Monday, August 19, 2013

Kukataliwa -2

Soma kwanza sehemu ya kwanza.
Unapoweka thamani yako kwa wanadamu ni lazima utaona kukataliwa na kujikuta unaruhisu roho za kukataliwa kuingia kwako. Lazima utambue kuwa thamani yako inatoka kwa Mungu na si wanadamu wanakuonaje. Haijalishi nani anasema nini bali tafuta Mungu anasema nini. Acha kumlaumu Mungu na kujilaumu unayopitia, biblia imasema mapito ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humlinda na hayo yote.

Usiruhusu chuki, uchungu, hasira na wivu vipate nafasi ndani ya moyo wako. Soma neno la Mungu lijae ndani yako na maombi kwa wingi. Kataa roho ya kukataliwa isipate kibali ndani yako kwa kuondoa milango ambayo ni kutokusamehe, chuki, wivu, uchungu na kumlaumu Mungu. Usiangalie yule aliyekutendea mabaya na kukukataa kama vile yeye ndiye mwenye hatima ya maisha yako bali muangalie Mungu aliyeahidi kuwa nawe siku zote.
EBR. 13:5b-6 
"kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?"

Mambo ya kufanya kushinda kukataliwa
1. Mruhusu Roho mtakatifu akuonyeshe umeumizwa wapi na kwa kiasi gani kwa kukataliwa.
2. Samehe wale waliokuumiza
3. Tupilia mbali matunda ya kukataliwa: chuki, hasira, uasi, uchungu n.k.
4. Kubali kuwa Mungu amekukubali kupitia Yesu Kristo.
5. Jikubali

ZAB. 71:5-7, 13 
"Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima. Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi, Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu. Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya."

Soma pia Ebrania 4:16 Zaburi 23 1 Samwel 53:4

Source: Woman of Christ

0 comments:

Post a Comment