Tuesday, August 27, 2013

Mwanamke sikia hii

Kila mmoja anafahamu kuwa biblia inawataka wanawake wawatii na kuwaheshimu waume zao, ila wengi hawajui mambo gani yanaonyesha haumuheshimu na athari za kutomuheshimu ni nini. Kumuheshimu mume kunaanzia ndani ya moyo na nje ni matokeo tu. Haijalishi mumeo ameokoka au la, unakipato kumzidi au la, mkorofi, mlevi au vyovyote. Maadamu ni mume wako yakupasa kumtii na kumheshimu katika Bwana.
Unapokuwa unambeza na kumdharau mumeo ndani ya moyo wako na kumuona hana faida ni sawa na kumfanyia akiwa anaona maana katika ulimwengu wa roho unampa shetani nafasi. Huwezi kumuombea mtu unayemdharau ndani ya moyo wako. Mambo mengine yanayoonyesha huna utii kwa mumeo ni kutomshirikisha mipango yako na kufanya mambo bila kujali yeye anasema nini, tangu unachangia kitchen party hana habari, umepata kadi bado kimya halafu asubuhi unamwambia "leo naenda kwenye kitchen party", hiyo haifai kabisa. Mumeo anapaswa kujua ratiba zako zote ziwe za kikazi, kanisani, kijamii, binafsi n.k na kwa pamoja mnakubaliana jinsi ua kufanya.
Kutokuwajali ndugu zake hasa wazazi wake. Wanawake wengi wanaonyesha upendo kwa mume ila hawawajali ndugu wa mume, hii kwa mume anaona ni kutokumheshimu. Mheshimu mume kwa kuwajali na kuwapenda ndugu zake bila kuangalia wao wanakutendea nini. Jambo lingine kubwa la kumuonyesha heshima ni kuwa tayari pale anapokuhitaji kimahaba na sio kila siku unatoa visingizio. Mume ambaye mkewe kila siku anatoa visingizio au haonyeshi ushirikiano anajiona kutoheshimika na mkewe. Mume hujisikia kuheshimika pale mkewe anapokuwa tayari kufurahi naye bila kuona kama ni kazi wala kulazimishwa bali kwa moyo uliochangamka na sio kutumia jambo hilo kama silaha ya kumuadhibu au pale anapotaka kitu.
Athari za mume ambaye mkewe hamheshimu ni nyingi, zikiwemo kukosa ujasiri mbele za familia, kazini na hata kanisani. Hujiona hajakamilika na hawezi kufanya kazi zake kwa ujasiri. Pia huwa ni mtu aliyejaa hasira na asiye na furaha hasa akiwa pekeyake, wakati mwingine hujikuta anajiingiza kwenye emotional affair ili kujaribu kutimiziwa hitaji la heshima maana ni hitaji kubwa sana kwa mwanaume. Kama ni boss ofisini basi atakuwa mkali sana au mkali kwa watoto. 
Kumheshimu mume sio utumwa wala unyanyasaji bali ndio msingi wa ndoa imara na yenye baraka.

Source: Woman of Christ

Reactions:

0 comments:

Post a Comment