Tuesday, July 15, 2014

Ni sawa kusema HAPANA kwenye ndoa na sio kulia muda wote....

KATIKA MAISHA YETU YA NDOA, MKE NDIYE ANAYEBEBA JUKUMU KUBWA SANA KATIKA KUINGOZA NDOA NA FAMILIA KWA UJUMLA

MKE YEYE NDIO HUWA ANAUMIA SANA KATIKA KILA IDARA AKIWA MKE ANAUMIA, AKIWA MAMA ANAUMIA...MAMBO MENGI SANA YANAMUUMIZA KWA UCHUNGU WA NDANI SANA MKE NA MARA NYINGI KUMFANYA ALIE SANA KWA UCHUNGU NA MARANYINGINE HATA KUKONDA SANA KWASABABU YA HUO MZIGO

UTASA NI HALI YA KUKOSA MTOTO, NADHANI MNAJUA PALE UNAPOTAFUTA MTOTO HALAFU UNAKOSA, KILA MARA MIMBA HAIJAINGIA UNAJUA ULE UCHUNGU UNAOUPATA, ILE AIBU UNAYOIPATA KUTOKA KWA NDUGU NA JAMAA, YALE MANENO MACHUNGU MUME ANAYOONGEA MBELE YAKO AKISEMA JINSI ANAVYOHITAJI MTOTO YANI LAWAMA ZOTE ZINAKUANGUKIA WEWE MKE..

NITATUMIA UTASA KAMA TATIZO KATIKA NDOA, JE WEWE KAMA MKE UTASA WAKO WA NDOA YAKO NINI NINI

JE NI MUME WAKO MLEVI, JE NI MUME HAKUJALI, JE NI WATOTO WATUKUTU, JE NI MUME MALAYA, JE NI MUME ASIYEPENDA UWEPO WAKO KATIKA NDOA, JE NI KUPATA WATOTO...KILA NDOA INA UTASA WAKE

KWANINI KAMA MKE UNAOGOPA KUONGELEA UTASA WAKO KWA WAZI, KWANINI UNAUGUMIA UTASA WAKO NDANI KWA NDANI, KWANINI UNAONA KULIA NDIO SULUHISHO, KWANINI ULIE NA KUUWAZIA MPAKA UNAUMWA NA KUPATA MATATIZO YA MOYO, KWANINI UTASA UKUTESE WAKATI UNAWEZA KUFUNGUA MDOMO

MUME ANAPOKUA MALAYA KWANINI HUONGEI NAE JINSI ANAVYOKUUMIZA, KWANINI HUMUULIZI, KWANINI UNALIA TU NA KUOMBA TU MUNGU, KWANINI HUTAKI KUJUA SABABU INAYOMFANYA MUME AWE MALAYA KWANINI UNAENDELEA KUKAA KIMYA NA KULIA MWENYEWE CHUMBANI

KAMA MUME NI MLEVI NA AKIRUDI UGOMVI KIDOGO ANAKUPIGA KWANINI HUUVUNJI UTASA NA KUONGEA KWANINI AKIWA HAJALEWA UMWAMBII AKIKUPIGA UNAUMIA, HUPENDI KUPIGWA KWANINI HATA AKIWA HAJALEWA UNAKAA KIMYA

KAMA UTASA WAKO NI MUME KUTOIJALI FAMILIA KIFEDHA NA KILA KITU UNAFANYA MWENYEWE, UNAKOSA HATA AKIBA YA KUWEKA BANK, UNAKOSA HATA KUVAA VIZURI UNAKOSA HATA KUSUKA NYWELE UKAPENDEZA UNAKOSA HATA KUTOA FUNGU LA KUMI KISA MAJUKUMU YAMEKUBANA KWANINI HUONGEI KWANINI MKE UNAKAA KIMYA UKIJIDANGANYA UNAVUMILIA KWENYE SHIDA NA RAHA

KAMA UTASA WAKO NI MUME AKUTHAMINI, HAKUJALI HATAKI HATA KUTEMBEA NA WEWE AMA KWENDA NA WEWE SEHEMU, UNATUMIKIA NDOA YAKO KAMA SINGLE LADY KWANINI HUONGEI KWAMBA UNATAKA NA WEWE WATU WAKUONE UKIWA NA MUMEO KWANINI UNAKUBALI NA KUENJOY KUTOKA OUTINGS ZINAZOHITAJI UWEPO WENU WOTE PEKE YAKO..

UNAHITAJI KUSEMA HAPANA, UNAHITAJI KUJITETEA, UNAHITAJI KUTETEA FEELINGS ZAKO, UNAHITAJI KUJITHAMINI UNAHITAJI UJIWEKE WEWE KWANZA NDIO MUME WAKO ILI UWEZE KULEA VYEMA FAMILIA YAKO

NI SAWA KUMWAMBIA MUMEO ASIPOKUTENDEA HAKI, HATA KAMA AKIWA MKALI, HATA KAMA ASIPOKUJIBU NA AKAONDOKA UNATAKIWA KUSIMAMIA HAKI ZAKO KAMA MWANAMKE NA MKE

NI SAWA KUMSHAURI MUMEO APUNGUZE ULEVI AMBAO UNASABABISHA MADHARA NYUMBANI AMA KWA AFYA YAKO NI SAWA KUMWAMBIA MUMEO HAPANA MUME WANGU JARIBU JAPO KUPUNGUZA IDADI YA BEER KIDOGO

TUJITAHIDI KUSEMA HAPANA NA SIO KILA KITU SAWA WAKATI UNAJUA KABISA TATIZO HALITATUKI KWAKUA TU UNAOGOPA KUACHWA, AMA KUPIGWA, AMA KUONEKANA HUNA ADABU

 HAPANA PIA NI JUBU LA KUOKOA NDOA YAKO

****END****

Reactions:

1 comments: