Tuesday, December 27, 2011

Rose, yani housegal wangu anakichaa anataka kuniletea balaa, tena balaa kubwa mwenzio nimesafiri miezi miwili nikamuacha mume wangu na msichana wa kazi pamoja na watoto wangu sasa nimerudi simuelewi kabisa house gal wangu mara anatapika, anachelewa kuamka, mara anakula halafu mda wote yeye ni kulala hana habari hata na wanangu.

Nilipomuelezea dada yangu akaniambia tumchukuwe tukampime mimba loooo kweli tukamkuta ni mjamzito, nikambana sana aniambie ule ujauzito ni wa nani akagoma ukapita mwezi siku moja nikamfokea kweli kunakazi hakufanya vizuri basi akaniambia unanifokea nini wakati kama hii nyumba yako nami ni yangu kama ni watoto na mimi ni nanaye na kama ni baba na huyu wangu baba yake ndio huyu aishie humu ndani.(NILIHISI KUCHANGANYIKIWA) ghafla nikawa mpole kama nimemwagiwa maji ya baridi nilihisi nahishiwa pumzi kama nataka kuzimia.

Nilichokifanya wala sikumuuliza mume wangu kwani najuwa angekataa, nikatulia kwanza kesho yake nikaenda kumuona tena dada yangu na kumueleza yaliyotokea, akaniambia angekuja kuonana na housegal wangu na kuongea naye, basi kweli alikuja tukamkalisha yule dada chini na kuongea naye kwamba yule baba ni muongo wala hatamuoa kwani ameshaoa na mambo mengine kibao ya kumkatisha tamaa na kumshauri akatoe ile mimba kwasababu bado ndogo.

Yule dada akasema jibu nitawapa kesho, ngoja nikafikirie bila kujuwa alienda kumueleza mume wangu na akamwambia asitoe, na atampangia chumba ili akae na mwanaye na atamlea yule mtoto (yani huyu mwanaume kachanganyikiwa), basi kesho yake dada akatueleza kwamba hawezi kutoa ile mimba, tukaondoka tukajipange upya ili tumfwate tena.

Keshokutwa yake tukamfwata dada na kumwambia kwamba unadhani huyo mtoto wako akizaliwa atapata matunzo imara kama ya watoto wangu ukiangalia hujasoma wala huna ujuzi wowote siku hizi wanaume wanapenda wanawake wa kuwasaidia maana hata akikupangia chumba huyu msichana atakayeajiriwa hapa ataliwa na kupewa mimba kama wewe(basi yale maneno ya kamuingia akilini na kujikuta analia) akaomba msamaha nikazidi kumponda mume wangu kwamba wanaume hawa hawana maana ni waongo na mambo mengine kibao...

Basi yule dada akakubali tukampeleka akaitoa ile mimba maana nilimwambia ukiitoa utarudi kufanya kazi hapa na nitakuchukulia kama mdogo wangu utaishi kwa raha nitakupa na hela zaidi, basi alivyopona tu baada ya kutoa ile mimba nikambadilishia line ya simu yake asubuhi nikampakisha mizigo na kumpeleka ubungo na kumpandisha gari la kwao kwenda singida, anitolee balaa umekuja kufanya kazi ama kuhudumia mume wa mtu.

Mume wangu kurudi anamuuulizia dada nikamwambia keshaondoka na namba pamoja na simu nimembadilishia mimi mwenyewe siijui, akabaki anaduwaa na aibu maana wakati wote huo sikumuuliza chochote mume wangi mpaka niwe nimelitoa hilo jini nikamgeukia yeye sasa kilichomsababisha kama kawaida yao Rose ananiambia shetani kisa nimesafiri muda kikazi akawa akisikia hamu anamalizia kwa dada siku akajisahau akaingia bila condom ndio mimba..

sasa najiuliza hii nikusafiri miezi miwili nikipewa safari ya zaidi ya miezi miwili si nitakuta mwanamke ndani mwangu, jamani wanaume kwanini mnakuwa na mioyo ya ukatili bado unatoka nje ya ndoa halafu unafanyia ufuska ndani ya nyumba ya mkeo hata heshima kwake huna pia haipendezi...

Reactions:

5 comments:

 1. pole sana aunty.ila ujiandae kwa chochote kwani uliweka mikono yako kwenye damu icyo na hatia..mmemuua mtt wa wa2 bure akiwa hajui hta kinachoendelea...na dunia ndogo siku moja huyo dada anaweza kutana na mumeo..

  ReplyDelete
 2. katika vyote ulikosea kutoa hiyo mimba ya hicho kiumbe,kiumbe kilichokuwa tumboni kilikuwa hakina hatia yoyote,umeonyesha jinsi gani roho yako ilivyo,mwanamume wako huwezi kumzuia kufanya chochote akitaka kufanya ungetumia tu busara ya kumrudisha huyo binti kwao bila kutoa hiyo mimba,ukadeal na mumeo,Pole,ila kuwa makini hii kitu itakurudi tu.kiumbe usingeuua

  ReplyDelete
 3. Wewe dada umemuua ndugu ya watoto wako kisa mwanaume? Utawaua wangapi sasa maana hujui huko mtaani kama ana watoto wengine au hapana. Unafikiri hivyo ulivyofanya umemkomesha mumeo au ndio umemsaidia kusolve hilo soo ili aendelee kuchezea wasichana wengine?

  Hivi pamoja na kazi unayofanya bado uko desperate kiasi hicho kuwa huwezi kuishi bila huyo mwanaume au? Ni mali au nini kinachokuweka hapo? Kwani kama ni mapenzi sidhani kama unampenda huyo baba kwani ungekuwa unampenda usingemuulia mtoto wake ambaye hujui angekuja kuwa nani hapa duniani au pengine angekusaidia wewe mwenyewe.

  Mimi bwana nisingemfukuza huyo msichana ama mie ningemuacha huyo kicheche au kama nimeamua kufa na huyo bwana basi huyo msichana angekaa humo humo ndani mpaka akazaa kisha mtoto angesogea kidogo tu ningemrudisha kwao nikamuacha yule mtoto humo humo ndani ili kila siku huyo baba anapoamka asubuhi aone matunda ya dhambi yake! Ningeleta kaka wa kunisaidia kazi za ndani na kumsaidia na yeye pia shughuli ya kitandani!!!

  ReplyDelete
 4. ama kweli shetani ni shetan tu yaan uhuru ulomuachia mumeo baada ya kusafiri shetanikaingilia kati kaivuruga nyumba kafanya kila anachojua house gal kabeba mimba,aisee dada hata kama ikatokea hivo unatakiwa kusimama katika maombi na ungekuwa mtu wa maombi hata hiyo mimba usingeitoa na ungeendelea kumshukuru tu Mungu
  nakushauri uokoke na utubu kweli na umuweke mumeo katika maombi hakika Mungu atafanya njia na kuwa mlinzi wa mumeo popote aendapo na ndipo nawe hutakuwa na wasiwasi hata usafiri mwaka mzima ukitumaini Mungu yuko kufanya jambo kwa ajili ya ndoa yako na familia yako kwa ujumla dada yangu.

  ReplyDelete
 5. nyiemnaomlaumu huyu mama pia mna makosa, ukishaingia kwenye situation kama hiyo ndio utajua reaction inakuwaje. Mwingne angeweza hata kuua mumewe na huyo hawara yake. Pole sana omba Mungu na atakusaidia kuilinda ndoa yako

  ReplyDelete