Sunday, January 1, 2012

NIMEKUKOMESHA HATA KAMA NYUMBA YAKO..

Dada Rose, za kwako na watu wote mnaotembelea hii blog yani kwakweli mwaka huu nimeuanza vibaya kweli kwa kupigana na mama mwenye nyumba yangu, sawa nyumba ni yake lakini ndio kuninyanyasa na familia yangu!!!!!

Kodi yangu iliisha 30 December nikatakiwa kulipa nyengine lakini kwa vile mambo hayajaenda vizuri nikamuomba mama mwenye nyumba anipe wiki moja yani mpaka tarehe tano january nitakuwa nimeshamlipa kodi yake, kwa maneno kibao ya kwamba sijui yeye asifurahie sikukuu kisa mimi sina kodi asile vizuri kwakuwa sina kodi ya kumpa akaongea maneno kibao kisha akaondoka zake.

tarehe 31 December mama mwenye nyumba akaja tena alikuja mida ya mchana nilikuwa jikoni napika akaniambia anataka aangalie nyumba ili ajuwe nini cha kubadilisha ili kuboresha nyumba yake, nikamruhusu basi akaangalia alivyofika jikoni mimi nilikuwa napika rosti la kuku na wali akanisifia chakula kinanukia vizuri akaendelea kuangalia nyumba akasema nakuja ngoja niangalie kwa nje kaenda mara karudi ndani na kufunua chungu cahangu jikoni na kumwagia mchanga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

sasa nilikuwa natenga meza kurudi niangalie mboga nakuta imejaa michanga na yupo yeye tu pale nikashtuka sana na kumuuliza kama amefanya hivyo akafyonyaa na kuniambia yani wewe na familia yako mjichane halafu kodi ya kunipa huna miye nile maharage na familia yangu.

Jamani hasira ilinipanda nilimkunja yule mama tulipelekeshana pale ndani, tulibondana watoto wangu wakaanza kupiga kelele majirani wakaja mpaka mjumbe basi yula mama akasema anataka niondoke nyumbani kwake akaambiwa inabidi anipe notice ya miezi mitatu amenunajee.

mada hii nimeitoa kufurahisha genge tu, na kuwaweka makini na hawa wenye nyumba zetu.

Reactions:

1 comments:

  1. Hehehehehe nimechekaje. Lesson Learned. Sidhani kama atarudia tena. Du ila we ni noma.

    ReplyDelete