Wednesday, August 3, 2011

RAHA YA MAPENZI YA MBALI....


mapenzi ya mbali ni magumu sana, lakini mapenzi ya mbali pia ni mazuri na ndio yenye kudumu zaidi kama utajuwa jinsi ya kuyatunza vizuri.


tuchukulie mmeoana halafu mpo mbali mbali...


kwanza kabisa mnakuwa hamchokani kwasababu sio muda wote mpo pamoja mnaonana mara chache, sio kama mkiwa pamoja ukienda chumbani yupo, sebleni yupo mara jikoni atakuja, lakini mkiwa mbali mbali mnapoonana mnakuwa manatamaniana sana na kutaka tu kugandana kama smaku...


mkiwa mbalimbali hamchoki kuongea pamoja, story zinakuwa nyingi mkiwa kama mnapigiana simu ama mnachat yani inaleta raha maana kila mmoja anakuwa na kitu kipya cha kumwambia mweni wake, tofauti na mnapo kuwa pamoja mnakuwa mmeshaongea kila kitu mpaka vimeisha mnaanza kuongea umbea mwisho....


uzuri mwengine ya mapenzi ya mbali jamani kila mara unamuona mwenzako mpya, yani kila mnapoonana utagundua huyu leo hivi na yule kafanya vile yani unakuwa na shauku lakumchunguza mpenzio kwa matamanio, tofauti na kuwa wote mda mwingi mwisho mnazoeaaaaanaaa mpaka unaweza kumchora mwenzi wako ukiwa usingizini.


kuachana kwa wapenzi wa mbali huwa haina idadi kubwa kama wanaokaa pamoja kwasababu kila mtu alipo anaficha makucha yake maana mnapoonana ni mduda tu na muda huo kila mwenza hufanya yaliyo mema kwa mwenza wake maana kila mtu ana hamu na mwenzake tofauti na mkikaa pamoja makucha yote yanatoka sasa mwisho mpaka kuchokana na kuachana, maana visa juu ya visa...

Reactions:

0 comments:

Post a Comment