Friday, October 18, 2013

Neno Kuntu

Mwanaume usijisifie kwa sababu unamcontrol mke wako, hawezi kusema chochote kwako na maamuzi yako ndio final. Mke ni msaidizi, anakusaidia pale anapoona unahitaji msaada, anakushauri pale unapokuwa na maamuzi ya kufanya, mnashauriana kwa ajili ya kujenga familia na anakupa mawazo ya kuboresha maisha yenu.
Kumtawala mke hadi anashindwa kutoa mawazo yake, kukusaidia unapotaka kufanya maamuzi mabaya na kukushauri unapokosea ni kujiumiza mwenyewe. Na wanaume wengi wanaowatawala wake zao na kuwanyima uhuru wa kuongea kuhusu mambo ya familia hutafuta ushauri kwa ndugu zao na marafiki. Haiingii akilini unaacha kukaa na mkeo upange mipango ya maendeleo na kusikia ushauri wake unaenda kusikiliza ushauri wa marafiki ambao mambo yakiharibika wala hawahusiki na hayawagusi. Wanaume mjifunze kuwashirikisha na kuwasikiliza wake zenu.
Mke ni zawadi umepewa na Mungu, na unapoacha kumshirikisha unaidhulumu ndoa yako.

Imeandikwa na: Woman of Christ

0 comments:

Post a Comment