Monday, May 31, 2010

MKE KUWA NA UHUSIANO NA HOUSEBOY......

kuna kisa kimoja kimemtokea kaka mmoja hivi karibuni, ameoa mke mzuri tu na wanawatoto wawili, wanaishi mitaa ya mbezi samaki wa bichi, huyu kaka kweli ni mtanashati kwa uzuri tu acha nimsifie kwani namjua nakumbuka pindi alivyokuwa shule wanawake wengi sana waligombana kwa sababu yake..

huyu kaka na familia yake wanaishi kwenye nyumba kubwa sana, yeye ni mfanya kazi na mkewe ana duka tu la nguo karibu na nyumbani kwao kwahiyo muda mwingi huyu mama yupo nyumbani, sasa hawana house girl kwani mama hufanya kazi zote halafu baadae ndio huenda dukani, lakini kwasababu nyumba yao ina garden kubwa yenye kila aina ya maua wakaamua kuajiri house boy wa kuitunza ile garden..

kwa mduda mrefu yule house boy alikuwa anafanya kazi vizuri sana, wakakaa miaka karibia sita na huyu kaka tokea akiwa kijana mdogo mpaka mkaka, alivyozidi kukuwa alizidi kumvutia yule mama, halafu ukiangalia kijana always yupo fit kimwili, akienda kufanya kazi zake huvaa kaptula fupi na vest akionyesha vitu ambavyo Mungu amemjalia..

ikafika kipindi yule mama akajikuta hawezi kuvumilia tena, kwa bahati mbaya mumewe akapata safari kikazi, lakini kwa huyu mama huo ndio ulikuwa muda mzuri wa yeye kumpata house boy, baba alivyoondoka mama siku moja akamwagia mtama kuku, akamueleza kijana jinsi alivyotokea kumpenda , na kijana kwasababu alikuja kutafuta pesa akajua atakapokuwa na huyu mama atapata pesa nyingi kuliko anazopata kutengeneza bustani..

kijana akaingia mkenge, akamkubalia mama siku hiyo wakapanga waende kulala hotelini mchana kwani watoto wakirudi watakaa na dada kama kawaida, kijana akajiandaa bwana kufika hotelini akampa mama shughuli ambayo hata baba hampi hivyo.. (Duhhhh pesa hizi jamani)

mama siakanogewa bwana, ikawa ndio mchezo wao, sasa kwa vile yule house boy alikuwa anakaa mule kwenye ile nyumba mama akawa hata kwenda hotelini anaona anapoteza muda akawa anajimiminia tu mzigo mule mule nyumbani kwa mumewe mbaya zaidi chumbani kwa mumewe..

siku hiyo bwana baba kule safari alipokuwepo akaona awahi kurudi nyumbani kwani ameikumbuka familia yake, akarudi nyuma ya siku aliyokuwa kamwambia mkewe atarudi, kwani watoto mda huo walikuwa bado hawajarudi na mama na kijana kama kawaida wapo chumbani, jamaa kufika akaamua kwenda moja kwa moja chumbani ili aoge akamfwate mkewe dukani, jaaaaaaniiiii kufungua mlango hehe asimuone mama juu ya kijana anashughulika, mbaya zaidi anamwambia kijana yani raha unazonipa hata mumwe wangu hanipi hivi....

jamni yule kaka alicho kifanya ni kudondosha begi alilobega ndio likawashtua wale wawili, kijana kuona hivyo akataka kukimbia lakini yula kaka akamdaka na kumrudisha chumbani, wote wakiwa hawana nguo kaka akawapa adhabu waendelee kufanya alicho wakuta wakifanya......

wawili wote walishindwa, yule kaka chakufanya akamwambia house boy aondoke, na kwa mkewe hajawahi kumwambia kitu chochote wala hata kumpiga na mpaka leo ni wiki ya pili hii yule kaka hajawahi kuongelea kitu chochote kuhusu hilo swala, mke wake sasa ndio anachanganyikiwa anaomba hata yule baba japo ampige yani kachanganyikiwa na kurudi kwao hawezi kwani familia itamchukulia vipi..

huyu kaka alikuja kunihadithia huu mkasa, anasema mpaka leo hajui afanye nini kama amuache mkewe ama ampige, kwani anaogopa akimuacha wanawe itakuwaje na akimpiga anaona linaweza kuwa balaa akiua je?

jamani mwenye ushauri uwanja wako..

2 comments:

  1. Kama ni kweli kisa hicho kimetokea, na kama ni kweli huyo kaka hajaongea na mkewe kwa wiki mbili sasa, cha kufanya ni kwanza kujiuliza yeye mwenyewe ni msafi kiasi gani, yaani je yeye anapokuwa huko safarini kwake hachukui vibinti ?? Kama na yeye anachukua basi aongee na mkewe amwambi kuwa waache huo mchezo. La sivyo waendelee tu na maisha yao, kama awali

    ReplyDelete
  2. mi kwa mtazamo wangu naona huyo kaka amwambie tu mkewe kuwa kaamua kumsamehe kwani likitokea tena basi ajue wazazi wake wata mkuta maiti kwani naona ameshaamua kusamehe basi na sidhani kama huyo mwanamke atarudia tena...

    ReplyDelete