Friday, December 23, 2011

Dada Rose,

nakushukuru sana kwa blog hii yako ambayo huwa kama mwanamke nasoma sana mada za humu kwani naamini kwamba siku moja nami nitajaolewa basi nini nifanye na nini nisifanye nikiwa na mume wangu.

kwasasa kweli nina mchumba ndio tunapendana sana lakini tatizo ni kwamba mchumba wangu huyu ni mtoto wa mbunge mmoja hapa mjini na kwao wanapesa sana wakati mimi mama yangu mwalimu na baba yangu ameajiriwa kwenye kampuni moja hivi hapa mjini.

Mchumba wangu japo kwao ndio wanapesa sana lakini hata siku moja sijawahi kumuona kama anaringa ama kama ananichukulia poa kwasababu matabaka yetu hayalingani na hata kama tukiwa na marafiki zake ambao wao pia wanahela zao hanifanyi kabisa kuonekana kama mimi wakawaida tu.

Nguo na mahitaji ya hapa na pale kwakweli sio mchoyo ananitimizia sana tu na ninamshukuru MUNGU kwa hilo tatizo ni kwamba sasa anataka tuoane kwahiyo anataka kuja kwetu nikamwambia acha kwanza niende kuwataarifu wazazi wangu, maana simnajuwa sio heshima wazazi kujuwa kama unamwanaume mpaka tu wakati akitaka kuoa?

Nilipofika kwa wazazi wangu nikawaeleza kwamba nina mchumba na wakafurahi sana, ilipofika wakati nawaeleza mchumba wangu ni nani na ni mtoto wa nani kwakweli wazazi wangu wakabadilika haswa baba akawa mkali sana na kuniambia ndio ni mchumba wako lakini huwezi kuolewa naye kwani wale unajuwa wanapesa sana usije kwenda huko ukateswa mwanangu kwakuwa sisi hatuna hela, usimuoe tafuta tu kijana mliolingana tabaka wacha hela zifwate hela zenzake!!!!!!!!!!!!

Kwakweli nilisikia kama moyo unataka kupasuka, yani kwasababu wazazi wake wana hela kuliko wangu ndio nisiolewe naye, wakati mwenyewe tatizo hilo wala halioni kweli kabisa wazazi wangu wamekataa yule kijana asinioe na kama siwasikilizi wamesema hata nikiolewa naye hawatakuja kwenye harusi yangu na wala hawatanifanyia send off maana hawajaridhia mimi kuondoka na huyo mwanaume!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nimeachwa njia panda ndio wale ni wazazi wangu lakini yule ni mpenzi wangu pia nampenda nifanye nini mimi?



4 comments:

  1. pole sana dada kwa majaribu haya piga magoti na kumwomba Mungu akutangulia na hato matatizo na aweze kukutatulia kwani yeye hashindwi na jambo lolote napia tafuta watu wazima wenye hekima ambao unajua wanahekima na heshima zao ambao utawaeleza jambo hili na wao wataenda kuzungumza na wazazi wako kwa busara tu naona yatawezekana tu kwani kigezo cha utajiri ambao wazazi wako wanasema mimi naona ktk mapenzi swala la kutofautia kimapato halina nafasi kama wahusika wamependana kwa dhati wanatakiw wazazi wako wakubaliana wewe na waombee baraka ndoa yenu hii mambo yakuchaguliana wachumba umepitwa na wakati pole dada usichoke kusali kwani unahitaji pia baraka toka kwa wazazi ikishindikana washirikishe wazee wa dini yako

    ReplyDelete
  2. Pole sana.(Mwenyezi Mungu huwafanya baadhi wawe maskini na baadhi wawe matajiri. Wengine huwashusha na wengine huwakweza, 1Samweli 2:7)Haya ni mameno kutoka kwenye Biblia. Binadamu hata siku moja hatulingani, hata kama ni mapacha lazima kutakuwa na utofauti in terms of characteristics.Kila binadamu yupo Unique. Mungu huyohuyo aliyewaleta wazazi wako hapa duniani ndo huyohuyo aliyewaleta wazazi wa mchumba wako.Sisi kama binadamu hatuna majibu ya kwanini upande mmoja wana uwezo na mwingine hawana uwezo. Na tukianza tafuta sababu hatutapata majibu. Kwasababu majibu anayo Mwenyezi Mungu aliyetuleta hapa duniani kwani yeye alijua maisha yetu yatakuaje kabla hata hatujatoka kwenye matumbo ya mama zetu. Mimi binafsi naona wazazi wako wanamakosa labda kama wanakigezo kingine ambacho kina uzito kuliko hilo walilorepresent kwako.

    Nakushauri utafute ndugu wa karibu, tena watu wazima wenye upeo mkubwa kuhusu maisha na wanaomjua Mungu waende wakaongee nao.Ikiwezekana hata kiongozi wa dini mtafute akaongee nao.

    Je kama ingetokea kwenye familia yenu kuna mmoja wenu kajaliwa na Mwenyezi Mungu na ana uwezo mkubwa kupita watoto wengine wangemkana kwa sababu nyie wengine hamna uwezo? au huyo mwenye uwezo akataka kuoa au kuolewa na maskini wangekataa na kumwambia atafute mwenye uwezo kama yeye? Kuna mambo mengine hapa duniani yapo nje ya uwezo wa binadamu na hili inabidi walitambue.

    Na pia mzazi wa mchumba wako ndio mbunge si mchumba wako.Hili na wewe pia lazima ulitambue.Mkishaoana ni wewe na mchumba wako, hayo mammbo ya ubunge hayaingiliani kabisaa na ndoa.Na hata huyo mzazi sidhani kama ataendelea kuwa mbunge FOREVER. Hiyo wasahau kabisaaaa.

    Katika kipindi kama hiki ilibidi wamshukuru Mungu kuwa umepata mchumba na si kulalamika. Sasa nanza kuamini ndo mana wengine hunyimwa na Mwenyezi Mungu kwa sababu hawana shukrani na hawamwogopi Mwenyezi Mungu.Kitabu cha Samweli(2:1-8) pia kinasema mwenyezi Mungu ana uwezo wa kukupa na kukunyang'anya.Yaani binti nakushauri umwombe sana Mungu wako ili akuongoze katika kipindi hiki. Mungu ni mwema, yeye husikia sauti zetu na kujibu maombi yetu. I wish you all the best.

    ReplyDelete
  3. Dada usiwe na hofu unajua wazazi wako wanakupenda ndio maana wamekuambia hivo, mimi nakumbuka Dada yangu alitaka kuolewa na jamaa mmoja hivi Baba na mama walipinga sana, na akaachana nae akaolewa na mwingine ambaye wanaishi naye mpaka sasa tena kwa amani na upendo na wana watoto wa2. Dada yangu alishukuru ilipopita miaka kadhaa baada ya kugundua kwamba yule jamaa alikuwa ni muongo na alidangaya mambo mengi sana wazazi wanaona mbali ndugu yangu, ndoa za wazungu ni mbovu zaidi ya kiafrika kwa sababu wao hawazingatii mambo kama sisi tunayozingatia, japo ndoa nyingi siku hizi zinavunjika huwezi kufananisha hata kidogo na za wazungu wao ndoa zao huwa zinavunjika sana. Sasa cha kufanya kaa chini uongee na wazazi wako na uwaeleweshe na uwaeleze jinsi uhusiano wenu ulivoanza, na mpaka mlipofikia kama wakigoma we achana na huyo jamaa japo itakuuma, lakini ukiwa mbishi utaolewa nae na ukipata matatizo wazazi wako wanaweza kukususa mpaka unaweza kuchanganyikiwa. Nadhani wameshaona jinsi wasichana walioolewa kwenye familia za kitajiri wanavonyanyaswa ndio maana hawapendi na wewe uingie huko, ila cha msingi ni mawasiliano na uwaeleweshe, kama kweli unampenda tumia diplomasia uwashawishi wazazi lakini fanya hivi kama unajua huyo kijana kweli anakupenda maana na sisi wanaume tuna mambo sana haswa tukiwa na pesa. Angalia upendo jizo hela huwa zinayeyuka tena na viongozi wa sasa walivo wezi kama ulifata pesa baba mtu anaweza akafungwa kwa ufisadi akafilisika ukaikimbia nyumba. Fuata true love alwayz kama mnapendana washawishi wazazi wakigoma usilazimishe my sister.
    Ni mimi kaka yako Izoo wa hapa Dodoma, Mjengoni. Kila la kheri my Sister.

    ReplyDelete
  4. UNAHITAJI PESA NA UNAPENDA MWANAUME WAKUTOMBANA NAYE MWENYE UWEZO WA KUNYONYA KUMA NA KUCHEZA NA KINEMBE CHAKO ? NITAFUTE -0752238295=NITAKULIA POA SANA WEWE UTAPENDA WENYEWE KUTOMBANA NI AJIRA NZURI NJOOOO

    ReplyDelete