Tuesday, December 10, 2013

SHUKRANI...

Shukrani nyingi sana ziwaendee wale wote waliokuja 9/12/2013 katika mafundo pale majestic hall sinza kwa remmy, natumaini mmejifunza mengi sana kama wengi wenu mlivyoniambia kuna mengi hamkuyajua ila mkaondoka na mengi mpya.

Kama tunavyojua hakuna shughuli inayonyooka kama kuna lililotokea ambalo limekukera ama kulikuwa na mapungufu sisi ni binadamu na ninashukuru kwa maoni yenu na tutazidi kujirekebisha.

Wengine hawakuwa na madera kutokana na kuchelewa kulipa jamani siku ya mwisho ya kugawa madera ni siku moja kabla ya siku ya kufunda kwahiyo ninapotangaza hakikisha hata kwasimu kama huna hela mkononi kwamba nikuwekee utalipa siku hiyo si ndio raha ya kuja kwenye shughuli sio wenzio wamependeza na sare wewe umevaa nguo zako tu za kawaida.

Tukutane tena kwenye mafundo mengine na madera yetu mengine MUNGU akitujaalia uhai na afya njema mwezi wa nne..mwezi wa pili nitaenda kufunda nairobi wako wapi watu wa nairobiiii hatareeeee tuombeane uhai MUNGU akipenda nitakuwa huko mwezi wa pili...

Gracias

Reactions:

0 comments:

Post a Comment