JAMANI WANAWAKE HASWA NATAKA NIONGEE NA SINGLE MOTHERS LEO, AMA WEWE MWANAMKE ULIYEOLEWA UKAACHIKA NA UKABAKI NA WATOTO KUNA HII TABIA MOJA NIMEIONA KWA WAMAMA WENGI TU WAAINA HII
WANAWAKE UNAWATOTO AMA MTOTO AMBAYE SIO MDOGO AU HATA KAMA NI MDOGO NA UMEACHANA NA BABA YAKE JAMANI NDIO NAJUA UTAPATA MWANAUME MWENGINE LAKINI UNAJUA NI NAMNA GANI ITAMUAFFECT MTOTO WAKO??? KWA UZURI NA UBAYA AMA HUWA TUNAJIWAZIA MATAMANIO YETU TU NA KUSAHAU HAKI ZA WATOTO WETU
SAWA BASI UMEPATA BWANA ANAKUJA NYUMBANI KWAKO?? NA ANAVYOKUJA UNAKAA NAYE VIPI MBELE YA MTOTO WAKO? ANALALA NYUMBANI KWAKO ?? NA AKILALA MWANAO ANAKUA AMELALA WAPI??AU WEWE HUWA UNAENDA KULALA KWAKE NA UKIENDA KULALA KWAKE MWANAO UNAKUA UMEMUACHA WAPI?? AU UMEMUAGAJE??
KUNA DADA MMOJA HIVI HUKU USWAHILINI KWETU YEYE ALIZALISHWA TU NA MWANAUME MMOJA MTOTO WA KIUME NA KUWA TU ANAMUHUDUMIA HAJAMUOA BADO
KWAKWELI HUYU BABA ANAJITAHIDI SANA ANAMMLIPIA NYUMBA, ANAMLISHA ANAMVISHA YEYE NA HUYO MWANAE
LAKINI JAMANI SISI WANAWAKE SIJUI MWALIMU WETU NANI, YANI HUWA TUNATAMAA ZA AJABU SANA HUYO ULIYENAYE SIJUI HAKUTOSHI AU KUENDEKEZA UMALAYA WAKATI UNAPEWA KILA KITU
YULE DADA KWAKUA BABA MTOTO WAKE HAKAI NAYE AKAANZA KUCHEPUKA, AKAPATA MWANAUME HUKO WA KUCHEPUKA NAYE HUYO MWANAUME ANAKAA MTAA KAMA WA NNE HIVI, MAPENZI TENA YAKAWA MOTOMOTO
KWAKUA HUYU DADA HAKUWA NA KAZI ALIISHI TU NA MWANAE NA KUHUDUMIWA KILA KITU HAKUONA UMUHIMU WA KUWEKA MSICHANA WA KAZI AKWA TU ANALEA MWENYEWE
NA TULIVYOWAJINGA ETI BASI BORA KAMA UNAENDA KUCHEPUKA BEBA MWANAO MLISHE VIZURI MBEMBELEZE UKIONA ANAANZA KUSINZIA MBEBE ONDOKA NAYE MPAKA AKIFIKA HUKO KESHALALA SIKU NYINGI WEWE UANZE SASA KUNENG'ENEKA VIZURI NA HUYO HAWARA YAKO
LAKINI KWA UJINGA WA HUYU DADA ALIKUA AKIENDA KUTUMIKA ANAMUACHA MWANAE WA MWAKA NDANI ANAMFUNGIA NA MLANGO ANAONDOKA, MTOTO AKIAMKA ANALIA WEEEE MPAKA ANYAMAZA ANALALA TENA AKIAMKA ANALIA WEEE ANANYAMAZA NA KULALA MPAKA MAMA YAKE ARUDI
MAJIRANI SASA NDIO WAKAANZA KUSHANGAA HUYU MTOTO KWANINI KUNA WAKATI ANALIA SANA NA WAKATI YUPO TU KAWAIDA MAANA KWA WIKI ILIKUA AINATOKEA HIVYO MARA TATU WAKAANZA KUCHUNGUZA
SIUNAJUA LAZIMA UTAKUA TU NA RAFIKI MMOJA HAPO JIRANI UNAMUELEZEA MAMBO YAKO, NDIO HIVYO SHOGA AKAWA NAYE MMOJA NDIO AKATOA SIRI KWELI WATU KUCHUNGUZA WAKAUPATA UKWELI KWA KUMKOMESHA WAKAAMUA KUTOKUMWAMBIA BALI SIKU BABA MTOTO ATAKAPOKUJA TU WAMUELEZE
MUNGU SIO MJOMBA WA MTU SIKUKUU YA EID BABA MTU KAJA NAMAZAGAZAGA KIBAO KUILETEA FAMILIA YAKE, NA KWELI ALIMKUTA MKEWE NA MTOTO BAADA YA SAA KUMI KUMBE KULE MAJIRANI WAKAJIPANGA WATATU KUJA KUMUELEZA YULE BABA
MARA WAKAINGIA KARIBUNI SHOGA AKAANZA KUJICHEKESHA NA KUSHANGAA KWANI VIPI OOHH TUMEKUJA TU KULA SIKUKUU YETU, WAKAKARIBISHWA NA KUINGIA NDANI NA KUANZA KUMWAMBIA YULE BABA KILA KITU
JAMANI YULE BABA ALICHANGANYIKIWA KUMUULIZA YULE MAMA AKAKUBALI KWAMBA NI KWELI HUWA ANATOKA NA KUMUACHA MTOTO AKAULIZWA HUWA UNAENDA WAPI HAPO SASA BABA KAPANIC NAKWAMBIA ANAONGEA KWA SAUTI MPAKA NYUMBA YA TATU WAMBEA TUNASIKIA NA KUANZA KUSOGEA KARIBU
MWANAMKE HASEMI ANAENDA WAPI JAMANI YULE BABA ALIMPIGA YANI ALIMPIGA YULE MAMA HATARI, AKAMCHUKUA MWANAE NA KUONDOKA
AKAMUACHA YULE MAMA HUKU ANALIA NA KUMLILIA MWANAE, MUDA SIO MREFU YULE DADA NAYE AKAONDOKA SIJUI SASA KAENDA WAPI SIJAMUONA TENA MMBEA MIYE NIKAONDOKA ZANGU KUFANYA YANGU
HUO NDIO MKASA WA KUENDEKEZA DYUDYU WAKATI UNAJUA UNAISHI KWA MSAADA, NA HUNA HAYA UNAMTOTO UNAENDEKEZA MWANAUME KULIKO MWANAO..MFYUUUUUU
****END*****
0 comments:
Post a Comment