Tuesday, September 9, 2014

Tuache kukariri ishi maisha yako kama wewe..

  JAMANI HIZI TABIA ZA KUIGANA HIZI NAOMBA LEO ZIFIKE MWISHO, YANI NAONGEA KWA MSISITIZO ZIFIKE MWISHO, ZIKOME KABISA

WANAWAKE WENGI WANAPATA SANA SHIDA KWENYE NDOA ZAO NA MAHUSIANO YAO LAKINI WAMEKAA HAWAONGEI HAWATAFUTI MSAADA KWASABABU TU YA KUTAKA KUONEKANA ANANDOA

KISA WAKATI UNAOLEWA ULIAMBIWA UVUMILIE, BASI WEWE UNAVUMILIA HATA VISIVYOVUMILIKA, KISA ROSEMARY MIZIZI ANAKUAMBIA MWANAMKE NDOA BASI NA WEWE UNATAKA KUGANDA KWENYE NDOA AMBAYO UNAJUA HAIENDI HAINA AMANI, MMEJITAHIDI KUSULUHISHA LAKINI MWANAUME HAELEWI WALA HASIKII TENA UNAPIGWA NA KUFUKUZWA JAMANI WANAWAKE JAMANI

WAPENDWA NDOA NI BARAKA, NDOA NI AGANO LA MUNGU NDOA UNATAKIWA KUIFURAHIA NDOA NI HESHIMA NDIO NDOA UNATAKIWA UNAWILI UKIENDA KWA MUMEO WATU WATAMANI NDOA SIO UKUMBI WA VITA BARAKA ZINAONDOKA

UNAJUA KABISA MUMEO AMEKUUDHI NA UMEUMIA SANA KWANINI UNAJIVUNGA HUONGEI NAYE UKWELI UNAJICHEKESHA KWAKE KAMA KILA KITU KIPO SAWA?????? KISA UNAOGOPA TU KUONEKANA HUNA ADABU KINAKUKULA WEWE MOYONI UNAUMIA, UNAJIKONDESHA KISA TU UMEAMBIWA MKE ANATAKIWA KUVUMILIA??

HAPANA MIMI MWENYEWE SIISHI HIVYO MUME WANGU AKINIBOA AKIRUDI NYUMBANI LAZIMA NIMWAMBIE HATA KAMA TUTAGOMBANA LAKINI NIMELITOA DUKUDUKU BAADA YA HAPO LIMEISHA HILO

WANASEMA OOHH MUME HANUNIWI BIBI MANENO YA TAARABU WAACHIE WAIMBA TAARABU, MUMEO AKIKUUDHI BIBI KAMA UNAJISIKIA KUNUNA NUNA, KUNUNA KWAKO NDIO KUTAMFANYA AJUE KUNATATIZO MIYE MWENYEWE NAMNUNIA SANA ANAJUA KUNATATIZO ATANIBEBISHA MPAKA TUNAONGEA YANAISHA

UKIPIGWA JAMANI SEMA, UNAPIGWA WANAUME WENGI SANA WANAMKONO WA KUPIGWA HATA MIMI NILISHAPIGWA KWENYE NDOA YANGU TENA SIO MARA MOJA, NILISHAPIGWA TENA MPAKA NIKALAZWA HOSPITAL SIKU TATU NA KOSA SIO LANGU NI LAKE LAKINI BAADA YA PALE SASA NIKAMWAMBIA HILI UKINIPIGA TENA SIKU NYENGINE NITAONDOKA SINTOKAA KURUDI NA KUMUHAKIKISHIA NILIKUA SERIOUS NIKAWAAMBIA NA WAZAZI WANGU KWAMBA IKITOKEA NIMEPIGWA NDOA IMEISHIA HAPO!!!!!! BAADA YA KUFANYA VILE NASHUKURU WAZAZI WANGU WAKAMWAMBIA KABISA BWANA HUYO HIVI NA HIVI MUME WANGU AKAAPA KUTONIGUSA TENA

WANAUME NI WAPIGAJI YANI WAO WANATAKA KILA KITU WANACHOTAKA WAO NDIO KIFANYIKE, NDOA SIO UKUMBI WA JESHI PALE KWAMBA KIONGOZI NI YEYE TU WEWE UFWATE HAPANA..SPEAK OUT MAMA

NUNA, GOMBANA, KASIRIKA, SUSA, FANYA VYOTE VITAKAVYOKUFANYA UPATE JIBU KUTOKA KWAKE UKIONA HUYU MWANAUME KASHINDIKANA NA HATAKI KABISA KUBADILIKA KAGOMA KABISA BEBA KILICHOCHAKO KAA PEMBENI

NA KUKAA PEMBENI SIO KUMUACHA HAPANA TOKA KWENYE NYUMBA HIO RUDI LABDA NYUMBANI HUKU UKIENDELEA KUSALI MUNGU AMBADILISHE MUMEO, HUKU WEWE UNAPATA HEALING YA KUKOMAA KUA MKE MWEMA

NDIO MAANA KILA SIKU NAWAAMBIA WANAWAKE ITS NOT BAD TO TAKE A BREAK KWENYE NDOA, ITS OK KURUDI NYUMBANI HATA WIKI MBILI UKIONA KWAKO MAMBO HAYAENDI JAMANI TUTAULIWA HIVHIVI TUKITAKA KUVUMILIA VISIVYOVUMILIKA TUMESHAYAONA KWA MWENZETU ALIYETUTANGULIA

LAZIMA KAMA MKE UWEZE KUSIMAMA IMARA UJITETEE, UKIPONA WEWE NA WANAO WATAPONA, WANAUME HAWA UKIFA ANAOA MKE MWENGINE NDANI YA MIEZI MITATU HANA HABARI WALA HAJALI

WATOTO WAKO NDIO WATAPATA TABU, USITEGEMEE MAMA WA KAMBO ATAKUA NA UCHUNGU NA WATOTO WAKO KAMA WEWE, NDIO MWANZO WA KUFUKUZWA KWAO NA KUWA WATOTO WA MITAANI

PIGANIA NDOA YAKO LAKINI PIA JIPIGANIE WEWE MWENYEWE, PIGANIA UHAI WAKO NA FURAHA KATIKA DUNIA HII, USIKANDAMIZWE KISA WEWE UMEOLEWA, USINYAMAZISHWE KWA KUTISHIWA UTAPIGWA TENA NA MUMEO, WALA USIOGOPE KISA UTAFUKUZWA, KWANI ALIKUCHUMA KWENYE MTI HUYO SI ALIKUKUTA KWENU KWANI KWENU HULI HUVAI HAULALI..ALAAAAA

SASA WEWE OGOPA AIBU UPEWE UKILEMA, AMA UFE KWA PRESHA NA UGONJWA WA MOYO

***END***

Reactions:

0 comments:

Post a Comment