Wednesday, May 12, 2010

DADA SALMA ANAOMBA USHAURI WENU

kuna dada amenitumia mail through facebook, anaomba apewe ushauri, anasema yeye ni mdada wa miaka 28 na ameolewa miaka mitano iliyopita na ana watoto wa tatu, kilio chake yeye ni kitu kimoja miaka miwili ya kwanza ndani ya ndoa yake ilikuwa mizuri sana na yenye upendo mwingi kati yake na mumewe lakini ghafla mwanaume akaanza kubadilika akawa muhuni akawa anawanawake (girlfriends) wa chuo na hata kazini kwake ikafika kipindi huyo baba japo ni mtu mzima anafanya mambo ya vijana mpaka ana save majina ya wanawake kutumia majina ya wanaume kama mary anamuandika matthew, salma akagundua na baada ya kumueleza mumewe kuhusu tabia hiyo mumewe akaomba msamaha na salma akakubali kumsamehe kwani ni mumewe hana cha kufanya, lakini cha kumshangaza salma nikwamba yule baba hakuacha ile tabila bado aliendelea nayo kwa siri, na pia akaanza kurudi asubuhi nyumbani watoto wakimuuliza anasema alikuwa kazini akitafuta ada yao ya shule mkewe akiuliza anamwambia hayamuusu ajue tu ametokakazini salma anasema huyo mumewe hakosi visa akiacha hichi anaanza chengine anaomba ushauri afanyaje na anawatoto nae wakati yeye anaogopa magonjwa??? ama ahamue kuachana nae??

3 comments:

  1. salama ...
    kuwamvumilivu tuu.. mana ukisema uchane nae nini itakuwa adhima ya watoto??
    japo kuna marathi dunia imekuwa si yenyewe tena, lakini jaribu kuwaingiza wakwe kma inawezekana ilikupata ushauri zaidi .. au kaakitako uongee na mumeo mueleweshe yaliyo moyoni , msikilize reaction yake kama ukiona hana mwelekeo dada angu bora usamabe urudi nyumbani maana mwisho wa siku unaweza kujikuta umelazwa hspt kwaajili ya marathi ya siku hizi ... alafu watoto wako wakabaki wakiteseka..
    pia walimwengu wanasema asiyefunza na mamae hufuzwa na ulimwengu.. ukishamsikiliza
    kaa chini fikiria what ur goin to do kwaajili yako na watoto ... then make a step and mdharau kwa anayoyafanya muone mjinga end of the day yeye ndo ataye jione mwehu and atajirudi... kama huna kibarua basi tafuta hata kama kujishikisha kwenye maduka ya watu ukawa part timer sio mbaya as long as unapata riski na hutakuwa unamtegemea mumeo sana .... hope ol goes well with ur marriage otherwise pole na misuko suko .. hiyo ndo mitihani ya maisha!!
    ... frm ley kijeti(hope umenitambua rose)

    ReplyDelete
  2. pole dada kwa yanayo kusibu lakini kitu muhimu kwakumrudisha mumeo kwako na utamu wa ndoa kwako ni lazima ujiandae wakati wake na wakati wa watoto , sio unakua unawaangalia watoto tu yeye huna shughuli naye lah hivyo sio inavyo takikana , ulipokua mwanzo wa ndoa anakupenda nikwasababu ulikua unawakati nayeye sasa hivi hanashughuli nawewe ila msaada wangu kwako ni naomba kama mumeo akirudi nyumbani hakikisha umejiremba, msafi umemuandalia chakula kizuri na chumba chako kiwe kisafi kwahali ya juu . akirudi nyumbani usiwe mwenye kumuliza mwaswali kama unatoka wapi ? lah jaribu usiwe mwenye hasira na wala usimjali . angalia maisha yako . naye hapo ataona kama ulikua na mwanaume mwengine na wala hata huna shughuli hiyo . na kwa haya inshaallah mungu atakusaidia

    ReplyDelete
  3. mwache tu tafuta mwingine u are still young bwana!

    ReplyDelete