Thursday, October 17, 2013

mategemeo ya mpenzi wako kwako kabla ya ndoa unayajua, ama unadhani kuzungusha kiuno tu ndio kitakupa ndoa nitaanza kugusia upande wa wanawake halafu somo la pili ni upande wa wanaume....

wanawake wengi wanapotaka kuingia katika mahusiani wanaingia na akili na muonekano wa nje wa mwanaume

kuna vitu wanawake wamejiwekea kwamba anataka mwanaume anayefanya kazi ya kulipwa mshahara mkubwa, mwanaume mwenye gari, mwanaume ana simu kali, mwanamme anayemuhonga hela, mwanaume mwenye mvuto yani anavaa anapendeza, wengine wanataka mwanaume mrefu mwenye mwili yani ukitembea naye unaonekana kweli una mwanaume

na wanapotongozwa na mwanaume wa aina hiyo wao ndio wanaona yani wamepata mwanaume wakipata huo muonekano wa nje wanajuwa ndio wamepata kila kitu kwahiyo tokea mwanzo wa mahusiano wao wanaenjoy tu kile wanachokiona nje na kitandani bila kuanza kupanga, kuwaza na kumsoma huyo mwanaume kama ni HUSBAND material au la

na ndio maana katika mahusiano wanawake huumizwa sana kimapenzi mpaka kujiua kuliko wanaume kwanini kwasababu wanawake wao tokea siku ya kwanza akishampata mwanaume anayemtaka basi atampenda kwa kila kitu moyo na mwili wake wote kwa haraka wakati mwanaume yeye hakupi vyote anakuangalia speed yako kwanza mpaka atakapoona kweli ndio kitu anachotaka ndio ataanza kukupenda kwa ukweli sasa lakini akiona hakuna kitu hapo atakuchukulia poapoa na baadae anakupotezea sasa wewe uliyempenda 100% ndio unaanza kufa kwa mawazo na ugonjwa wa moyo

naanza sasa kufundisha kwa mfano

kuna kaka mmoja ni mzuri jamani, mtanashati, anasifa zote mwanamke anapenda kwa mwanaume namjua sana na ni rafiki mkubwa wa familia yetu

alipata mwananmke mmoja ambaye na yeye kwakweli ni mzuri hawa masista duu sijui wenyewe wasichana wa kileo mnawaita wakawa kwenye mahusiano motomoto

mwanaume yeye alikuwa amepanga kwake na huyu msichana alikuwa mtoto wa chuo kwahiyo anakaa hostel simnajua watoto wa siku hizi tena unakaa hostel lakini ukipata bwana unaenda kuhemea kila leo hostel tena hukai au hela ya hostel unakula

basi shoga akawa na yeye anakaa kwa bwana, unajuwa sijui nyie lakini mimi kabla mume wangu hajanioa tulivyoanza tu uchumba nikamwambia baba utanipa funguo ya nyumbani kwako maana sisi si wapenzi kwako ni kwangu nataka nije muda wowote ninaotaka mimi..nahivi alipanga karibu na nyumbani kwetu mbona alijuta nilikuwa simpi muda wa kuhema..hahaha

basi mtoto wa kike nikapewa funguo, nikawa naenda najishughulisha kufua, kufanya usafi na picha zangu kibao nikaweka za frame pale shoga hata ukiletwa usiku bahati mbaya ujuwe nyumba hii ina mwenyewe wewe jikinge tu na majambazi usiku asubuhi paki uondoke

sasa kumbe marafiki wa mume wangu walikuwa wakija na kukuta ninavyoshughulika walikuwa wanapenda na kunisifia sana kwa husband ila mimi nilikuwa sijui maana yule bwana alikuwa hana jiko lakini nilikuwa naenda nyumbani napakua chakula kwenye hotpot namletea mume wangu inahusu nini kumlisha vya barabarani kila siku...ebooo basi hivyohivyo na mengine mengi mpaka nikaolewa

NARUDI KWENYE STORY SASA: basi shoga mapenzi yanaendelea lakini hata siku moja humkuti anafanya usafi, anapika, wala kufua..nguo zinapelekwa kwa dobi chakula wanakula barabarani usafi mpaka bwana mwenyewe afanye weekend dada yeye kazi yake ni kuzungusha tu kiuno baby hiki, baby kile baasi

nakumbuka siku hiyo ilikuwa jumamosi mimi huyo nikaenda kumtembelea shoga nyumbani kwake maana siku nyengine tulikuwa tunakutana juu kwa juu nikamkuta mwanaume anafanya usafi anasogeza makabati mavumbi kibao akamwambia mpenzi wake tumalize basi usafi ndio uondoke shoga akamwambia baby siunajua nina pumu siwezi kuwa karibu na mavumbi mailizia tu

Dada Rose twende bwana, nikasema huyu mtoto mshenzi kweli ngoja nimstahi hapa nikampe vidonge vyake mbele ya safari nikiwa nimekaa maana nikimchambia hapa bwana atamuacha leoleo nionekane nimemuharibia

shoga tukafika sehemu tukawa tumekaa tunasubiri wamenzi waje sasa jamani nilimchambaaaa sitaki kuandika hapa maana nitamaliza space, mpumbavu alijuta mpaka chakula akashindwa kula mbona siku hiyohiyo alienda bank akatoa hela akaenda kariakoo akanunua jiko, sufuria,mabeseni, na makorokoro yote ya mwanamke yanayotakiwa nyumbani

kisingizio chake siwezi kupika kisa tunakaa chumba kimoja nikamwambia mtoto unawazimu wewe huoni wapangaji wenzio wanapikia kwenye corridor mfyuuuu unaendekeza usistaduu kama hujui kupika bora uboronge mwanaume ajuwe ulijaribu, oohhh kufua sijui basi utafua zile nguo laini tu hizo ngumu endeleeni kupeleka kwa dobi na usafi utafanya siku ya kutoa makabati ndio atakusaidia ili pumu isikuue

shoga akaanza kujitahidi kubadilika lakini mwanaume alikuwa ameshaingiwa na kinyongo maana kila wakizozana tusi likawa mbona mwenzio Rose kabla hajaolewa alikuwa anajituma sana kwa mumewe kwanini wewe huwezi wewe ni wanamke wa aina gani

shoga basi yale maneno yakaanza kumnyima usingizi akihisi kuna jambo basi bwana akaacha nyumba na kuondoka akaachana na yule bwana

MUNGU sio baba wa mtu wala mjomba wa mtu akampa yule bwana mwanamke mwengine

ndugu yule mwanamke alikuwa anajua kujituma, anafua nguo za bwana, ukiingia hile nyumba hukanyagi mchanga, unakuta pasafi yani mpaka chakula yule dada akawa anahakikisha bwana hali vya barabarani yani jamaa akawa mwenye furaha hata siku moja sijawahi kumkuta anafanya usafi wala nini

msichana anajua kujipangilia nyumbani hiki kigeuzwe hapa, hiki toa, mara anunue hiki alete kwa mume yani nyumba ukiingia utaipenda kwakweli alijua kumtunza yule bwana na MUNGU akawabariki ndani ya mwaka tu wakaoana na sasa wanamtoto wa kiume na maisha yanasonga

*******END********

WANAWAKE MNAJIFUNZA NINI HAPO LAZIMA KAMA MWANAMKE KWANZA USIENDE TU KWENYE MAHUSIANO KWA KUANGALIA PICHA YA NJE

NENDA UKAANGALIE KAMA HUYU MWANAUME ANAWEZA KUWA MUME NA JE NAMPENDA KWELI UKISHAONA UNAMPENDA KWELI BASI KUWA WIFE MATERIAL MSAIDIE MWANAUME HATA KWA MAWAZO TU SIO UNAKAA TU WEWE KAZI YAKO IWE KUZUNGUSHA KIUNO TU

KIKITEGUKA JE UTAZUNGUSHA NINI SASA...

YANI WEWE UINGIE KATIKA MAISHA YA MWANAUME NA AJUWE KWELI HAKUNA MWANAMKE KAMA WEWE, UKAMBADILISHE HATA KAMA ALIKUWA SIO MUOAJE AKAJUWE UMUHIMU WA MKE NA KUTAKA KUKUOA SIO UNAKAA TU UMEKAZANA BABY,BABY,MFYUUUUUUUUUUUUUU

Reactions:

1 comments:

  1. Dada Rose mimi ni fan wako. Asante sana kwa kutufundisha mabinti wa Kitanzania tusipoteze maadili yetu kwa visingizio kama ooo sijui utandawazi au utajiri.

    ReplyDelete