Thursday, July 17, 2014

UTOAJI kwa mchumba wako na kwa mume wako...

JAMANI JAMANI JAMANI HASWA NYIE AMBAO HAMJAOLEWA NDIO NATAKA NIANZE NA NYIE MAANA WENGINE WENU MNAVIHEREHERE KUINVEST KWA MWANAUME UKIDHANI UKIFANYA HIVYO ATAKUONA WEWE NDIO WIFE MATERIAL WA KUOA KISA AKUONE UNAJIMUDU KWENYE SHIDA NA RAHA, BILA KUJUA KAMA MWANAUME ANATAKA AKUOE WEWE AMA ANAPITA MATOKEO YAKE UNABAKI NA MASIKITIKO NA AIBU

UTAKUTA MWANAMKE KAPATA BOYFRIEND LABDA ANAKAZI YAKE NA KAAMUA KUNUNUA KIWANJA NA KUJENGA SHOGA WEWE TENA UNAMSAIDIA KUJENGA..UNADHANI MWANAUME ATAKATAA MSAADA MKUBWA KAMA HUO TENA MAPENZI ATAZIDISHA MARA MIA NA WEWE KWAKUPENDA SIFA BORA KWENYE ACCOUNT UBAKI HUNA KITU LAKINI YOTE UKAJENGE NA WEWE UONEKANE UNAJENGA MJINI HAPA...INAHUSU

UNAJITAPA KABISA KWA MASHOGA ZAKO MIMI NA FRANK TUNAJENGA KIMARA, KISA TU ANAKUKALIA NYONGA MWENYEWE UNAJIONA KAMA MUMEO, MWANAUME MWENYEWE AKIKUITA LA MAANA UNAITWA BABY HATA SIKU MOJA HUJAWAHI MSIKIA AKIKUITA MKE WANGU HATA KWA KUZUGA NA WEWE UMEKAA UNAJIPA TU MOYO ATANIOA

JAMANI KWELI KABISA KUNA WAKATI MWENGINE UNAJUA KABISA HAPA BOYFRIEND WANGU KABANWA, YANI UNAMJUA KABISA HANA KITU PALE NDIO PAKUMSAIDIA NA YEYE NDIPO ATAKAPOKUONA WA MAANA NA SIO KUJISHEBEDUA KUTOA MSAADA AMBAO HUJAOMBWA

 KWELI KABISA KUNA MWANAUME MWENGINE AMESHAKUONA KWAMBA WEWE NDIO MKE ANAYETAKA KUKUOA, NA MSAADA WAKO KWAKE UTAZIDI KUMPA CHACHU YA KUTAKA KUWA NA WEWE NA KUKUPA SIFA KIBAO KWA NDUGU NA MARAFIKI ZAKE..WANAUME WA HIVI WAPO KABISA

NARUDI KWA WALIOOLEWA SASA NYIE MLIO KWENYE NDOA

MTOTO WA KIKE ULIYEMUOMBA MUNGU MUME UKAMPATA UPO KWENYE NDOA UNASHINDWAJE SASA KUA MTOAJI, MTOTO WA KIKE UNAKUA MCHOYO INAHUSU UBINAFSI WA NINI KWENYE NDOA HAUJUI MTAKUA MWILI MMOJA, MNAKAA KWA UMASIKINI KISA UNASHINDWA KUJITOA KUMSAIDIA MUMEO..INAHUSU

PIA JAMANI HATA KAMA UPO KWENYE NDOA LAZIMA UWE MAKINI KATIKA UTOAJI, KUNA WANAUME WENGINE WASHENZI WASHENZI WASHENZI WATABIA UNAWEZA UKAINVEST ASILIMIA MIA SIKU ANAKUONA WA KAZI GANI BIBI UNAACHWA ANAVUTA CHOMBO KINGINE KINAKUJA KUTAWALA MALIZA ZAKO

HAHAHAHAHA LAZIMA KUJITOA KWA MAKINI KAMA MKE HUKU UKIWA NA MALENGO YAKO, NA UKIAMUA KUJITOA HAKIKISHA HIYO MALI UNAYOJITOLEA INAMAJINA YA WATOTO WENU NA SIO MUMEO, ILA KAMA INAJINA LA MUMEO UJIPANGE ZAIDI JINSI YA UTOAJI WAKO

UTAKUTA MWANAMKE UMEOLEWA UNAWATOTO WANNE NA BADO UNAKAA CHUMBA NA SEBULE WAKATI UNAFANYA KAZI UNAUWEZO WA KUPANGA NYUMBA NZIMA, TENA LABDA UNAMSHAARA MKUBWA KULIKO WA MUMEO, LAKINI UBINAFSI TU NDIO UNAKUFANYA UNAISHI MAISHA HAYO, KWAMBA KILA KITU AFANYE MUME..HAIPENDEZI

LAZIMA TUBADILIKE, TAKA KUBADILIKA MIMI FURAHA YANGU NI MUME WANGU KUNISIFU MKE WANGU NATAMBUA MCHANGO WAKO KATIKA MAISHA YANGU NA WANANGU SIO KWAKUZAA TU BALI KIUCHUMI PIA..YANI SIKU NIKIWA SIPO ALIE NAKUONA PENGO LANGU

*****END*****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment