Monday, May 31, 2010

MKE KUWA NA UHUSIANO NA HOUSEBOY......

kuna kisa kimoja kimemtokea kaka mmoja hivi karibuni, ameoa mke mzuri tu na wanawatoto wawili, wanaishi mitaa ya mbezi samaki wa bichi, huyu kaka kweli ni mtanashati kwa uzuri tu acha nimsifie kwani namjua nakumbuka pindi alivyokuwa shule wanawake wengi sana waligombana kwa sababu yake..

huyu kaka na familia yake wanaishi kwenye nyumba kubwa sana, yeye ni mfanya kazi na mkewe ana duka tu la nguo karibu na nyumbani kwao kwahiyo muda mwingi huyu mama yupo nyumbani, sasa hawana house girl kwani mama hufanya kazi zote halafu baadae ndio huenda dukani, lakini kwasababu nyumba yao ina garden kubwa yenye kila aina ya maua wakaamua kuajiri house boy wa kuitunza ile garden..

kwa mduda mrefu yule house boy alikuwa anafanya kazi vizuri sana, wakakaa miaka karibia sita na huyu kaka tokea akiwa kijana mdogo mpaka mkaka, alivyozidi kukuwa alizidi kumvutia yule mama, halafu ukiangalia kijana always yupo fit kimwili, akienda kufanya kazi zake huvaa kaptula fupi na vest akionyesha vitu ambavyo Mungu amemjalia..

ikafika kipindi yule mama akajikuta hawezi kuvumilia tena, kwa bahati mbaya mumewe akapata safari kikazi, lakini kwa huyu mama huo ndio ulikuwa muda mzuri wa yeye kumpata house boy, baba alivyoondoka mama siku moja akamwagia mtama kuku, akamueleza kijana jinsi alivyotokea kumpenda , na kijana kwasababu alikuja kutafuta pesa akajua atakapokuwa na huyu mama atapata pesa nyingi kuliko anazopata kutengeneza bustani..

kijana akaingia mkenge, akamkubalia mama siku hiyo wakapanga waende kulala hotelini mchana kwani watoto wakirudi watakaa na dada kama kawaida, kijana akajiandaa bwana kufika hotelini akampa mama shughuli ambayo hata baba hampi hivyo.. (Duhhhh pesa hizi jamani)

mama siakanogewa bwana, ikawa ndio mchezo wao, sasa kwa vile yule house boy alikuwa anakaa mule kwenye ile nyumba mama akawa hata kwenda hotelini anaona anapoteza muda akawa anajimiminia tu mzigo mule mule nyumbani kwa mumewe mbaya zaidi chumbani kwa mumewe..

siku hiyo bwana baba kule safari alipokuwepo akaona awahi kurudi nyumbani kwani ameikumbuka familia yake, akarudi nyuma ya siku aliyokuwa kamwambia mkewe atarudi, kwani watoto mda huo walikuwa bado hawajarudi na mama na kijana kama kawaida wapo chumbani, jamaa kufika akaamua kwenda moja kwa moja chumbani ili aoge akamfwate mkewe dukani, jaaaaaaniiiii kufungua mlango hehe asimuone mama juu ya kijana anashughulika, mbaya zaidi anamwambia kijana yani raha unazonipa hata mumwe wangu hanipi hivi....

jamni yule kaka alicho kifanya ni kudondosha begi alilobega ndio likawashtua wale wawili, kijana kuona hivyo akataka kukimbia lakini yula kaka akamdaka na kumrudisha chumbani, wote wakiwa hawana nguo kaka akawapa adhabu waendelee kufanya alicho wakuta wakifanya......

wawili wote walishindwa, yule kaka chakufanya akamwambia house boy aondoke, na kwa mkewe hajawahi kumwambia kitu chochote wala hata kumpiga na mpaka leo ni wiki ya pili hii yule kaka hajawahi kuongelea kitu chochote kuhusu hilo swala, mke wake sasa ndio anachanganyikiwa anaomba hata yule baba japo ampige yani kachanganyikiwa na kurudi kwao hawezi kwani familia itamchukulia vipi..

huyu kaka alikuja kunihadithia huu mkasa, anasema mpaka leo hajui afanye nini kama amuache mkewe ama ampige, kwani anaogopa akimuacha wanawe itakuwaje na akimpiga anaona linaweza kuwa balaa akiua je?

jamani mwenye ushauri uwanja wako..

KUWASHWA BAADA YA KUNYOA....

jamani wenzangu kuna dada mmoja amenitumia msg through blog hii anajambo ambalo linamtatiza kwa muda sasa baada ya kunyoa sehemu zake nyeti baada ya muda huwa anawashwa, anaomba ushauri wenu zaidi juu ya hilo....

tatizo la kuwashwa baada ya kunyoa kwa ninavyo fahamu mimi maranyingi husababishwa na kitu unachotumia kunyolea, kwani wengi hutumia wembe, wembe wa aina yeyote ile huwasha baada ya kunyoa na mara nyengine mpaka ikakutoa vipele vidogo vyenye maji na huuma sana vikitumbuka..

na wakati wengine huwashwa kwasababu ya dawa za kunyolea, siku hizi dawa za kunyolea zimekuwa nyingi sana, sasa dawa hizi unaweza ukatumia na kukusababishia muwasho baada ya kunyoa, kwani zinaweza zikawa hazipatani na ngozi yako..

hizo ndio sababu mbili kuu ninazo zifahamu, kwa wengine wote wenye sababu nyengine tafadhali tumsaidie huyu dada ajue jinsi ya kutatua hilo jambo alilokuwa nalo...

Friday, May 28, 2010

RAHA YA MKEKA.........

mkeka ni kitu muhimu sana kuwepo nyumbani kwetu, japo wengi hudhani ni watu wa pwani tu hupendelea kutumia mkeka, ama labda kwavile watu wengi hawatambui matumizi ya huo mkeka..

raha ya mkeka ukaliwe bibi, jioni ile siku ambayo wote mpo nyumbani sio mbaya watoto wakiwa nje wanacheza utandike mkeka ukumbini ama hata barazani kukiwa hamna jua uandae na kahawa na haluwa, tende ama kwa sie wapenzi wa juice uiweke pale ikiwa kwenye jagi la mvuto, mkaribishe mpenzi wako mkae wawili ukipenda umlalie ama akulalie kwenye miguu mkitafakari maisha yenu pamoja na ya watoto wenu..

kuna wakati pia hujisikii kukaa mezani kula na watu wengine ama labda mpo wawili tu nyumbani kwenu basi sio mbaya siku moja moja ukatandika mkeka wako chumbani ukaweka chakula kidogo mkaamua kuhamishia meza chumbani kwani wakati mwengine baba hupenda mkewe akimlisha na haipendezi watoto wakaona baba anapokuwa analishwa na mama..

kwa wale ambao wanachoka mara nyengine kulalia kitanda, kwanini usijaribu kutandika mkeka na ukashusha godoro lako ukalala chini, mgongo ukapata kunyooka, huku pembeni ukiwa umekumbatia kilicho chako... hehe

jamani sababu za kuwa na mkeka nyumbani ni nyingi sana hizo ni chache tu, na ndio maana mama zetu kati ya zawadi nyingi wanazotupa basi mkeka lazima huwa moja wapo kwani wanadhamini sana matokeo yake.

DAWA YA CHUNUSI KWA WANAWAKE.....

kabla ya yote nitaandika hii mada kwasababu ya uzoefu lakini sio kwamba nilichoandika hapa kinaweza kutekelezeka kwa kila mtu, kwani tunajua ya kwamba ngozi zinatofautiana kama imefanya kazi kwangu sio lazima na wewe ikukubali kwahiyo ukiwa unajaribu na ukiona tofauti hamna basi juwa labda dawa hiyo sio ya ngozi yako..

marafiki zangu wengi sana walikuwa wananiuliza inakuwa vipi ngozi yangu kuwa nyepesi na yenye mvuto bila chunusi, ama mabaka ya chunusi, kwani wengi wao chunusi ndio tabu kubwa sana kwao, nilikuwa na hofu kubwa sana ya kuwaambia dawa lakini leo nikawaambia nitaitoa humu ili wapate wote kuelewa na mwenye kujaribu haya shauri yao matumaini yangu ni kwamba tu ngozi zao pia ziwe nzuri..

hamna kitu ninacho kiogopa mimi kama kupaka cream za ngozi kwani nyingi ndio chanzo za hizo chunusi na mabaka, na nyengine nyingi huchubua ngozi. naona mpaka aibu kuandika lakini ngoja tu niandike, jamani hamna scrub nzuri ya ngozi kama shahawa najua kila mtu anayesoma atasikia kinyaa lakini ukweli ndio huo..

na shahawa sio ya kila mtu leo upake ya Paul, kesho John an wengineo hapana, inafaa ya mtu mmoja kama umeolewa basi ya mume wako tu ama kama una boyfriend basi ni ya huyo mmoja tu ndio upake kwani scrub hiyo hufanywa kila mwezi ili ngozi yako izidi kupendeza inataka kupokea virutubisho vya sehemu moja tu sio kwa watu tofauti..

ni ngumu sana kuanza kwa mara ya kwanza lakini baada ya muda unajikuta umezoea na utashangaa jinsi ngozi inavyo pendeza.. kwa miaka zaidi ya minne nimeona tiba yake...

na kwaushauri scrub hii ni vizuri ifanywe siku ambayo unajua hutoki kabisa nyumbani, kwani hutatakiwa kupaka kitu chochote usoni siku hiyo..

nikiasi kidogo tu cha shahawa huitajika, kutumia vidole unaipaka sehemu mbalimbali za uso ikiwa imeenea vizuri unaiacha kama dakika tatu mpaka tano, halafu taratibu sugua uso wako uhakikishe yote imetoka kwa msuguo huo, baada ya hapo bila sabuni osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu, ukaushe vizuri halafu uuache bila kupaka kitu chochote usoni siku hiyo.

hii ni point tu kati ya dawa za ngozi ya asili ambayo nimeona mafanikio yake, simshauri mtu yeyote kwa nguvu atumie, ila tu kwa wale ambao wanaweza kutumia za waume ama mabwana zao haya, na kumbuka inaweza ikakupenda ama isikupende...

Thursday, May 27, 2010

COMMENTS........

hii blog ilianzishwa kuwekana sawa na sio kutukanana, kwahiyo mnaotuma comments kutaka kuwatukana watu haipendezi na wala hatuhitaji... nimeitoa blog hii kwa watu wanayetaka kuisoma wenye kupenda maendeleo sasa kama wewe shida yako kuichambua lipi zuri lipi baya unakazi... hapa mwendo wa kuelimishana tu na kwa lolote ambalo linahusu maisha ndani ya nyumba tutaliweka hapa liwe baya ama zuri.....
kwahiyo comments zenu mnazotuma za matusi hapa hazina nafasi...

Wednesday, May 26, 2010

UBUNIFU JAMANI MHHHHHHHHHH........

sisi kama binadamu lazima tuwe wa bunifu katika nyumba zetu, katika usafi, upambaji, rangi, hata mapishi na sio hivyo tu ubunifu hata chumbani ndugu yangu..

tatizo kubwa ambalo nimetokea kushuhudia na kusikia watu wengi sana wakisema katika ubunifu wa chumbani ni kwamba wanawake wanapo buni style mbalimbali za kitandani wapenzi wao hudhania ya kwamba wametoka nje iwaje ujue kitu hichi ambacho hujawahi kufanya.

ndio maana hata kwenye topic ya mapenzi bafuni niliongelea ya kwamba mapenzi yanaweza kufanyiwa sehemu yeyote sio tu kitandani, kuna jikoni, sebleni, kwenye gari, kwenye lift yani nikianza kutaja sehemu hapa sitamaliza kuandika,

mapenzi jamani ili yazidi kunoga lazima tuwe wa bunifu sio kila siku umelala wewe tu chini, jamani yani mpaka inachosha kunakuwa hamna raha lakini leo ikiwa hivi, halafu vile, halafu huku hata kama mwenza wako anakuwa hana hamu pale unapo mpa chejo jipya lazima apate msisimko wa kutaka tena na tena..

kwahiyo tujifunze kubuni jamani penzi nikitu Mungu alikileta duniani tu enjoy kufanya sasa wewe usifanye iwe adhabu kwa mwenzako, tulia upewe mambo wewe (hehehehehehehe)

MDALASINI, TANGO NA ASALI....




jamani wenzangu nina jambo mlikuwa mnajua kama mdalasini, asali na tango ni dawa ya kumpa mtu nguvu kwenye mechi? kama ulikuwa hujui ndio ufahamu eti..


kuna dada mmoja alikuwa analalamika mpenzi wake nguvu kitandani hana, anasema jamaa akishatoa moja tu basi nguvu zote zinaisha jamaa hawezi hata kurudia ya pili, na hapo mwanamke wake huyo anakuwa hajatosheka lakini jamaa hajiwezi kabisa..




sasa huyu dada akawa anaomba ushauri kwa watu wazima akiwaeleza swala lake na mumewe watu wengi wakawa wanamshauri mengi tu pamoja na ya kwamba mumewe anywe maji ya mchele yale ya kwanza, sijui mwengine akamwambia anywe maji ya madafu kwa wingi na wengine wakimwambia aende kutafuta dawa za miti shamba...



akafika kwa bibi mmoja wa zamani (umri umeenda) yule bibi akamwambia yule dada ampe mumewe mdalasini pamoja na asali achanganye kwa pamoja atie na maji ama aiweke kwenye chai, halafu kila chakula cha yule baba kisikose kipande cha tango..



yule dada akafanya kama alivyoambiwa na yule bibi, sasa hivi dada anafuraha mambo si shwari, kwahiyo huu ni ushauri tu ya kwamba ukiona mwezio nguvu hana akienda moja anahema kama kasukuma trekta, mwanaume anahema kama presha imeshuka (hehehe) basi sio vibaya ukijaribu hayo..



lakini naomba niseme sio tu kwasababu huyu dada yeye mpenzi wake alipata nafuu ndio kila mtu itakuwa hivyo wengine vyao vya kurithi utalisha hivyo vitu milele jamaa hata kubadilika asibadilike...

Tuesday, May 25, 2010

RAHA YA MECHI BAO?

jamani leonimesikia wanaume fulani wanaongelea swala la mapenzi wanasea eti raha ya mechi ni bao, kweli nimeamini wanaume wanamatatizo wewe kama bao ndio la muhimu basi mechi huijui.... raha ya mechi kufika babu lakini cha kushangaza wanaume wengi wanafikia bao lakini kufika kilele hawafiki....

mechi sio kutoka na kuingia na kuelekea upande huu na ule, kijana unaweza kumfikisha huyo dada bao linapigwa na wengi hata mbwa ana bao kufika unafika?????????????

ndio hapo wasaidizi waliokaa bench wanaanza kuingia uwanjani...

poleni wanaume kama nawaonea lakini ukweli wengi wenu mnajua kuingia na kutoka tuhalafu mnajisifu mnajua mechi wakati kumfikisha mwanamke kilele hamuwezi, labda mpaka mfanye alamba.....

raha ya mechi kilele babu sio bao..

Monday, May 24, 2010

MAPENZI BAFUNI........


kwawale wenye uwezo wa kujenga ama kupanga nyumba ni vyema ukizingatia kufanya hivyo ukahakikisha chumba chako cha kulala kuna bafu, na vizuri kamalitakuwa la beseni kama lilivyo hapo juu lakini kwa wasioweza kuwa nayo basi sio vibaya ukipata hela umpeleke mpenzi wako mkalale japo siku moja kwenye hoteli najua kwa uzoefu hoteli nyingi za sasa zinahayo mabafu.

sio wakati wote mapenzi yafanywe kitandani jamani, uzuri mbadilishe, kama kitandani, jikoni, sebleni, kwenye gari mapenzi ni kitu cha ubunifu sio sehemu moja tu wa kuchezea (mimi huuita mchezo wa upendo).

kuna wanaume wengine wasiopenda mambo ya ubunifu kama huu wakati wanawake wengi hupendelea mambo kama haya, basi wewe baba, kaka, mjomba jitahidi kumridhisha mpenzi wako ni mambo madogo lakini mzuri ambayo humchanganya mwanamke.

bafuni ndio sehemu yangu niipendayo kuliko zote, pakiwa pamezimwa taa na kuwashwa mishumaa ya upendo yenye manukato, na melody kwa mbali sio ufungulie mziki mkuubwa ukaharibu yale mapenzi yanayozunguka kati yenu, mkiwa na wine pembeni..

maji ndani ya beseni yanaweza yakawa ya uvuguvugu ili kufanya mwili kurelax, ukaweka na sabuni ya maji yenye kutoa mapovu isiwe na harufu ili isichanganyike na harufu ya mishumaha ili harufu zisije kuharibu wakati..

mda huo ukiutumia kumvutampenzi wako kwa karibu ukimpapasa mwili wake na kumsifia jinsi alivyoumbika, hata kama hana mwili uupendao lakini msifu kwani huyo ndio mpenzi wako, na wakati huo hutakiwi kufikiria chochote cha zaidi bali ni huyo tu uliyekuwa naye mbele yako..

wakati mziki wa mapenzi ukipiga taratibu acha miili yenu iongee yenyewe mkiwa mmekumbatiana kwa upendo na upendo huo uendelee mpaka mtakapotosheka....

VYOO VYA NJE JAMANI......


tunajua ya kwamba wengi wetu huishi maisha yakawaida tu ya kiafrika na tunakaa kwenye nyumba zile za kawaida tu choo, bafu vyote vipo nje tofauti na watu wachache wenye uwezo wakuishi kwenye nyumba ambazo vyoo, na bafu vipo ndani na wengine wenye bahati zaidi hata vipo chumbani mwao wanapolala...

jamani vyoo na mabafu yetukwakuwa vipo njeya njumba zetu basi visitupe sababu ya kufanya mambo ya ajabu, utakuta baba anaenda chooni amevaa taulo fupi linaloonyesha miguu yake na ilivyokuwa na manywele mpaka kichefuchefu, ama utamkuta mwanamke anatoka na kanga moja anaenda bafuni ama kuswaki jamani haipendezi mnatafuta nini maneno ama kuchekwa maana vitu vyenyewe vya kuvutia hamna sasa kwanini msijistiri miili yenu?

na wengi wanakaa nyumba za kupanga mara baba haupo mkeo katoka na kanga moja labda kaka chumba cha pili kavutiwa nae basi kiulaini unasaidiwa maana wanaume kwa kuomba mpaka wanatia huruma...

na wewe baba ndio umetoka na hicho kitaulo mara kimekudondoka dada wa jirani kaona mambo ambayo hata mpenzi wake hana unadhani kitatokea ni ni dada atajilengesha mpaka uingie mkenge na hivi wengi mlivyokuwa wadhaifu??????

jamani tujitahidi kuepuka tusiyoyategemea haswa tukiwa tunawakwaza wale tunaoishi nao karibu....

WANAWAKE HUPENDA NINI KWA WANAUME.......


wanawake hupenda vitu mbalimbali toka kwa wanaume je wewe ukiwa kama mwanamke unajua unapendelea mwanaume wako ama mwanaume unayemtaka awe na vigezo gani? iliwahoji wanawake na haya ndio wanayoyapenda......

Zaituni: anasema yeye anapenda mwanaume kama alivyo bila kuongeza wala kutoa chochote pindi wanapokutanakwa mara ya kwanza.

Mary: yeye anapenda mwiko wa mwanaume kama mfupi, mrefu ilimradi tu unakoroga chakula na kukipika vizuri mpaka kuiva.

Fatma: anasema yeye anapenda mwanaume mzuri tu akikuona humvutii hatakama mtoto wamfalme huna chako kwake.


Teddy: anasema anapenda mwanaume anayejua alamba style, sio wewe unataka kuchovya tu, kuweka vidole utadhani unaonja supu.

Rhoda: yeye anapenda mwanaume anayejua kujiheshimu na kumuheshimu yeye kama mwanamke wake.

Mwani: anapenda mwanya, na kitambi haswa vya mpenzi wake vinamuacha hoi jamani.

Irene: yeye anapenda mwanaume wake anavyokuwa nae pindi wanapo kuwa faragha, jinsi anavyo tulia na mwenye mapenzi tele sio mpo wawili halafu mwanaume unajifanya too much to do.

Rosemary Mizizi: kwakweli hamna kitu ninachokipenda kwa wanaume kama kiuno, jamani uwe mfupi, mrefu uwe mshamba ama wa mjini ujue kuvaa ama hujui kiuno mimi ndio ugonjwa wangu mkubwa..

Saturday, May 22, 2010

UNARINGA UNANINI.........

jamani hivi kunawanawake wengine wana matatizo sana, huko mjini Leicester kuna dada mmoja hivi anaitwa vumi anapenda sana kujitapa na mwanaume wake, eti anasema wanawake wanamtaka huyo bwanake.. juzi tu umeenda kumsingizia mpaka khadija(shoga yangu kipenzi) kwamba anamtaka bwanaako sasa leo naomba nikutolee uvivu hivi wewe unaringa unanini amahuyo mwanaume wako unyemringia ananini haswa kwenda kujitapa mpaka London kwa kina leyla aunt yake khadija kwamba unachukuliwa bwana kama unampenda sana siumfunge kamba utembee nae kila kona uendapo? mbona mwanaume mwenyewe hafungiki akija kwako anajifanya mwema mbona juzi tu alikuwa anajigonga kwa khadija pale club afrique katikati ya london......

ndugu yangu wenzako wamekuchoka na ushamba wako, kwanza huna lolote hata nusu hujafika bado unachezea robo na tabia zako za kishamba ziache hukohuko usione wanakuchekea ukadhani unaogopwa...

UK nzima inakujua wewe kwa ushamba uliokuganda, nenda kwanza kajifunze kuupara, oga vizuri toa jasho fua na chupi yako itakate halafu ndio utafute ugomvi na sisi....

khadija, asha, vaioleth, nasikia anajigamba eti aja olewa bongo, inatuhusu nini sisi kama ndoa kila mtu anayo kwani wewe ndio wa kwanza kuolewa ama ndio wa mwisho? na kama wanaume kila mtu anao tena wazaidi ya kwako babu hatujaona chochote kile cha wewe vumi kututisha, tafuta wa size yako dada maana kama size hii XXXXXXL haina mpinzani.....

na huyo mwanaume wako kabla hajaja kukuoa huku bongo mtafutie scrub japo ang'ae atoe hizo chunusi zilizomjaa usoni, na mpe lishe anenepe maana hehehehehehehehehehehe halloooo, kama wembamba wa reli treni linapita mbona hajali za treni zinazidi?

unaringa unaringia nini? na wote marehemu watarajiwa?
unaringa wakati tukikuvua nguo unanuka shombo? hehehehehehehe halllooooooo unalo hilo bibi...

na siku yako ya harusi akikisha umekuja na make up kutoka huko uingereza maana na hiyo sura yako kama ya mzee mbona utachekesha,


na kwalolote na chochote vumi unajua pakutupata....

khadija mpenzi nakukaribisha ndani ya bongo nitakuja airport kukuchukua, japo nikupe bia baridi kwa uchovu utakaokuwa nao kwani safari ndefu kutoka UK mpaka Dar...

ROSEMARY MIZIZI.

Friday, May 21, 2010

ALAMBA AMMMMHHHHHHHHH......

kuna post moja niliandika kuhusu kufikia kilele katika mapenzi, na rafiki yangu mzuri sana FK alisema kabla ya kuanza shughuli ni vyema kama utaanza na mamboz kama alamba najua wengi mnafahamu..
kwa wengi huwawia vigumu sana kufanya hilo tendo la alamba, kwakweli nafahamu ni wengi sana wanasema hawawezi kabisa hata kama wanataka kujaribu wanajikuta tu wanashindwa wengine wanasema ni kinyaa, wengine wanakosa pumzi kila mtu analake..
ndio maana leo ninataka kuwaambia njia rahisi ya tendo la alamba, tendo hilo kwanza kwa ushauri sio la kufanya tu kwa mtu yeyote hata wale wa pita njia yani wale ambao sio wa kuduma wa mara moja tu ama ambao hutaki kuwa nao kwa mda mrefu..
alamba inapendeza ukimfanyia mpenzi wako ambaye mnaaminiana kwa afya na usafi, sasa asi kuna syrup moja huwa ni za ladha tofauti tofauti lakini mimi hupendelea ya strawberry, huwa zinapatikana kwenye supermarkets nyingi hicho ni kitu ambacho hutakiwi kabisa kukikosa nyumbani kwako...
sasa mnapokuwa pale chumbani baada ya kuoga mmekaa tayari kwa kuchuma matunda, mpake mpenzi wako mwili mzima halafu ulambe, hii husaidia kukata harufu yeyeote ile ambayo mwenzi wako anayo na pia hukupa hamu ya kufanya tendo la alamba kwa mwenza wako naye humfanya ajisikie vizuri kwani kila wewe unapo zidi kulamba ile strawberry yeye anazidi kupata raha ya kufikia kilele.
haikinahishi, na ni tamu sana...

KARAFUU......



tunajua ya kwamba karafuu ni zao linalonukia saaana na tena harufu yake ni nzuri sana sasa jamani kuna watu fulani siku hizi wanasema mwanamke ama mwanaume shurti uogeshwe na karafuu ama iliki ili unukie vizuri na kumvutia mpenzi wako haya mambo zamani yalikuwa yanafanywa na watu wa pwani lakini siku hizi kila kabila bibi lina manjonjo...

kwa mimi binafsi harufu ya karafuu ama iliki naipenda tu kwenye chakula lakini kwenye mwili wa mpenzi wangu wala sitaki kuisikia, na kwa wengine ambao wapo kama mimi wasiopenda harufu kuna vitu vyengine ambavyo vinaweza kuchukuwa nafasi ya karafuu na iliki kama udi wa vanilla, roses, ama hata wa lily flower.. manukato hayo unayachoma kwenye kifukizo na kuyaweka chumbani kwangu kuliko hiyo harufu kali ya karafuu (huu ni kwa upande wangu)...

na kabla mwanamke hujaamua kuweka hizo karafuu na iliki kumpendezesha mpenzi wako hebu muulize kwanza maana usije ukanunua ukaweka chumbani kumbe mwenzako badala aingie ndani anakimbia chumba, itakuwa aibu...

wote tunapenda chumbani kwetu panukie vizuri lakini wapenzi wetu huwa wana matatizo na harufu iwe nzuri ama mbaya wao kutwa na chafya, mafua mpaka utawaonea huruma...

kwahiyo tusijifanye tunaujua ufundi hebu kabla ya kumuwekea mpenzi mankodinkodi hebu tuulize tujuwe kipi kina faa na kipi hakifai....

USAFI WA MWIKO NA SUFURIA........










tumehsauriwa ya kwamba tupunguze ukali wa maneno katika kuandika na kutoa ushauri katika blog kwasababu inawezekana watu chini ya umri(18) kuangalia blog hii halafu haitakuwa vizuri wakutane na maneno mazito..

sasa basi tuelekee kwenye point, uoshaji wa sufuria na mwiko, jamani ni muhimu sana kuosha miili yetu pindi tunapomaliza shughuli zetu zile..........

kuna siku tulitoka kwenda club moja hivi maarufu sana na ndio kwanza mpya kabisa katika jiji hili la Dar es Salaam, tukaketi katika viti tukicheza pamoja na marafiki wengine, mara akaingia mdada mmoja alikuwa pamoja na mpenzi wake kwa style walizokuwa wanakumbatiana na kucheza mtu yeyote angejua wale walikuwa ni wapenzi.

cha kusikitisha ni kwamba yule mwanamke alikuwa ananuka chini jamani yani kama nichakula sufuria yake ilipikia basi lile sufuria chakula kiliungua, jamani wananawake hata kama ni mrembo kiasi gani utakaposhindwa kuosha sufuria yako vizuri basi hata huo urembo wako unakuwa hauna maana.

na nyie wananaume pia sio umemaliza kusonga chakula kwenye sufuria halafu unavaa tu unaondoka hata hausubiri vile vinavyoshuka baadae uvifute... haipendezi mkaka wa maana umependeza halafu kumbe unanuka shombo ya mbegu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

tujifunze kujiosha jamani hatakama ikitokea mara moja iwe bahati mbaya, labda sehemu uliyokuwepo maji ya kutosha hamna, lakini usafi wa sufuria ni muhimu sana.

Wednesday, May 19, 2010

KUVAA SHANGA...


watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu, nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..

kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..

kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..

wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..

sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....

KWA WALAJI KITIMOTO.....





Nina swali kwa wali wa kiti moto, hivi kuna dada mmoja ameolewa na muislamu ambaye ni swala tano kama wanavyoitwa watu ambao huswali sana, sasa huyu dada yeye ni mkristo hodari sana na mbaya zaidi ni mpenzi sana wahiyo nyama katoliki kama nilivyosikia watu wanavyoiita, huyu dada yeye anadai ya kwamba hawezi kuizcha kula hiyo nyama japo mume wake hali hata siku moja, rafiki zake wengine wanamwambia aendelee kula kwani mumewe hawezi kugundua kwani inaandikwa usoni kama umetoka kukila wanamwambia......sasa yeye anachojisikia vibaya ni pale anapotoka kula na kurudi nyumbani na kumpa penzi mumewe maana mume wake akitaka anashindwa kumkatalia, mpaka imefikia sasa ameamua kumdanganya akisikia jamaa anaanza kuomba yeye anajifanya anausingizi ile mbaya.... anasema amejitahidi sana kuacha kuila lakini ameshindwa... afanyeje?

Tuesday, May 18, 2010

KUFIKA KILELE KATIKA KUFANYA MAPENZI..


hivi jamani tumeshawahi kuwauliza wapenzi wetu kama huwa wametosheka ama wamefurahia penzi ulilotoa? maana bwana samahani kama nitakuwa nakukwaza kuna wanaume wengine wao wanachojali ni kuingia, kutoka na kukojoa....

wanaume hivi mnajua kwamba wanawake wengi ni vigumu sana kuwafikisha kilele?na pindi wanapopata watu wa kuwafikisha kileleni husahau hata kama wana wapenzi (na hapo ndipo wapenzi wapembeni huanza) raha ya penzi ni wote wawili kuridhika, basi kwanzia leo tujitahidi kuwauliza wapenzi wetu kama wanafurahia na kuridhika na penzi tunalowapa na kama hawatosheki tuwaulize ni vipi hupendelea kufanyiwa ili aweze kuridhika na kufurahia mapenzi yako..

hamna starehe nzuri kama mkifanya mapenzi wote wawili na kuyafurahia.. sio baba unafurahi halafu mama moyoni anawaza utamaliza saa ngapi maana unamchosha bure tu.. hehe

MWANAUME KUWA NA UUME MKUBWA NI MBAYA?


Jamani nina rafiki yangu mmoja kwa jina namuhifadhi, yeye anabwana mmoja ambaye anauume mkubwa sana kwa upana na hata urefu, sasa kila wanapokutana kimwili na rafiki yangu mwanaume yeye anakuwa ana enjoy sana kufanya mampenzi (kumuingilia mwanamke) lakini yeye rafiki yangu huwa anapata tabu sana kwasababu ya ile size ya jamaa.. sasa mwanamke ananiambia anapata tabu sana kufika kileleni kwasababu jamaa akiingia yeye husikia maumivu wakati wote hamna hata chembe cha starehe.. jamani wenye maoni mnakaribishwa.... maana mimi hata cha kumwambia sijui.

WANAUME NA NGUO ZENU ZA NDANI....


jamani wanaume hii ndio fashion ama? maana tumeona wanaume wengi ama sijui ndio wanaitwa mabrazameni kama nilivyoambiwa kitaa.. wao huwa wanavaa nguo chini ya makalio madai yao tuonyeshwe nguo zao za ndani ama? kwakweli that just aint good haivutii hata kidogo tena afadhali wemgine wanaofanya hivyo na kuvaa nguo nyeupe ndani kuliko wale wanaovaa nyekundu, njano, kahawia na rangi hizo nyengine kali kwakweli haivutii...

mwanaume anapendeza akiwa amevaa vizuri sio nguo anatembea anazishikilia chini maana zinataka kumdondoka, ama utakuta saingine anatembea kama amebeba fuko la unga kwenye suruali limemuelemea kwa uzito, its just not right..

ladies jamani unless unapenda mpenzi wako avae hivyo kitozi wenyewe wanaita, lakini if you dont like that style and your man is dressing that way, gal tell him to his face.....

Haipendezi....

SALON ZA KIKE ZINA MAMBO JAMANI................


kweli nimeamini ya kwamba salon za kike zinamambo... jumamosi niliingia salon moja mitaa ya tabata, ndani mule kulikuwa na wateja wengine wengi tu wakitengeneza nywele zao na kucha, mara wakaingia wadada wa wili ni wasichana tu wenye umri kama miaka 25-28 sasa wakiwa salon wanatengeneza kucha kuna dada mmoja akaanzisha story ya kuhusu mapenzi na jinsi gani anavyofurahia mapenzi anayopewa na mpenzi wake..


pembeni ya huyo dada kulikuwa na mama mmoja yeye alikuwa anafanya steaming ya nywele wote tulikuwa tunasikiliza story tukicheka na kuchangia panapotakiwa, sasa cha kushangaza kati ya wale wadada walioingia wawili mmoja akaanza kutoa story ya bwana yake jinsi anavyompenda yani hajawahi kuona mtu kama yeye..

isitoshe huyo dada akawa anajitamba kwamba mwanaume kampangia nyumba, anampa hela ya matumizi, kila anachotaka anapewa, kamnunulia gari na sasa hivi yule mwnanaume anamjengea huyo msichana nyumba pande za kinyerezi..

yule msichana akiendelea kutupa story ya kuhusu huyo mwanaume wake yule mama mtu mzima akamuuliza huyo mwanaume wako ameoa? ama ni mwanaume mwenye mmpango wa kukuoa? yule dada akamjibu bado hawajaongelea hayo mammbo ila tu yule dada ni mjamzito na mimba ni ya yule kaka, ameona ampe zawadi ya mtoto kwa yote mazuri aliyemtendea..

watu wakazidi kuchokonoa story, wakamuuliza sasa huyo mwanaume wako anafanya kazi ama ni mfanya biashara yule dada akaanza kumwaga manyanga na kusema yule mwanaume anapofanya kazi, jinsi alivyokuwa mcheshi, naanaendesha gari gani na mpaka namba na aina ya gari akaitaja na kumalizia na kusema yani nipo tayari kwa kufanya lolote kwa mtu atakaye nichukulia mwanaume huyu..

JAMANI, JAMANI, JAMANI kweli nimeamini siku za mwizi ni forty, kumbe mwanaume wa yule dada ndio mume wa yule mama mtu mzima aliyekuwa pale saloni anafanya steaming nywele yula mama aliposikia mpaka namba ya gari lake limetajwa alicho kifanya ni alitoka kwenye steamer alimpiga yule mwanamke, jamani yule dada alipigwa.....

tukashangaa yule mama akifanya hivyo mara akasema "wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana" kumbe yule mama alishajuwa mume wake anahawara nje, alisha kuta simu akipigiwa mara nyingi sana yule mwanamke na message nyingi sana akituma na kutumiwa yule dada ila tu yule mama hakupata nafasi nzuri ya kumtafuta mpaka Mungu alipowakutanisha salon siku hiyo...

yule mama akampigia mumewake simu amfwate ile salon alipo kwani walikuwa wanakaa jirani, makusudi tu ili amuone mume wanke angefanyaje kumuona yule hawara pale akiwa amepigwa basi yule baba kufika tu pale salon alivyomuona yule mke wake na hawara akadondoka na kuzimia...

sikutaka kufwatilia zaidi baadada ya mume kuanguka ila nikipata hiyo story ilivyokuwa baada ya pale nitakuja kuiandika tena, maana nitaenda tena ile salon...

kweli nimeamini za mwizi zikifika zimefika...

Friday, May 14, 2010

WOMEN AND PREGNANCY







lazima tukubali yakwamba wakati wa mimba ni wakati mzuri zaidi katika maisha yetu, kugundua kuna mtu mwengine ndani ya tumbo lako ni upendo ambao hauwezi kusimuliwa..

tuliona wananwake wa zamani pindi wanapokuwa wajawazito sio wote walipenda bado kujipendezesha miili yao, labda ni mimba zinawafanya wawe wavivu kuvaa vizuri, kujipamba, kutengeneza nywele, n.k

pregnancy ni kipindi tu cha kupita cha kumleta mtoto duniani sio kitufanye tusijipende, tusione ya kwamba kwasababu nina mimba basi ninaweza nikaacha kujitunza, hapana... tujitunze vizuri na kwa usafi ili tupendeze wakati wote wa miezi tisa...

huo ndio uwanawake wa leo..

Thursday, May 13, 2010

BARAKA ZA WATOTO




KHLOE MIZIZI


watoto hutupa baraka nyingi sana katika nyumba, nikupitia hao watoto familia zetu husimama imara, watoto hufuta ugomvi unapotokea kati ya wazazi, watoto hukaa nasi kutupatia tabasamu tunapokasirishwa, watoto hutuuguza wakati hakuna mtu mwengine wakutuuguza tukiumwa, watoto hutupa heshma pindi wanapo oana, watoto hutupa furaha zaidi wanapotuletea wajukuu, ni mambo mengi sana naweza kusema kuhusu watoto yasitoshee kwenye blog hii..

natambua maumivu ya watu wasio na watoto, vilio vyao wakinyanyaswa iwe na wakwe ama mawifi, japo huweza kuchukua muda kwakuwa Mungu ndio hutupa watoto basi tusichoke kumuomba watoto..

kwenye vitabu vya Mungu tunaambiwa mke wa Abraham alipata mtoto wake akiwa na miaka 80 basi nasi tusikate tamaa bado tumaini lipo.

kwa muda wake, na wakati wake Mungu atatupatia tusinyanyasane, wala tusichekane pindi watu tunaowafahamu wanapoishi muda mrefu bila watoto..

KUNYONYESHA MTOTO



ROSEMARY AND KHLOE MIZIZI

hakuna jambo zuri kama kumnyonyesha mtoto wako, haswa kwa mara ya kwanza kuna kama uoga na furaha kwa wakati mmoja, mwanangu khloe nakumbuka nilivyoanza kumnyonyesha mara ya kwanza nililia kwasababu alikuwa anajitahidi kula kwani alikuwa na njaa na akilia muda wote.
kwa wamama na wadada wenye watoto wengine huogopa kunyonyesha kuhofia maziwa yako kulala na kuhisi yakiwa yamelala hautakuwa na mvuto, nataka nikujulishe ni mvuto gani utakuwa nao wewe mzuri zaidi ya mvuto wa watu kujua unamtoto!!!!!
sasa wewe unayekataa kumnyonyesha mwanao hebu fikiria kuna watu ambao wanalia na kunyanyasika kwasababu tu hawajahimili maumivu na kuwa na huyo mtoto wa kumnyonyesha basi tujitahidi katika kuwapa watoto wetu afya kupitia ziwa la mama..
huyo aliyekupa mimba atakuthamini zaidi utakapomkuza mwanae vyema, kwasababu miili yetu baadae itanyauka kwa uzee lakini watoto wetu siku zote watatuletea furaha, upendo na amani nyumbani..

TABASAMU TOKA MOYONI

ROSEMARY MIZIZI

watu husema ukitabasamu ama kucheka unaongeza siku zako za kuishi duniani..

tabasamu katika nyumba nikitu muhimu sana sio tu hukufanya upendeze bali huongeza upendo katika familia na watu wanaokuzunguka ndio maana mara nyingi huwa tunajitahidi kufanya ama kuongea mambo ambayo yatafurahisha watu tulio kuwa nao karibu.

tabasamu la mpenzi wako ni tofauti na la rafiki yako, ukiwa na mpenzi wako ni vyema ukafurahi kutoka moyoni, kwani ni ndani ya moyo ndio upendo wenu huanzia, hatakama watu wametukwaza, hatakama mpenzi amekukwaza, kumbuka ukimpuuzia na kutabasamu huwa ile hali ya hasira hutoweka kabisa.

mke hupenda kumuona mume wake akitabasamu na mume pia hivyo hivyo, basi tusinyimane furaha ya tabasamu.


Wednesday, May 12, 2010

DADA SALMA ANAOMBA USHAURI WENU

kuna dada amenitumia mail through facebook, anaomba apewe ushauri, anasema yeye ni mdada wa miaka 28 na ameolewa miaka mitano iliyopita na ana watoto wa tatu, kilio chake yeye ni kitu kimoja miaka miwili ya kwanza ndani ya ndoa yake ilikuwa mizuri sana na yenye upendo mwingi kati yake na mumewe lakini ghafla mwanaume akaanza kubadilika akawa muhuni akawa anawanawake (girlfriends) wa chuo na hata kazini kwake ikafika kipindi huyo baba japo ni mtu mzima anafanya mambo ya vijana mpaka ana save majina ya wanawake kutumia majina ya wanaume kama mary anamuandika matthew, salma akagundua na baada ya kumueleza mumewe kuhusu tabia hiyo mumewe akaomba msamaha na salma akakubali kumsamehe kwani ni mumewe hana cha kufanya, lakini cha kumshangaza salma nikwamba yule baba hakuacha ile tabila bado aliendelea nayo kwa siri, na pia akaanza kurudi asubuhi nyumbani watoto wakimuuliza anasema alikuwa kazini akitafuta ada yao ya shule mkewe akiuliza anamwambia hayamuusu ajue tu ametokakazini salma anasema huyo mumewe hakosi visa akiacha hichi anaanza chengine anaomba ushauri afanyaje na anawatoto nae wakati yeye anaogopa magonjwa??? ama ahamue kuachana nae??

MNENE LAKINI BADO MZURI


HII NI KWA WANAWAKE WOTE WANAOJIHISI NI WANENE NA HAWAPENDEZI...

swala la unene limekuwa kubwa sana hapa duniani, tunasikia na kuona kwenye vyombo vya habari watu wanatumia madawa ili wakonde wengine hata kwenda hospitali kupunguza sehemu za miili yao.
lakini cha kushangaza nikwamba watu hukimbilia wembamba lakini hawataki kukubali kwamba hata ukiwa mnene unaweza onekana mzuri kwa kujivalisha nguo zitakazokupendeza zisikushike sana mwili kwasababu zikikushika mwili basi utaanza kujisikia hukai vizuri na nyama za mwili wako kujikunja pamoja na nguo na kukufanya ujione mnene na uuchukie mwili wako..

ukiachana na hayo tunajua nguo nyeusi humfanya mtu kuonekana mwembamba japo chini ya umbile lako kidogo basi akikisha hukosi nguo nyeusi pia hutupa ujasiri..

mwanamke yeyote awe mwembamba ama mnene anapojipamba vizuri huonekana mzuri sana hiyo pia ni silaha kubwa.

kwahiyo haina maana kuogopa na kukaa bila raha kisa tunaogopa watu wataongelea unene wetu tunaweza kuwa wanene lakini tukavaa na kujipamba kama hao wenye miili membamba nakuonekana wazuri kama wao na hata mara nyengine kupendeza zaidi yao.

NDOA ZETU......


jamani hivi tunajua maana ya hizi pete za ndoa ama tunazivaa tu kama urembo..? hebu tuongelee swala la ndoa wengine husema ndoa ni bahati, wengine husema ndoa ni zali, na mambo mengine mengi tu..
lakini kwa upande wangu naamini ndoa inastahili kwa kila mtu na sio bahati wangapi tumewaona wanaoa na kuolwa na miaka 40 hata 50? katika vitabu vya Mungu vinasema Mungu alimuumba mwanaume na katika mbavu zake akamtoa mwanamke na kama ni hivyo basi kwa kila mwanamme kuna mwanamke ni muda tu wa yeye kutokea.
lakini nashangaa siku hizi wanaume na wanawake wengine wameoa lakini bado wanataka cha pembeni sasa ukienda kuchukua mwanamke sio wako huyo mume wake atampata lini???
wenyewe waitwa "vidumu" ndio wanawake na wanaume wanavyojidangaya kama wewe kidumu basi huyu mwanaume ama mwanake wako anayekufanya kidumu atakuwa hakupendi kwanini usingewekwa ndani ukawa wa ndani ama tank kama wanavyoitwa wanaume ama wanawake wenye ndoa..
wapembeni atabaki kuwa wapembeni siku zote na utakapo pata shida na magonjwa hatakudhamini cha zaidi atakuacha na kufwata mwengine kilichobaki ni tuheshimu ndoa zetu na wale tuliowachagua kwakuwa ndio watakuwa nasi kwenye shida na raha kwani ni wao tuliowachagua na kuapa nao kanisani.....

mume wa mtu ama mke wa mtu kuwa mchumba wa mtu mwengine inahusu???

Night Dresses




Now lets talk about night dresses..

naamini ya kwamba muda wa kulala ni mda wa kupumzika na hutaki kulala ukiwa umevaa suit yako ya kazi ama umevaa jeans.. ndio maana wakati wa kulala watu huwa tunapenda kuvaa nguo ambazo zitatufanya tusisikie joto, nguo ambazo hazitatubana sana nguo ambazo hupendeza mwili wakati wa usiku.

wanawake tulio na waume ndani hatutaki kulala tukiwa tumefunga kanga ama vitenge ama kulala umevaa bukta, vaa kitu chepesi chenye mvuto ambacho hata mwenzi wako atakapokuwa amelala pembeni yako basi asitake kuamka alale apumzike kabisa tu atakapo kukumbatia usiku ukiwa mwepesi sio kumkwaruza na pindo za jeans ama kanga kufunguka wakati anakuvuta pembeni yake..

wanawake tunaweza kufanya kila usiku uwe kama usiku wa kwanza na mwenza wako..

MWANAMKE JIKO


Mengi huwa tunafundishwa kuhusu jikoni iwe na wazazi, marafiki ama hata kwenye kitchen party mengi tunaambiwa kuhusu jikoni na tunajua afya zetu zinatokana na majiko yetu hata yakiwa ya kifahari sana ama hata ya kawaida.

mwanamke jiko bwana liwe katika kupanga ama kupika.. ilimradi majiko yote hutoa chakula chenye afya basi aihusu kama jiko lako ni la kifahari ama labei ya chini.. tunachojali afya ipo??????

CHUMBANI.... mmmhhhh CHUMBANI


naamini baadaya ya siku ndefu kutafuta riziki, na baada ya siku ndefu kuongea na watu tofauti, kukasirishwa na watu tofauti na wakati mwengine inafika mda mwili wako unakuwa umechoka unachohitaji na kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani.. wengi nimesikia wakisema huwawia vigumu kupumzika vizuri kitanda kingine tofauti na alichonacho nyumbani.. sababu ni kwamba labda godoro la nyumbani ni zuri kuliko sehemu nyengine ama tu ukilala nyumbani unapumzika vizuri zaidi ukiwa pembeni ya mtu aliyekaribu na moyo wako..

ndio swala la chumbani linapoingia, sehemu ya kulala hupaswa kukufanya uchovu uliokuwa nao wote kutoweka, chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi vya kufanya hata hewa isiingie, sijui viatu, kapu la nguo chafu, ma vengine vingi.

hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda eote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa.

chumbani mambo mengi sana hufanyika ukiacha kulala, hata kupumzika tu na mwenzi wako mkiongelea mambo fulani ya maisha yenu. kwahiyo hutaki kufanya hivyo na harufu mbaya ikiwapitia pembeni.

WELCOME NOTE


Kwa Ujumla nataka kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wote kwenye tovuti hii.. mwanamke na nyumba ni tovuti inayoongelea maswala ya nyumbani kwa ujumla iwe mambo ya kuelimishana cha kufanya nyumbani, iwe mahusiano katika nyumba kwa mume na mke na hata ushauri kwa
wanaoingia katika ndoa na sio hilo tu bali hata kwa watu wasio na ndoa na mtu mwengine yeyote mkubwa ama mdogo anaye thamini nyumba yake.

mimi ni mama na pia ni mke kwahiyo ikija kwenye swala la nyumba hamna ambacho kitakuwa kigeni kwangu. basi wote kwa ujumla tuungane pamoja kwa kupeana mawazo pamoja na mafunzo kwani nyumba za zamani ni tofauti na nyumba za sasa japokuwa mara nyingi ujenzi ni uleule.

Ahsanteni kwa ushirikiano.

Tuesday, May 11, 2010

MEZA YA CHAKULA

Mpangilio mzuri wa meza ya chakula katika nyumba huvutia walaji wa chakula chako ulicho andaa. Pindi sehemu ya kulia inapokuwa chafu na katika mpangilio usio nadhifu unakuwa ni kero kwa watumiaji.