Wednesday, August 10, 2011

MKE WANGU SIO MWAMINIFU....

mama mizizi,


ahsante kwa mada zako nzuri za kutuelimisha, mimi nina tatizo moja ambalo kwa sasa sijui la kufanya ningeomba wewe na wadau mnisaidie.


mke wangu nahisi sio mwaminifu kabisa, kwanza yeye ni mama wa nyumbani mimi ndio ninayefanya kazi kukidhi mahitaji ya nyumbani, katikati hapa mke wangu ameanza kubadilika sana sio tu kuwanza kujiweka vizuri bali hata siku nyengine nikimgusa nikitaka penzi huniambia amechoka na nikibaki kushangaa amechoka akifanya nini wakati yupo tu nyumbani.


siku moja nikiwa kazini rafiki yangu alinipigia simu na kuniambia alikuwa gesti na demu wake na kumuona mke wangu kwa mbali japo mke wangu hakumuona alikuwa amekaa bar ya gesti na mwanaume na baadae wakatokomea hakuona walipoelekea na kwamkao ule yule mwanaume hakuweza kuwa nduguye.


kwa kweli nilishtushwa sana na kupata jibu la kwanini mara nyingi nikimtaka kimapenzi hakubali na kuniambia amechoka na kazi za nyumbani na hata kama akinipa nikitaka mzunguko wapili ananinyima kumbe alikuwa anamtu wa kummaliza hamu pembeni.


tokea nimepewa habari hizi sijui hata nianzaje kummuuliza mke wangu kwani kwa ubishi aliokuwa nao najua hatakubali nikimuuliza kwakuwa sikumuona mimi nashindwa hata nimuanzaje maana kwakweli najisikia vibaya sana kila mara ninapomuona nina dukuduku..nahisi hata kumpiga


naombeni ushauriReactions:

2 comments:

  1. Duuuh! Inauma aiseee! Nahisi hata moyo umelipuka. Kaka usimuulize, jaribu kutengeneza mtegoDuuuh! Inauma aiseee! Nahisi hata moyo umelipuka. Kaka usimuulize, jaribu kutengeneza mtego

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka najua hili swala ni kwa jinsi gani linakuumiza haswa ukizingatia ni mke wako wa ndoa sasa mimi kitu nitakacho kushauri usiamini sana marafiki sisi binadamu tuna hulka za aina mbalimbali usimwamini sana mwanadamu mwenzako simtetei mkeo lakini nataka ufanye uchunguzi zaidi na uwe na evidence ya kutosha ukisha pata ushahidi wa kutosha mkalishe mkeo umwonye kwama ya kwanza sikuambii umwache la hasha maana kama mna watoto watapata shida umweleze madhara ya kutoka nje na kwanini akashaushika kuvunja uaminifu umweleze polepole kwa utaratibu usiwe mkali maaana na yeye atakuwa na tatizo lake lililomsababisha kutoka nje ya ndoa na akishakiri mwambie kwa vile umekuwa siomwaminifu katika ndoa mwende mkapime afya siku hizi magonjwa mengi akikubali mnaenda pima kama mkosalama unakuja kumpa masharti umweleze umeweka ulinzi kila mahali wa kumchunguza yeye kwa anayoyafanya ni hayo tu usiwe na hasira maana hasira hasara pole sana

    ReplyDelete