Thursday, June 12, 2014

tuongelee kuhusu mume kusikiliza sana ndugu zake haswa wa kiume yani mashemeji zetu...

MASHEMEJI ZETU NI NDUGU WA WAME ZETU AMBAO WAMEZALIWA PAMOJA, WAKAKUA PAMOJA, WAKACHEZA PAMOJA, WAKAENDA SHULE WOTE, WAKAANZA KAMA NI KULEWA NA KUPATA WANAWAKE WOTE, WAKAANZA KUELEZANA SIRI ZA WANAWAKE ZAO WOTE, MPAKA PALE UKAMKUTA WEWE NA ALIPOKUPATA ALIMWAMBIA KAKA YAKE, NA ALIPOTAKA KUKUOA KAKA YAKE ALIKUA MTU WA KWANZA KUJUA

BAADA YA WEWE KUOLEWA WEWE UNAKUJA NA MAWAZO YAKO JINSI UNAVYOTAKA UISHI KWENYE NDOA YAKO, JINSI ULIVYOACHANA NA NDUGU ZAKO NA KUAMBATANA NA MUMEO TU AMBAYE NDIO NDUGU YAKO WA SASA, NA RAFIKI YAKO MKUU

LAKINI KWA MUMEO NI WEWE UMEONGEZEKA KWENYE FAMILIA AU MZUNGUKO WA WATU WAKE, HAIMANIISHI ATAWAACHA NDUGU ZAKE NA KUAMBATANA TU NA WEWE HAPANA SIO KWA WANAUME WENGI, BADO ATASHIKAMANA HASWA NA KAKA ZAKE ANAWEZA ASIWAPE NAFASI SANAAAA KAMA MWANZO LAKINI BADO WATAKUA WAKWANZA KATIKA MAISHA YAKE

LAKINI PIA KUNA WANAUME WENGINE BADO ATAENDELEA KUMUWEKA KAKA YAKE MWANZO HALAFU WEWE WA PILI NA HII NI ASWA KWA WALE WALIOZALIWA LABDA MAPACHA AMA WAPO WANAUME WAWILI TU AU WATATU KATIKA FAMILIA YAO

WEWE KAMA MKE HUWEZI KUMKATAZA MUMEO KWA MANENO KWAMBA SITAKI UWE KARIBU NA KAKA YAKO SHOGA HAPANA TENA UNAWEZA UANZISHE UGOMVI AMBAO UTASHINDWA KUUPOOZA MAANA WALE WATAUNGANA NA WEWE UTABAKI PEKE YAKO TENA UNAWEZA UZALISHE MADHARA MENGINE MAKUBWA

CHA MUHIMU WEWE KAMA MKE KWANZA JITAMBUE WEWE NI NANI KATIKA MAISHA YA MUMEO NA KAKA YAKE NI NANI KATIKA MAISHA YA MUMEO KILA MTU ANA ROLE YAKE YA TOFAUTI YA KUCHEZA KATIKA MAISHA YA MUME

NA WEWE KAMA MKE LAZIMA LAZIMA LAZIMA UWE NA MIPAKA YA NDUGU WA MUMEO NA MUMEO AIJUE MIPAKA YAKO NA KUITHAMINI KWAKUWA WEWE NDIO MLEZI WAKE KWA SASA SIO MAMA YAKE WALA HAO NDUGU ZAKE

LAZIMA WEWE KAMA MKE UFANYE BIDII YA KUMFANYA MUMEO AJUE UNAMPENDA NA UNAPENDA NDUGU ZAKE LAKINI HUTAKI KAKA YAKE ACHUKUE NAFASI YAKO, YA KUWA MUDA WOTE NA MUMEO, MARA KUTEMBEA WAENDE WAO TU WEWE UBAKI NYUMBANI, NA MBAYA ZAIDI HUTAKI WEWE KUBEBA JUKUMU LA KAKA YAKE KAMA NI MUMEO

SHEMEJI ABAKI KUWA SHEMEJI NA KAMA ANAMATATIZO AMA ANAHITAJI SEHEMU YA KUKAA BASI KWA PAMOJA TUMSAIDIE AKIWA MBALI YANI TUMPANGIE HATA CHUMBA KIMOJA KAMA HAJIWEZI, NA KAMA ATAHAMIA KWETU BASI SHEMEJI AISHI KWA MATAKWA YETU SISI SIO YEYE AJIACHIE KAMA HAPA NI KWA MKEWE

NA LAZIMA KAMA MKE UTAKAPOONA SHEMEJI YAKO ANAKOSEA AKIWA KWAKO UNAHAKI NA MAMLAKA YA KUMWAMBIA KWASABABU YEYE ANAKUCHUKULIA POA HAPA SI KWA KAKA YEYE NDIO NAMUHESHIMU SIO HUYU, SASA WEWE UNAPOOENDELEA KUKAA KIMYA UJUE KAKA YAKE HATAMWAMBIA AKIWA ANAOGOPA LAWAMA KWAHIYO NI JUKUMU LAKO KAMA MKE KUMWAMBIA SHEMEJI KITU FULANI NA FULANI SITAKI NA SIKIPENDI NYUMBANI KWANGU

ACHA AKUONE UNAROHO MBAYA, MCHOYO LAKINI WEWE UISHI KWA AMANI NDANI KWAKO HUTAKI KUWA MTUMWA KATIKA NYUMBA YAKO MWENYEWE.

LAKINI PIA KAMA MKE NI VIZURI MARA MOJA MOJA UKAMPA MUMEO NAFASI YA KUWA NA NDUGU YAKE KAMA NI KUTOKA, KULEWA, KUKAA TU NA KUONGELEA YAO YANI USIMBANE SANA MUMEO AKIWA NA NDUGU YAKO THEY NEED MEN TIME ALONE KUONGEA YANAYOWAHUSU

SIDHANI KAMA MUMEO ATAKASIRIKA AMA KUGOMBANA NA WEWE KISAO UMETUMIA SILAHA YAKO YA KUWA MKE VIZURI KWA KUMDHIBITI SHEMEJI YAKO

****END****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment