Monday, August 25, 2014

Tumeongelea yote, gubu la mawifi, mashemeji, wake wenzetu ila hatujaongelea gubu la mama wakwe....

JAMANI KWENYE KITCHEN PARTY, SENDOFF NA NDOA TUNAHASWA KUWAPENDA NA KUWAHESHIMU WAKWE ZETU, TENA KUNA ULE MSEMO HUWA WANASEMA UKAWE BALOZI MZURI WA FAMILIA YAKO KWA MUMEO..

LAKINI JAMANI WAKATI MWENGINE NI NGUMU HII KITU, BORA HATA UKUTANE NA MAMA MKWE MYE HESHIMA NA ADABU NA MWENYE KUELEWA UPENDO WA UKWELI KULIKO UMKUTE MAMA MKWE AMBAYE ANA GUBU

BILA KUWAKOSEA HESHIMA JAMANI KUNA MAMA WAKWE WENGINE HAPANA AISEE, HATA UMFANYIE LIPI YEYE KWAKE HAONI LA MAANA, WALA HALITAMFANYA ABADILISHE AKILI YAKE AKUPENDE KAMA MWANAE AMA TU KUKUTHAMINI

BORA HATA SISI TULIOOLEWA MAMA MKWE ANAWEZA KUWA NA GUBU KWA MWANAE AKIONA UNAVYOMNYANYASA MWANAE LAKINI MAMA WAKWE UPANDE WA MUME WALE HAWANA CHA KUNYANYASWA WALA KUPENDWA WAO NI GUBU TU

KUNA DADA MMOJA YEYE AMEOLEWA, NA NDOA YAKE INAMIAKA KAMA NANE HIVI, HUYU DADA KWA MUMEWE WAMEZALIWA WANAUME WA NNE NA WALIOOA NI WATATU TU BADO MMOJA

KATIKA FAMILIA HII TOKEA SIKU YA KWANZA ANAOLEWA HUYU DADA HAJAWAHI KUPENDWA KWA DHATI NA MAMA MKWE WAKE LAKINI ANASHANGAA MAMA MKWE JINSI ANAVYOWAPENDA WALE WENGINE WALIOOLEWA NA MASHEMEJI ZAKE

WAKIENDA KUMUONA MAMA MKWE YANI WAKATI WANAONDOKA WANAFUNGASHIWA HATARI KAMA MNAVYOJUA WATU WENYE MSHAMBA BASI KAMA NI MIHOGO, MATUNDA MBOGA NDIO USISEME KILA MTU KWENYE SALFET YAKE

AKIENDA HUYU DADA YEYE ANAAMBULI KUSONYWA NA KUPEWA MANENO ALIYOAMBIWA ANAMSEMA MAMA MKWE NA WANAE, KITU AMBACHO SIO CHA UKWELI BADI DADA WA WATU ANABAKI KULIA NA KUUMIA SANA IKAFIKA KIPINDI AKAACHA KABISA KWENDA KUMSALIMIA MAMA MKWE WAKE

BASI MAISHA YAKAENDELEA HIVYO AKAMUELEZA NA MUME WAKE KAMA MNAVYOJUA WATOTO WA KIUME HUWA HAWAWEZI KUONGEA NA MAMA YAO ISHU KAMA HIZO NA NDIO HIVYOHIVYO ILIKUA KWA MUMEWE ALIKAA KIMYA NA KUOMBA TU MKEWE AMVUMILIE MAMA YAKE

BASI MAISHA YAKASONGA HUYU DADA AKABEBA MIMBA, WAKATI WA UJAUZITO MAMA MKWE ALIMPA TABU SANA KWA MANENO YA KASHFA NA DHARAU, KUNA KIPINDI HUYU DADA ALIKUA HANA MSICHANA WA KAZI AKAOMBA NDUGU WA KIKE WA MUMEWE AJE KUKAA NAO NYUMBANI ILI AMSAIDIE BASI MUMEWE AKAMLETA

KUJA PALE NYUMBANI SHOGA NAYE AKAANZA TU KUJIBWETEKA KWAKUA NI KWA NDUGU YAKE, YULE DADA AKAWA ANAMVUMILIA TU SIKU AKAMPANGIA KAZI KWAMBA NATAKA USAFISHE CHOONI, HEEEEEE IKAWA UGOMVI SI AKASUSA NA KWENDA KUSEMA KWAO YANI MKE WA KAKA KANIONA MIMI NDIO WA KUSAFISHA CHOO, MAMA TENA AKAJA JUU NA YULE MTOTO HAKURUDI TENA KWA WIFI YAKE

 VISA KILA KUKICHA HAVIISHI NA YULE MAMA MPAKA AKAJA AKAJIFUNGUA, YULE MAMA HAKWENDA KUMUONA MTOTO MPAKA MTOTO AMEANZA KUKUA NDIO AKAENDA, MPAKA SASA KABEBA MIMBA YA PILI MIAKA MITATU BAADAE BAADA YA KUZAA WA KWANZA LAKINI HAKUNA AMANI NDANI NA MAMA MKWE WAKE

SASA NIAMBIENI MAMA MKWE KAMA HUYU UTAMVUMILIAJE?? NA MBAYA ZAIDI MAMA MKWE NI MASHOGA NA WAKE WA MASHEMEJI NA HAO WAKE ZA MASHEMEJI HAWAPATANI NA HUYU DADA WANAMSEMA ANAJIONA NI MSOMI NA WANAHELA..KISA WAO TU HAWAJASOMA

 JAMANI NI NGUMU SANA, UKIKAA KIMYA UTAAMBIWA UNADHARAU, UKIONGEA ANAKUNYALI,,MMHHH HAPANA AISEE

***END****


Reactions:

0 comments:

Post a Comment