Tuesday, June 17, 2014

Mwanamke haya yakupe nguvu...

Duniani tunapitia magumu mengi sana. Na wanawake tunapitia mengi zaidi, yani kuanzia mtoto akiwa mdogo wa kike hadi mzee majaribu kwa mwanamke ni mengi sana. Ukivuka hili, linakuja lingine na lingine na lingine. Ila jambo la kutia moyo na kufariji ni kuwa Mungu wetu kamwe hajatuacha wala hatatuacha.
Majaribu ya mwanamke yako kila eneo kuanzia shule, kazi, mahusiano, kiuchumi, marafiki, wakwe, mume, watoto, majirani n.k. na hakika mengine ni makubwa sana kiasi kwamba yakikupata unaona kama dunia imefika mwisho, hakuna msaada. Unakosa wa kumlilia na unaishia kulia ndani ya shuka na bafuni. Napenda kukutia moyo usikate tamaa, usife moyo, muangalie Mungu aliye rafiki yako wa kweli.
Wewe ndiwe unajua jaribu lako limekugusa kiasi gani, mtu mwingine anaweza liona ni dogo na kushangaa kwa nini unalia... Usitegemee faraja ya wanadamu bali muangalie Mungu aliye msaada wako. Haijlishi nchi imebadilika kiasi gani, milima inatetemeka kwa utisho, mafuriko yamejaa... Mungu wa majeshi yupo nasi na ni ngome yetu daima.
ZAB. 46:1-3, 11
"Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu."

Imeandikwa na Women of Christ


Reactions:

0 comments:

Post a Comment