Wednesday, June 11, 2014

tumechoka kupigwa, kunyanyaswa, kutokuthaminiwa, kudharauliwa, kuishi kujua mumeo ni malaya, ama kugombana na mwanamke mwenzio kisa mumeo, lakini chanzo ya haya yote ni nini...

MATATIZO MENGI HAYA TUNAYOYAONA LEO KWENYE FAMILIA ZETU MAMBO AMBAYO YANATUUMIZA NI KWASABABU YA MALEZI TULIYOPEWA KABLA HATUJAOANA

NDIO MAANA ENZI ZA WAZAZI WETU MTU AKIJA KUKUCHUMBIA KUKUOA YANI WATAFATILIA UKOO WAO WOTE WAUCHUNGUZE VIZURI NA KUUJUA KABLA HUJAOLEWA ILI WAJUE UNAENDA KWENYE FAMILIA GANI NA KAMA WALIKUA WANAMAMBO YA AJABU LABDA USINGERUHUSIWA KUOLEWA HUKO

KUNA FAMILIA NYENGINE YANI WANAUME KWAO NI KAMA MUNGU WAO YANI MWANAUME AKIONGEA AMEONGEA MWANAMKE HURUHUSIWE KUCHANGIA WALA KUKOHOA WANAUME WAKIONGEA

MWANAUME AKITAKA UNYUMBA HATA KAMA UPO KWENYE SIKU ZAKO LAZIMA UMPE, HATA KAMA UNAUMWA LAZIMA UMPE, HATA KAMA HUJISIKII LAZIMA UMPE, HATAKAMA UMECHOSHWA NA KAZI LAZIMA UMPE..YANI HIYO NI HAKI YA MWANAUME TU SIO YA KWAKO

TENA USIOMBE UOLEWE NA UKALIPIWA MAHARI KUBWA BASI ILE MAHARI ITAKUCHAPA WEWE SIKU ZOTE ZA NDOA YAKO MWANAUME ATAKUNYANYASA NAYO MKIGOMBANA KIDOGO UTACHAPIWA NAYO (NDIO MAANA MIMI NAONAGA BORA NDOA YA KIISLAM MAHARI UNAITAJA MWENYEWE HATA 5000 NAOLEWA) UKINICHAPA NA HIYO FIMBO NAKURUDISHIA 5000 YAKO..MAANA VINAZIDI SASA

MUMEO AMELELEWA KWENYE FAMILIA AMBAYO BABA ANAMPIGA SANA MAMA, TENA MPAKA ANAMSIGA CHINI KWA KIATU KAMA MBWA, HALAFU MAMA ANAUGULIA KESHO YAKE ANAKUWA KAMA HAKUNA KILICHOTOKEA MAPENZI MOTOMOTO KWA BABA UNATEGEMEA HUYU MTOTO AKIOA INAKUWAJE??? SI ATAFANYA HIVYO NAKUJUA NI KAWAIDA KWA MWANAMKE KUFANYIWA HIVYO!!!!

JAMANI WAZUNGU WANASEMA CHARITY BEGINS AT HOME

JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LA BABA NA MAMA, LAKINI MTOTO ANAAMBUKIZWA UPENDO, NA MAPENZI NA MAMA TU

NDIO MAANA MTOTO ANAPOZALIWA BAADA YA MUDA MAMA KUPATA NGUVU UNAPEWA MWANAO UMNYONYESHE NA UNAAMBIWA UMWANGALIE MACHONI AU NCHI ZILIZOENDELEA MTOTO ANAACHWA UCHI NA MAMA ANAVULIWA NGUO JUU ILI AMKUMBATIE MWANAE KUMPA ULE UPENDO WA MAMA SKIN TO SKIN

 WEWE MAMA NDIO WAKUBADILISHA NA KUTENGENEZA MUME BORA WA MTOTO WA MAMA MWENGINE NA WEWE MAMA NDIO WA KUTENGENEZA MKE BORA KWA MTOTO WA MAMA MWENGINE

MUNGU AMENIBARIKI KUNIPA WATOTO WAKIKE NA WAKIUME MALEZI YAO NI TOFAUTI NA WANAJIBU TOFAUTI ILA KWAKUWA NI MAPACHA WA NJE MARA NYINGI WANAKUWA WANAFANYA VITU VINAYOENDANA LA SIVYO NI UGOMVI LAKINI KWAKUWA NAJUA HIVYO VITU NI VYA MANUFAA BASI HUWAACHA WAFANYE

KWA MFANO: MIMI HUWA NAMFUNDISHA MWANANGU WA KIKE KAZI ZA NDANI MWAKA HUU ANATIMIZA MIAKA MITANO KWANZIA MWAKA JANA NILIANZA KUMFUNDISHA KAZI NDOGONDOGO WANAPOKUJA NYUMBANI MAANA WANAKAA KWA BIBI YAO

 MIMI NAPENDA SANA KUPIKA YANI AFYA YA FAMILIA YANGU NAIJENGA MWENYEWE LABDA NIWE NIMECHOKA SANA NAMUACHIA DADA APIKE LAKINI KWA UANGALIZI WANGU, KWAHIYO NIKIWA NAPIKA LAZIMA KHLOE AWE JIKONI

NITAMPA HATA KAZI YA KUOSHA TU NYANYA, HALAFU MIMI NIMENYE, AU NITAMPA KAZI YA KUTWANGA VITUNGUU SWAUMU LAKINI HAMNA KAZI ANAYOIPENDA KAMA KUSUUZA VYOMBO NA KUPANGA, YANI ANAIPENDA SANA

SASA NA KHREFLO AMBAYE NI MWANANGU WA KIUME AKIONA ZILE PURUKUSHANI ZA JIKONI NA YEYE ANAKUJA ANATAKA APIKE BASI NITAMBEBA NA KUMPA MWIKO AKOROGE MBOGA, AU NITAMPA KHLOE KAZI NYENGINE YEYE ATWANGE VITUNGUU WENYEWE WANAFURAHI SANA KUFANYA HIZO KAZI

KHLOE MUNGU AKIPENDA NAJUA ATAIPIKIA FAMILIA YAKE BAADAE NA KHREFLO PIA NAMUONYESHA JUKUMU LA JIKONI SIO LA MWANAMKE TU HATA BABA PIA ANAWEZA MSAIDIA MKEWE KUPIKA PANAPOHITAJIKA..NI MAPENZI TU SIO LIMBWATA

KHLOE SASA AENDE KULALA HUJARUDI NYUMBANI ASUBUHI HIYO NDIO KESI YA KWANZA TU AKIAMKA MAMA,BABA JANA HUJARUDI NYUMBANI NA HAPO UTAKUTA KALALA SAA MBILI NA WEWE UMEINGIA SAA TATU LAKINI NI UGOMVI ILA NASHUKURU YA KWAMBA WANAJUA LAZIMA KUWAHI KURUDI NYUMBANI KABLA WATOTO HAWAJALALA WATAKUA WAKILIJUA HILO NA WAO KUFANYA HIVYO WAKIWA NA FAMILIA ZAO

KITU AMBACHO NAKIFANYIA KAZI SASA NI KHREFLO MWANANGU ANAMKONO MWEPESI SANA WA KUPIGA YANI KITU KIDOGO UMEPIGWA YANI NAMUOMBEA SANA KWA MUNGU HIYO AACHE NA KUJITAHIDI KUMFUNDISHA KUPIGA SIO SULUHISHO LA KILA KITU AKIKUKOSEA MSAMEHE, AMA AKICHUKUA KITU CHAKO MUACHIE ACHEZEE NI NDUGU YAKO LAZIMA MPENDANE..BASI ATAFANYA SIKU MOJA YA PILI KARUDIA KUPIGA TENA...YYUEUEWWWWW

CHA JUU ZAIDI NI LAZIMA TUJIFUNZE KUWAFUNDISHA KUHUSU DINI NA KUMJUA MUNGU, KUSALI KWA PAMOJA KABLA YA KULA AU KULALA MIMI WATOTO WANGU NILIANZA KUWAFUNDISHA HIVYO MUDA NA NINASHUKURU WAMEZOEA SASA, NA HIVI SIKU HIZI WANASOMA SHULE YA MASISTA YA KIKATOLIKI NAMSHUKURU MUNGU WANAMPENDA NA KUTAKA KUJUA KUSALI ZAIDI

MAJUZI WALIVYOKUJA KHREFLO AKANIFUNDISHA NYIMBO MOJA AMBAYO MANENO YAKE YANASEMA HIVI: NAMPENDA YESU YEYE NI MWOKOZI WANGU KILA SIKU....ANAIIMBA KWA KISWAHILI NA KINGEREZA BASI NA MIMI KUZIDI KUMTIA MOYO KWA SIKU NAAIIMBA MARA TATU AU NNE NA KUONGEA NAYE KUHUSU YESU

NI JUKUMU LETU SISI KINA MAMA KUKATAA MABAYA YOTE TULIYOFANYIWA NA WAME ZETU KUYAPELEKEA KWA WATOTO WETU, TUJITAHIDI KUWALEA WAKITAKA KUMJUA MUNGU, KUTHAMINIANA, KUPENDANA KWA DHATI NA KUHESHIMIANA, WAJUE UKIKOSEWA CHA KWANZA NI KUSAMEHE NA SIO KUPIGA.

WEWE UKIFANYA HIVYO, UKAWAELEZA NA WAZAZI WENGINE NA WENGINE NA WENGINE, WATOTO WETU HAWATAKAA KULIA VILIO TULIVYOLIA SISI, NDOA ZITADUMU, NA BARAKA ZA MUNGU ZITATAWALA JUU YAO, UTAUONA UZEE WAKO UKILA MATUNDA YA BARAKA ZA WATOTO WAKO.

****END*****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment