Thursday, July 10, 2014

Hili ni jambo ambalo wengi huwa hawaliongelei ila nataka tuliongelee hapa, hivi unajipanga vipi siku mumeo akifa, umeshawahi kujiuliza itakuaje????...

MMMHHHH MPAKA NIMEHISI KUCHANGANYIKIWA, NASHUKURU MUNGU TUNAPEANA MOYO NA KUFUNDISHANA NINI CHA KUFANYA WAKATI MUME BADO YUPO HAI, ILI ATAKAPOKUA HAYUPO USISHINDWE KUENDELEZA FAMILIA

HAKUNA KITU NINACHOOGOPA KAMA SIKU MUME WANGU ATAKAPOFUNGA MACHO NA ASIAMKE MILELE, NAJUA NITALIA SANA KWA MAMBO MENGI AMBAYO AMENIFANYIA, TUMEFANYA PAMOJA, NITALIA KWA WATOTO WANGU KWA JINSI WANAVYOMPENDA BABA YAO HAWATAMUONA TENA, NITALIA AMENIACHA NA NDUGU ZAKE AMBAO LEO WANANIPENDA KWAKUWA YUPO LAKINI JE KIPINDI AMBACHO HAYUPO ZILE MALI TULIZOCHUMA PAMOJA WATACHUKUA, WATANIFUKUZA,AMA WATAWANYANYAPAA WATOTO WANGU

HAYO NI MASWALI AMBAYO WAKE TULIOOLEWA TUNAJIULIZA, LAKINI PIA WAKATI MUMEO BADO YUPO HAI MNAISHIJE NDANI YA NYUMBA?? NDIO ANATAKIWA KUKUHUDUMIA KWA KILA KITU LAKINI UNAISHI KAMA GOALKEEPER YA KWAMBA KILA KITU UPEWE NA YEYE AMA UNAJISHUGHULISHA MNASAIDIANA KIPATO

KAMA ULIKUWA NI WA KUSUBIRI UPEWE SHOGA YANGU AAMKA CHAKARIKA MWENZANGU, SIKU HIZI WANAWAKE WANACHAKARIKA BIASHARA HUKU NA KULE, HATA KAMA HATAKI UTOKE MARA KWA MARA TAFUTA MARAFIKI WA VIKUNDI LABDA KAMA HIVI CHEZA UPATU ZUNGUSHA HELA ZAKO KWA TIGO PESA SIKU UKIPOKEA WEWE UTAUMWA UENDE HOSPITAL ILI UPITIE BANK UKAWEKE HELA ZAKO..

SOMESHA WATOTO SHULE AMBAZO UNAJUA KABISA LEO MUME WANGU HAYUPO KWA KAZI NINAYOFANYA NA BIASHARA NILIZONAZO SINTOSHINDWA KUENDELEA KUSOMESHA WATOTO, KUWAVISHA WALA KUWALISHA NA KUENDELEA KUWAPA OUTINGS AMBAZO TULIKUWA TUNAWAPA BABA YAO ALIPOKUA HAI

LAZIMA UJUE RIGHTS ZAKO KAMA MKE BAADA YA KUOLEWA NA HII NAONGELEA KISHERIA KWAMBA NDUGU WA MUME WATAKAPO ANZA KUKUFWATA NA KUTAKA UWAPE MALI ZA KAKA YAO UTAANZA KUJITETEA WAPI, ILI UTETEE ULICHOPIGANIA NA MUMEO

MUMEO ANAPOKUA HAI NI VYEMA MKAANDIKIANA KWA MWANASHERIA NA KATIKA KIKAO CHA UNDUGU KWAMBA YEYE AKIFA MALI NI ZA WATOTO JUU YA USIMAMIZI WA MAMA YAO, HII ITAPUNGUZA VURUGU ZA NDUGU, WANAUME WENGI HUWA HAWAPENDI KUANDIKA WAKIDHANI KWAMBA HAO NDUGU HAWAWEZI KUWASUMBUA BAADAE BILA KUJUA MALI NA HELA NI SHETANI MTU ANAWEZA KUKUTOA ROHO AICHUKUE

TUINGIE KATIKA MAPENZI NAJUA WAME ZETU WANATUUDHI SANA MARA NYENGINE YANI UNAWEZA UKAJIKUTA UNAMTUKANA MITUSI AU HATA KUGOMBANA NAYE KISA TU YA MIKWARUZANO ISIYOISHA LAKINI TUNATAKIWA KUWAPENDA SANA JAMANI, LEO ANAKUUDHI UNAMKASIRIKIA KWASABABU YUPO AKIWA HAYUPO JE UTALIA UTAOMBA JAPO AAMAKE SIKU MOJA UMPENDE TU HATA KWA SIKU

UMALAYA, ULEVI, KIBURI, DHARAU,UCHOYO,UBINAFSI NA MABAYA YOTE ALIYOKUA NAYO MUMEO YASIKUFANYE UMCHUKIE SANA UKASHINDWA KUMPENDA KIPINDI ANAPOKUA HAI, KILA SIKU UNAPOAMKA NA KUMKUTA YUPO HAI MSHUKURU MUNGU NA UMPENDE SANA SIKU HIYO KAMA NDIO SIKU YA MWISHO UTAKAYOMUONA HAI

MIMI NDUGU WA MUME WANGU NAWAAMBIAGA KABISA SIKU MUME WANGU KAFA NACHUKUA DOCUMENTS ZOTE NAPELEKA KWETU, NAFUNGA CHUMBA CHANGU NA FUNGUO HALAFU NAKUJA SASA KULIA MSIBA WA MUME WANGU

BAADAE UNAKUJA KUPATA SHIDA WEWE NA WATOTO MPAKA WENGINE WANAANZA KUWA MALAYA SASA ILI UPATE MWANAUME AKUPE HELA UKASOMESHE WATOTO, MARA WATOTO WENGINE NDIO HAWAWEZI TENA KUSOMA WANAKAA TU NYUMBANI KISA MAMA KASHINDWA KUWAPELEKA SHULE BAADA YA BABA KUFA, MARA WANAANZA KUWA WATOTO OMBAOMBA NA MAMA YAO MAANA HAWANA PA KULALA NYUMBA WANENYANG'ANYWA..YANI WANAWAKE NA WATOTO NDIO WANAOTESEKA JAMANI

ILA JAMANI KUNA WANAUME WENGINE NI WABISHI, YANI UKIMWAMBIA KUHUSU KUANDIKA HATAKI KABISA KUSIKIA, YUPO TAYARI MUACHANE LAKINI ASIKUANDIKIE, UKISHAONA HIVYO JAMANI MWANAMKE KUWA MAKINI ISHI KWA MALENGO UNAISHI KAMA SHILINGI UPANDE KWA UPANDE USIWEKE HELA ZAKO NA KILA MALI YAKO KWA MWANAUME, TAFUTA KIWANJA UANZA KUJENGA NA WEWE KIDOGO KIDOGO, HATA KAMA UKIDHULUMIWA WAKATI UNAKIPIGANIA HUKU UNAISHI KWA AMANI KWAKO

KUNA MICHEZO KAMA UMEAJIRIWA TAFUTA MICHEZO MIKUBWA AMBAYO UKIPOKEA UTAPATA MIL 2 NA KUENDELEA UTAWEZA NUNUA KIWANJA NA KUANZA KUJENGA JAPO TARATIBU...LAKINI TU UWE NA SEHEMU YAKO HATA BILA KUMWAMBIA MUMEO KAMA UNAONA UKIMWAMBIA HUTAKUA NA AMANI NACHO ILI AKIWA HAYUPO USIPATE SHIDA

***END****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment