Monday, December 2, 2013

Kila mwanamke ana jumamosi na ijumaa yake, hata wakikubania vipi ipo siku wataachia...PART 3

neema kwakuwa alikuwa ameshaumizwa sana na michael akaona wanaume wote ndio haohao akamwambia unataka nini yule kaka anaitwa sam akamuuliza neema mimi nilikuwa tu nataka kuongea na wewe neema akamjibu kwamba hana muda wa kupoteza anawahi nyumbani

basi kumbe yule kaka alishampeleleza neema na akawa ameshaambiwa kila kitu ambacho neema amepitia kwahiyo alishajua kinachoendelea na ndio maana neema hataki mwanaume kwahiyo hakuchoka kila jioni kwenda kazini kwa neema na kumsubiri nje anapotoka

ikapita miezi miwili amini msiamini yule kaka kila siku ya kazi alikuwa pale ili aweze tu kuongea na neema wanawake wa ofisini kwa neema walimshangaa sana neema kukataa kuongea na huyo kaka mwenye hela zake na ni mzuri wa sura akawa anawaambia kama mnamtka basi mumchukue nyie

baada ya mwaka tokea matatizo yale neema siku hiyo akaamua tu kumsikiliza yule kaka alipokuja siku hiyo akamuomba aingie kwenye gari neema akaingia wakaenda protea hotel kuongea

neema hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia hoteli za kitalii na kuagiza chakula na kinywaji basi akala vizuri yule kaka akmwaga amaneno yake na neema akasikiliza na kuahidi kuyafanyia kazi

basi neema kama kawaida yake akaenda tena kumuhadithia astazia..kumbukeni hajui bado kama astazia ndio aliyemuharibia kwa michael astazia akajifanya kafurahi sana kumbe moyoni kilimuuma sana kwanini neema tena kwa mara nyengine tena huyu anahela zaidi kuliko michael

basi jioni hiyo akampigia simu sam na kumwmabia sawa nimekubali kuwa na wewe sam alifurahi sana sana sana

kesho yake neema alipoenda kazini wakati anatoka kama kawaida sam alikuja kumchukua akampeleka sehemu ya kula na kumrudisha nyumbani alipofika nyumbani sam akampa neema millioni moja ya matumizi yake neema hakuamini alikuwa anasikia tu kuna wanaume wanahonga lakini alikuwa hajawahi kuongwa alitetemeka alipokuwa anapokea zile hela alitaka kukataa lakini moyo wake ulizitamani

akachukua akaweka kwenye pochi akambusu sam akaondoka cha kwanza alivyofika ndani ni kumuhadithia astazia...astazia alitaka kufa akamwambia neema wewe pokea tu hela za huyo baba hata humjui shauri yako akawa anampamadongo neema kiaina lakini neema hakujali akaziweka vizuri kesho akapelekea bak

Basi mapenzi yakawa motomoto huku astazia anaumia, neema alipendeza sana kila mtu akawa anamsifia

Neema akarudia tena kosa lake bila kujua weekend anamchukua astazia wanatoka wote kama zamani

Yani astazia wivu na roho mbaya ikazidi mara mbili akaapa moyoni kwamba atamkomesha neema tena sianajifanya anazali atalia mara ya pili

Baada ya astazia kumzoea sam akatafuta siku moja akampigia na kumueleza yote ya uongo kuhusu neema na kama ushahidi anataka angepewa

Sam aliumia sana kwa kusikia hayo na hakuamini na ndio akapata picha itakuwa ni umalaya huu ndio maana yule mwanaume alumkimbia mmhhhh

Lakini sam alkuwa mtu mzima aliyaelewa mapenzi hakutaka kusikia kutoka kwa astazia bali alimpigia simu neema na kumwambia angependa kesho atakapomchukua kazini kwa mara ya kwanza aende naye nyumbani kwake...neema akasita lakini hakukataa

Kesho yake sam akamchukua neema mpaka nyumbani kwake goba wakafunguliwa na mlinzi na baadae nyumba ikafunguliwa na dada wa kazi

Wakaingia ndani kwenye gorofa zuri sana neema hajawahi ona, kila kona nyumba ilikuwa nzuri yenye vitu vya thamani na ni safi ajabu, mara akaja msichana wa kazi mwengine tofauti na aliyewafungulia mlango na kuwauliza watakunywa nini na kama aandae chakula

Neema akasema atakunywa maji tu ila sam akamwambia mpenzi kwanini usinywe juice kuwa huru hapa ni kwako..sam akamwambia dada ampe neema juice na atengeneze wali na kuku

Sam hakuwa na haraka ya kumueleza neema bali waliongea tu mambo mengine na neema akaanza kuuliza mengi ya undani ya maisha ya sam kwanzia ndugu,kazi na utajiri wake huo bila kusahau wanawake wake wa nyuma

Sam akamwambia anashughulika na biashara za migodi, hajawahi kuoa ila alikuwa na mwanamke ambaye alitaka kumuoa ila wazazi wake wakampeleka ulaya hakurudi tena na sasa ameolewa huko na mzungu

Kama anavyojua ofisi zake zipo karibia na kwao ndio maana alimuona hapo..sam akamuuliza neema vipi wewe upande wako

Najua hatujawa wote muda mrefu kuna machache umeniambia lakini je kuna ambayo hujaniambia kuhusu wewe na maisha yako

Neema akamwambia hapana kila kitu nimekwambia

sam akamwambia unanificha kuhusu hao wanaume uliokuwa nao wa nje wanaokuhonga??? neema alishtuka sana na kumwambia sam unamaanisha 

sam ndio kumpasulia jipu neema lote aliloambiwa na astazia

looohhh neema alipasuka kwa kulia ghafla alishindwa kujizuia alilia sana akasema mimi mbona sina kitu chochote kama hico unachoniambia kama huniamini basi muite astazia umuulize mbele yangu

basi sam ndio kuanza kumbembeleza neema mara dada akaja kuwaambia chakula tayari neema akamwambia sam hana hamu ya kula tena anataka tu kuondoka kwwenda nyumbani ila sam alijitahidi kumbembeleza neema hadi neema akarudi kwenye hali yake ya kawaida na akaenda kula

wakati wanakula neema akawa anajiwazia moyoni kwanini astazia aliamua kumwambia sam yale maneno ya uongo akasema atamuuliza akifika nyumbani

UNATAKA KUJUWA ILIKUWAJE ALIPOFIKA NYUMBANI...SUBIRIA PART 4

Reactions:

0 comments:

Post a Comment