Thursday, July 3, 2014

wanasema mdomo unaumba...

KATIKA NDOA YAKO NA FAMILIA YAKO UNAIZUNGUMZIAJE KILA MARA

KAMA WEWE NI MWANAMKE NA HUJAOLEWA UNAZUNGUMZIAJE MAHUSIANO YAKO AU URAFIKI WAKO KWA WANAUME

KWA NAMNA MOJA AU NYENGINE LEO UPO HAPO ULIPO KWA SABABU YA MDOMO WAKO..NDIO SIO KWAMBA UNAMATUSI AMA UNAONGEA MEMA TU HAPANA IPOJE SASA

TUONGELEE KWA AMBAO HAWANA NDOA YANI HAWAJAOLEWA UTAMKUTA MWANAMKE MZURI SANA, AMESOMA NA ANAKAZI YAKE NZURI LAKINI AKIFUNGUA MDOMO WAKE KUONGELEA KUHUSU WANAUME UTAKIMBIA OOHH SIKU HIZI HAKUNA MAPENZI MAPENZI YALIKUWA ZAMANI, OOHH SIKU HIZI MAMBO YOTE NI KUBANANA TU KWA WAME ZA WATU AU MIYE SIONI WA KUDUMU NAYE SANA SANA NAONA UMRI UNAENDA NITAZAA TU NILEE MWANANGU SI NINAKAZI YANGU BWANA HAKUNA LITAKALONISHINDA

KWELI MIAKA INAZIDI KWENDA TU HUPATI WA KUKUOA UNAOWAPATA WANAKUCHEZEA TU MWISHO UNABEBA MIMBA UNAJIONEA BORA UZAE TU MAANA UMRI UNAENDA UKIDHANI NA KUMUOMBA MUNGU KILA SIKU AKUPE MUME UMESAHAU KWAMBA ULIKUWA UNATAMKA KWA KINYWA CHAKO KWAMBA MUME KWAO SIO LAZIMA BALI MTOTO NDIO HAJA YAKO

KWENYE NDOA ZETU SISI TULIOLEWA UNATAMKA NINI KUHUSU NDOA YAKO NA MUME WAKO UNAMZUNGUMZIAJE MUME WAKO KWA WATU HILI LI MWANAUME YANI NI MALAYA SIJUI NIMEMTOA WAPI, OOHHH MARA MUME WANGU HIKI NA KILE MARA UTANIUA WEWE KWA MAGONJWA YANI MANENO MABAYA YENYE KULETA LAANZA JUU YA NDOA YAKO NDIO UNAKAZANA KUMSEMEA MUMEO..HAIPENDEZI ATATOKAJE KWENYE LAANA KAMA UNAENDELEA KILA MARA KUMNENEA MABAYA

MARA MWANAO ANA MAMBO MACHACHE YAWEZA KUWA MABAYA KAMA YA BABA YAKE BADALA UMUOMBE MUNGU AMUONDOLEE WEWE UNAJITAPA YANI MWANANGU MUUNI KAMA BABA YAKE, AU MWANANGU ANAVAA MLEGEZO KAMA BABA YAKE YANI WEWE BADALA UKEMEE KWA VIZURI NA KUMUOMBA MUNGU AKUSAIDIE HIVYO VIISHE WEWE UNAVINENA KAMA SIFA JAMANI ATAENDELEA KURITHI HIZO TABIA MBAYA ZA BABA YAKE

TUJITAHIDI KATIKA NDOA ZETU NA MAHUSIANO YETU KUNENA MAZURI YANAYOMPENDEZA MUNGU NA MWENZA WETU UTAONA KAMA NDOA YAKO HAITAKUWA YA BARAKA, UTAONA KAMA MUME WAKO HATA BADILIKA MUNGU ALIPOSEMA MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE HAKUKOSEA..KITU KIDOGO TU KITOKACHO MDOMONI MWAKO KINAWEZA KUBOMOA NDOA ULIYOIHANGAIKIA SANA KUIJENGA MPAKA HAPO ILIPO

***END****

Reactions:

1 comments:

  1. Keep it up kwa kweli unatukosha.

    ReplyDelete