Katika somo la leo jamani nataka tujifunze kuacha ubinafsi ndani ya ndoa, maana siku hizi wanandoa wengi hulalamika wenza wao kuwa wabinafsi na maanisha nini:
Utakuta kwenye ndoa mtu ameoa halafu anaishi maisha kama yupo bachelor yani hajawahi kumtoa hata mkewe out hata bar ya jirani kumnunulia soda, yani mama yeye tena ndio kama kazi hana basi akae tu nyumbani alee watoto na nyumba baba akija akitaka mzigo ampe baasi ndio alichoolewa jamani huu si utumwa ama wanaume wa aina hii wanaogopa kusaidiwa wake zao kwahiyo wanawakalisha ndani tu wasionekane.
Utakuta mwanamke umeolewa na unafanya kazi hata siku moja hujawahi hata kumnunulia mumeo socks, au hata nguo ya ndani yani huyo baba asipojinunulia mwenyewe ndio anavaa zilezile tokea mlipokutana mpaka leo mna mtoto...mmmhh mwanamke hii ni aibu likitokea dharula mara suruali imemtoka si aibu kuona nguo ya ndani imechakaa? ama kavua viatu mbele ya watu socks mpaka imetoboka loooh..
Wame wengine kutwa barabarani kwenye starehe bila wake zao, tena wengine ndio wanakula starehe na magumegume ambayo ukimlinganisha na mkewe hamuingii hata kwa punje ya mchanga, mkewe yeye yupo nyumbani tu anahesabu mabati akimsubiri mumewe jamani haipendezi.
Ama wanawake ndio ushapata mashoga barabarani basi wewe kutwa na masgoga zako hata muda wa kumuwekea mumeo mkae muongee mjadili mambo yenu ya ndoa hamna, umekalia umbea tu wa mashoga inahusu..
Ubinafsi ni sumu kwenye ndoa ulipoamua kuoa ni kwamba wewe na mwenzio muwe mwili mmoja sasa wewe unataka mwili mmoja kwenye mechi tu ila wakati mwengine miiliii unayo sijui hamsini, rafiki yako, kaka yako, jirani yako, yule hawara yako, sijui boss wako mkeo au mumeo akuuu huna habari naye utatupwa kwenye dustbin...shaurilo
0 comments:
Post a Comment