Thursday, June 12, 2014

MLEMAVU katika ndoa....

Dada mamu ni mmoja kati ya madada niliokuwa nao ambao nawapenda sana na wananipa sana moyo sio kwa kazi hii niifanyayo bali kwenye mambo ya ndoa pia ni kati ya wadada ninao jua wanandoa zaidi ya miaka 12 kwahiyo najua wamepitia mengi sana.

katika mambo mengi sana tuliyoongea kuna moja lilitaka kunitoa chozi akaniambia Rose mdogo wangu usidhani mpaka natimiza miaka 20 ya ndoa sijapitia matatizo, makwaruzano, na hekaheka zote za ndoa ambazo watu wanapitia nimepitia hayo yote ila baadae nikaja kugundua vitu vitatu vikuu

Kwanza kabisa nikumtegemea MUNGU katika ndoa yako, pili nikuashiriki sana katika hizi semina za ndoa unajifunza mambo mapya kila mara na tatu nikuwa mlemavu katika ndoa!!!!

Nikamwambia dada Mamu mlemavu??? akaniambia ndio mlemavu mdogo wangu nikamuuliza nakuaje mlemavu katika ndoa???akaniambia katika ndoa lazima uwe kipofu, kiziwi na kiwete

KIPOFU.. kamwe usitumie macho yako kuchunguza chunguza vitu kwa mumeo ambavyo havitakupa amani, na wala usitumie macho yako kuhukumu mara ukimuona mumeo kasalimiana na mwanamke unaanza maneno oohh yule nani mbona kakukumbatia,mbona umesalimiana naye muda mrefu, acha kabisa. ukiona kwa macho simu ya mumeo iache kama ilivyo usiiguse tena fanya kama umeona bomu ukiligusa litakulipukia.

KIZIWI...kamwe usitumie masikio yako vibaya ukaharibu amani ya ndoa yako watu wakikuletea maneno kuhusu mumeo kuwa kiziwi usiyasikilize na kuanza kugombana na mumeo.

KIWETE.. akaniambia mke mwema hafwatani fwatani na mumewe muda wote bali lazima utenge siku yako ya kuwa na mumeo kama ni jumamosi au jumapili wewe na mumeo tu kama mtatoka out ama mtakaa ndani haya, akaniambia lazima ujifunze kumuamini mumeo sio akiwa mbali unampigia simu kila mara, akichelewa kurudi huna amani kumsumbua kila mara au kumfwta sehemu zake za starehe, lazima uwe mtulivu ionekane tofauti ya mke.

akaniambia mdogo wangu ndoa ni baraka, ndoa ni heshima ukiacha wazazi wako mumeo ndio maisha yako pamoja na watoto wako basi tujifunze kuthamini na kupenda ndoa na wame zetu...

NA MIMI NAKUAMBIA WEWE LEO VAA ULEMAVU MWANAMKE KATIKA NDOA YAKO.

 ****END******

Reactions:

0 comments:

Post a Comment