja wao.
0 comments:
Post a Comment