Tuesday, January 13, 2015

hahahaha wanawake jamani tupunguze umbea, haswa kuchokonoa ndoa za watu haipendezi...

SHOGA CHOKOCHOKO ZA UMBEA KUHARIBU NDOA ZA WATU MWANAMKE HAIPENDEZI

UNATAKA NINI KWANZA WAGOMBANE, WAACHANE AMA WEWE NDIO UONEKANE SHOGA NA RAFIKI MZURI SANA MWAMINIFU KWANI WEWE YAKO HUNA YAA AJABU MBONA UNAYAFICHA HUYATOI KILA MTU AKAYAONA UNASHADADIA YA MWENZIO TU NDIO MAANA SIKU HIZI WANAWAKE KWA WANAUME KILA KUKICHA WANASUTWA

JANA NIMERUDI NYUMBANI NAFIKA TU NAPEWA STORY NA UMBEA WA MTAA WA TATU

SHOGA MIYE TENA ENHEEE KUNA NINI, NIKAANZA KUAMBIWA SIUNAMJUA MAMA FULANI NDIO KAFANYAJE 

HUYU MAMA JAMANI NI MAMA MTU MZIMA YANI MWANAE WA KWANZA ANAMIAKA 26 NI KIJANA MKUBWA AMBAYE ANAFANYA BIASHARA ZAKE ZA HAPA NA PALE

HUYU MAMA MWENZANGU AMEPANGA NYUMBA MOJA NA WATU WENGINE TOFAUTI WALIOO OOANA NA WENGINE MASINGLE BADO

SASA SHOGA HUYU MAMA AKATOKEA KUMPENDA MUME WA DADA FULANI, SEMA HAJAMWAMBIA SIUNAJUA TENA WANAWAKE WAKIPENDA ANAJISHEUA NA KUJISHEBEDUA AKIMUONA MWANAUME KAMA KAMEZA MNYOO UNAMTEKENYA

BASI SHOGA NAYE NDIO HIVYO HIVYO ILA WATU WAKAWA WANAPOTEZEA, WANAMUONA HUYU MAMA MTU MZIMA LABDA UMRI UNAMSUMBUA KUJIBEBISHA KWA MWANAUME MDOGO TENA MUME WA WATU

HUYU KAKA YEYE NI DEREVA WA MALORRY HAYA YANAYOENDA CONGO, KWAHIYO ANAWEZA KUSAFIRI WIKI TATU NA KUENDELEA NA AKIRUDI KAMA MNAVYOJUA WAME ZETU WAKISAFIRI LABDA KAMA WEYE MUMEO HAJITAMBUI ATAKULETEA MAZAGAZAGA KIBAO, SIJUI MKAA, NYANYA, VITUNGUU BASI NA MKEWE AKAWA ANALETEWA SANA NA MATENGE YA CONGO BASI WEEE

YULE MAMA NDIO ROHO IKAWA INAMTOKA, AKAZIDI KUMTAMANI YULE MWANAUME, AKAJICHEKESHA NA KUJIZOELESHA NA ILE FAMILIA MPAKA AKAPATA NUMBER YA SIMU YA YULE KAKA

WAPANGAJI WENGINE WAKAWA WANASHANGAA MBONA HUYU MAMA ANAUSHOGA SANA SIKU HIZI NA HUYU DADA ILA WAKAWA WANAKAA TU KIMYA, BASI MWANAUME AKIRUDI SHOGA TENA ANAMPUNGUZIA YULE MAMA VITU SI SHOGA YAKE TENA USHOGA KAZI JAMANI MJINI HAPA USIOMBE UWE NAYE..

MAISHA YAKAENDELEA HIVYOOO, NA YULE MAMA SASA NDIO KASHAMZOEA KABISA YULE BABA AKAANZA MTINDI YULE BABA AKIWEPO YULE MAMA MTU MZIMA ANAJIVALISHA NGUO ZA AJABU

ANAWEZA KUVAA DERA LA KANTANGAZE BILA HATA GAGULO WALA TIGHT, MARA AVAE VIMINI NA VIPENSI ANAINGIA NDANI MWA YULE SHOGA YAKE

SASA SIJUI HAPO YULE BABA NAYE AKAANZA KUMTAMANI SIUNAJUA WANAUME WANAVYOTEGEKA KWA URAHISI KAMA LABDA HAPO NDIPO WALIPOANZIA MAHUSIANI YA CHINICHINI SIJUI

BASI BWANA YULE MAMA AKAANZA MCHEZO YULE BABA AKISAFIRI MAMA ANAMPA YOTE YANAYOENDELEA KWAKE MKEO LEO KATOKA KAENDA HUKU, MARA MKEO LEO HIVI MARA VILE

SASA YULE DADA SI ALIKUA ANAMUAMINI HUYU MAMA KWAMBA NI SHOGA YAKE BASI ANAMPA STORY ZOTE ZA USHOGA HATA KAMA AMETONGOZWA AMA ANAENDA KUMNYWEA MTU BEER YULE MAMA YOTE ANAYAFIKISHA KWA MUMEWE

SHOGA AKAWA ANASHANGA MUMEWE AKIMPIGIA SIMU ANAMCHAMBA NA KUMTUKANA HATARI, MPAKA BWANA KARUDI WAKAGOMBANA SANA TENA SANA IKAWA MPAKA MWANAMKE AKAONDOKA KWENDA KWAO

AKIWA KWAO AKIJARIBU KUTAFAKARI HAPATI JIBU ILA ANAJUA NI MTU MMOJA TU ALIKUA ANAMUHADITHIA MAMBO YAKE, YULE MAMA BASI AKAENDA AKAMCHAMBA SANA, KWAKUA ALIONDOKA NA UFUNGUO WA NYUMBANI KWAKE AKAMWAMBIA WEWE SHIDA SI MUME WANGU SASA NAKUACHIA

SHOGA KAJA NA GARI KAJIPANGA KABISA KAENDA NDANI KAKOMBA KILA KITU, MAANA MUMEWE ALIONDOKA SAFARI BILA KUMUAGA SIWAPO KWENYE UGOMVI YANI KAKOMBA KILA KITU KAACHA NYUMBA NYEUPE KAMA WALIVYOIPANGISHA

MWANAUME YUPO SAFARI AKAPEWA TAARIFA MKEO KAJA KAKOMBA KILA KITU, BWANA TENA KUCHANGANYIKIWA ILA ATAFANYAJE NA YUPO MBALI AKAFANYA KAZI ZAKE HUKO MPAKA KUISHA KURUDI NYUMBANI YULE MAMA KWA UMBEA TENA BWANA KAJA ANAAZA KUMUHADITHIA NA KUJIFANYA ANAMPA COMPANY KWAKUA BWANA KITU HANA

YULE MAMA MPAKA AKAMSHAWISHI YULE BABA KWENDA POLISI KUSHTAKI MKEWE KAMUIBIA..KUFIKA POLISI WAKAMWAMBIA HAKUNA KESI KAMA HIYO MKEO ATAKUIBIAJE WEWE NENDA KAMTAFUTE MKEO MMALIZANE

BASI BAADA YA KUKAA KWA UPWEKE KAMA WIKI MBILI YULE BABA NDIO KWENDA KUMTAFUTA MKEWE NA KUMUOMBA MSAMAHA NA KUMUOMBA ARUDI, JAPO KWA UGUMU NA TABU YULE MAMA AKAKUBALI AKARUDI KWA MUMEWE

SASA AIBU KABAKI NAYO MTU MZIMA KAUMBUKA KUWAGOMBANISHA KISA UNAMTAKA BWANA BWANA NAYE KAENDA KUMRUDISHA MKEWE, SASA HIVI MPAKA NJIA KABADILISHA YA KUPITA MAANA AIBU KILA AKIPITA WATU WANAMUWEKA MIDOMONI.

TUJIFUNZE MAPENZI HAYAINGILIWI JAMANI

***END****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment