naamini baadaya ya siku ndefu kutafuta riziki, na baada ya siku ndefu kuongea na watu tofauti, kukasirishwa na watu tofauti na wakati mwengine inafika mda mwili wako unakuwa umechoka unachohitaji na kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani.. wengi nimesikia wakisema huwawia vigumu kupumzika vizuri kitanda kingine tofauti na alichonacho nyumbani.. sababu ni kwamba labda godoro la nyumbani ni zuri kuliko sehemu nyengine ama tu ukilala nyumbani unapumzika vizuri zaidi ukiwa pembeni ya mtu aliyekaribu na moyo wako..
ndio swala la chumbani linapoingia, sehemu ya kulala hupaswa kukufanya uchovu uliokuwa nao wote kutoweka, chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi vya kufanya hata hewa isiingie, sijui viatu, kapu la nguo chafu, ma vengine vingi.
hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda eote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa.
chumbani mambo mengi sana hufanyika ukiacha kulala, hata kupumzika tu na mwenzi wako mkiongelea mambo fulani ya maisha yenu. kwahiyo hutaki kufanya hivyo na harufu mbaya ikiwapitia pembeni.

Swadakta dada, tena kwa nyongeza Chumba chako cha kulala ni mahala patakatifu sana hivyo usipo patunzsa utakatifu huo hutoweka na mwisho wa siku chumba kukiona kama jehanamu. Sasa kwanini wewe mwanamke chumba chako na mumeo kiwe Jehanamu.Kitunze nacho kikutunze hadi ifikie mahali baba au mama unahamu ya kurudi mapema nyumbani maana kuna kitu unahamu nacho, mandhari nzuri ya chumba hatakama kidogo lakini mama anakitunza vyema.
ReplyDeleteJambo la hatari ni chumba cheni kukifanya jalala na mtaa wa wapita njia. Hii namaana kuwa JALALA ni kutupa tupa vitu hovyo, viatu chini ya kitanda na nguo chafu kila pahala ukutani na kila kona. Pia MTAA ni pale ambapo Chumba chako kina kosa kusitiri mambo ya Mke na Mume. Watoto wanakimbizana hadi kujificha chumbani kwa baba na mama, Housegirl nae kila saa anaingia chumbani kama kwake, Kitanda anatandika huyohuyo Housegirl "Beki tatu" ni dharau kubwa sana kwa mwanamke katika chumba chako wewe na mumeo.
Piga marufuku tabia hiyo mara moja maana ni hatari sana, mtoto akisha fikia umri wa kuanza shule chumbani kwa wazazi apaone sehemu ya hatari na aingie kwa sababu maalum tu.
Alamsiki. FK.
FK
ReplyDeletehapo somo naona umelielewa vizuri, sasa kwa watu wenye watoto wadogo na nyumba zao ndogo ni muhimu kucha chumba wazi ili housegal aweze kumlaza mtoto chumbani kwa mama siunaelewa tena maisha yetu ya kibongo.. ila kweli mtoto akishaanza shule hapaswi kuingia tena ovyo chumbani kwa wazazi mara kaona something wrong anaenda kuhadithia watoto wenzake.. itakuwa aibu
Jambo jingine chumbani panakosa stara, kwani wanawake wengine pindi mumewe akitoka tu, hupafanya mahali pa kukaa na mashoga anaodhani yeye ni wapenzi na wasiri wake kuweza kuteta mambo yao ya msingi na mengine yasiyo na maana. Ni vibaya kwa mwanamke kuwaita mashoga zake nyumbani na kujifanya kuongelea mambo yao ya madili chumbani eti kuepuka watu wengine sebuleni au kwingineko nyumbani hapo kuweza kwenda na movie ya mazungumzo yao. Chumba ulalacho na mumeo hakipaswi kuonekana na mashoga au watu wengine unaodhani ni maswahiba zako bila sababu yoyote. Hakuna haja ya kuonyeshea ufahari chumba chako. Vinginevyo unatafuta balaa toka kwa hao mashoga zako.
Deletemwenzangu hilo ndio la muhimu haswa maana sehemu ya kulala ikisha songamana na mavitu mengi lazima na usungizi uwe wa kuunga unga na nani wakufanya hayo maswala ya usafi ni sisi wenyewe wanawake.tunashukuru sana mpenzi kwa kuja na vitu vipya na kukumbushana majukumu mahana ...........
ReplyDeleteni kweli tupu mapenzi ni afya njema,usafi,kuheshimiana.
ReplyDelete