Thursday, December 29, 2011

MTENDA AKITENDWA...

Habari zenu wote mnaotembelea hii blog, mimi ni mwanake niliyeolewa miaka sita iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu, kwakweli maisha ya ndoa yangu ukiniuliza sijui nitasema kama miaka yote hiyo niliifurahia maana kero ni nyingi mpaka natamani kutoka kwenye ndoa lakini navumilia tu sasa kwasababu ya watoto wangu na kwasababu nimepata wa kuniliwaza na kunipa nguvu ya kuendelea kuwa kwenye ndoa.

Mume wangu mimi yani ni malaya jamani sijapata kuona yani yeye akiona mwanamke anapita huku mboo yote inamsimama yani akili inasimama na kuwaza mechi tu, nimeshamsema sana na kumonya sana lakini naona hamna siku anayobadilika, ukiacha hivyo ni cha pombe ile mbaya muda wake mwingi kama hawi na hawara basi analewa mpaka saa kumi za usiku na akirudi ukimuuliza anatukana tena siku nyengine mpaka na kukupiga kwakweli miaka yote hiyo nimevumilia vituko vyake nikiamini kwamba iposiku atabadilika lakini sioni akibadilika mpaka leo.

Hapa katikati nikiwa nimetoka kwenda kupunga upepo kwenye hoteli moja hapa jijini nikiwa na marafiki zangu wa kike akaja kaka mmoja akaonyesha kunipenda akaniomba namba ya simu kwavile na mimi nilikuwa na machungu yangu basi nikampa tu for fun, kweli jamani yule kaka akaanza kunipigia simu kila siku mara tatu kwa siku kama dozi, na anavyoongea na mimi hata simu sitaki akate tukikutana ndio usisema mapenzi motomoto yani nikiwa naye nasahau kama nimeolewa mpaka amenipa ufunguo wa nyumbani kwake niwe free anytime akitoka kazini tunakutana pale napika na kufanya kazi kama kwangu tunakula raha zetu ananipa hela ya taz ama ananirudisha karibu na nyumbani mimi huyooooo.

Nina miezi naye miwili yani amenifanya nisahau matatizo yangu yote na ameniichanganya sana akili, kwasasa mume wangu hasikii nikimuuliza alipotoka huo usiku, sigombani naye yani naishi tu kulea wanangu, mpaka akaja kugundua kama nina mwanaume na kweli nikamkubalia kwakuwa nipo tayari kwa lolote ninachotaka tukae tutunze tu watoto lakini kwa mapenzi no way.

Sasa anasema atanifanyia vurugu na mpenzi wangu atamtafuta mpaka amjuwe amuonyeshe yeye ni nani kwakweli ananiudhi ile mbaya alipokuwa na mimi wakati namvumilia hakuniona wa maana leo nimepata wa kunituliza roho na kunipa amani anataka kunifanyia vurugu na ndio ananiona wa maana inahusu jamani?


Reactions:

2 comments:

 1. Kwa hili ndugu yangu hakuna mtu mwenye akili timamu atakaye kuunga mkono. Unajifanya umemkomoa mumeo lakini kumbuka na fuatilia kwenye vyombo vya habari wanawake wanaogundulika na waume zao kuwa wanatembea nje wamefanywa nini. Ungefanya siri ungeleweka lakini kuweka wazi? hiyo siyo busara kabisa.

  Ingekuwa umechoka hiyo ndoa basi ungeomba talaka, lakini kufanya uzinzi ndani ya ndoa eti unalipîza kisasi? hiyo ni mbaya sana na ni chukizo kwa Mungu. Jiandae kwa lolote baya kutoka kwa mumeo muda wowote. Hata huyo kijana wako usifikiri anakupenda bali anakutumia tu kumaliza shida zake kwani amekuona wewe ni bei rahisi kupatikana kwani kubadilishana namba za simu tu ndiyo ilikuwa njia yako, yaani sijakuelewa kabisa. Kumbuka njia ya kuelekea kwenye ukahaba au malaya ndiyo umeisha ianza hivyo. Nina imani huyo kijana hiyo ndiyo tabia yake kubadilishana wake za watu, nina uhakika akiisha kuchoka atakushiti kama vile hajawahi kukuona, nawe kwa kuwa umeisha zoea kutoka nje ya ndoa yako hautasita kutafuta mwanaume mwingine na wanaume wa namna hiyo wanaosubiria mizoga kama wewe wapo wengi, na huo ndio utakuwa utaratibu wa maisha yako, kuvuliwa chupi na kila mwanaume anaye kudanganya kukupenda.

  Kwa kweli kama unajipenda unatakiwa ujihurumie na kujisikitikia, umejidhalilisha na kuwa dhalilisha wanawake wenzio.

  Pole sana, ingekuwa bora uweke contact zako ili na sisi tukutafute ili tupate hiyo huduma ya bure!

  ReplyDelete
 2. Mimi ni mwanamume huyu mume wako akimjua huyo bwana ni shauri yako,hapo juu aliyetoa ushauri akatoa ushauri wa maana kwanini usichukue talaka uwe huru.kaongea ukweli kabisa,kazi iko kwako

  ReplyDelete