Thursday, September 19, 2013

NIMESHANGAZWA....

Mimi wakati nataka kuolewa nilikuwa nafikiria ndoa yani ni maisha ya raha tele yani wewe na mumeo hakuna kufichana siri yoyote yani chako chake chake chako na kweli ilikuwa hivyo mpaka siku moja sijui nilikuwa nataka kutumiwa kitu i think from abroad sasa email yangu ikawa na matatizo kwakuwa nyumbani tuna PC nikamwambia mume wangu anipe email yake na password nitumiwe huo mzigo kutumia email yake hahahahahahaha jicho na jibu nililopewa hapo alikataa katu katu japo alikataa kwa mapenzi lakini ujumbe ulionifikia mimi ni NO...anyways still mzigo ulikuja through mail yake japo sikupewa password hapo sasa ndio akili ikaanza kuniika sawa na kujiuliza maswali i thought ndoa tunatakiwa kuwa mwili mmoja kumbe kuna sehemu mpo mwili mmoja na sehemu nyengine ni miili tofauti...hahahahaha lakini miaka ilivyozidi kwenda siku hizi ni mwili mmoja kila sehemu password zote ninazo (naona ameanza kuzeeka anajionea kila kitu sawa)...lets get to the point

Wiki hii kulikuwa na msiba wa mtu wa karibu sana na familia yangu, huyu mwanaume alikuwaga muislam katika pita pita zake akakutana na mdada ambaye alimpenda sana sana sana sana lakini hawakuweza kuoana kwasababu ya dini zao kwakuwa yule kaka alimpenda sana yule dada akaona isiwe tabu akabadilisha dini na kuwa mkristo japo ndugu wa huyu jamaa hawakupenda lakini hawakuwa na la kufanya  wakaoana na wakazaa mtoto wa kike mmoja.

Ndoa yao imedumu miaka zaidi ya kumi sasa huyu baba akaumwa kama mwaka hivi ila ikawa analazwa na kurudi nyumbani muda wote huo anahudumiwa na mkewe, sasa mwanzo huu wa mwezi akawa amezidiwa sana akakataa na kurudi hospital akasema ni bora akae tu nyumbani kama ni kufa afe nyumbani kwake.

Siku moja mkewe anasema akaagiza ndugu zake wa kiume aliozaliwa nao ambao wote ni waislam akaomba waje na shekh basi yule baba akamfukuza chumbani mkewe na akamuomba shekh amrudishe kwenye dini yake ya kislam, na ikawa hivyo bila hata kumwambia mkewe.

Basi mama wa watu akaendelea kumuuguza mumewe, mpaka yule baba alivyofariki jumatatu, sasa kasheshe ndipo zilipoanza hapa ndugu zake ndio kuja na kuanza msiba na wakasema huu msiba utafanyika kislam kwakuwa marehemu alirudi dini yake dakika za mwisho mkewe kusikia hivyo tu akazimia, basi watu wakampepea pale akawa sawa, wanakwaya wa kanisa ambalo walikuwa wanasali wakaja ili waimbe wakafukuzwa, basi ikawa bala bin balaa msiba ukatengwa sasa wanawake wake kwao na wanaume wakae kwao.

Wakati bado analia kwa uchungu mumewe kubadili dini bila kumwambia mara anatambulishwa kwa wake wenzie watatu ambao jamaa aliwaoa nyuma kwa ndoa ya kislam na kuzaa nao watoto kabla ya kubadili dini na kumuoa yeye yule mama akazimia tena..jamani watu tulisikitika

Basi yule mama kuamka akaonyeshwa na watoto wa yule baba ni wakubwa kuliko hata wa kwake, basi tena hapo jinsi yule mama livyokuwa analia jamani hataka kama wewe mgumu kama sabuni ya geisha lazima chozi litakutoka akawa anaongea maneno ya uchungu hakuamini kama mumewe angemficha yote hayo si bora angemwambia tu ili ajuwe kwajinsi alivyokuwa anampenda angekubaliana nayo tu kwanini ameacha leo anaumbuka..


Jamani pata tu picha kwa kukuhadithia ungekuwepo ungelia sana....

Na nyie wame za watu jamani ndio nini hayo mnayofanya tatizo manpenda sana kuchukulia vitu kirahisi unamficha mkeo ili iwaje basi wewe ni muuaji kama unaweza ukaka na mkeo nyumba moja usimwambie unamtoto unabalaa, yani anabahati kazikwa kislam naona ingekuwa mimi wakati wa kuaga kabla hujazikiwa ningekupiga bonge la bao MAMAE ukazidi kufia mbele..

Wewe na mkeo mnatakiwa muwe kitu kimoja hata kama umezaa watoto kumi nje mueleze mkeo ajuwe mtaishije na hao watoto watapataej huduma kwanini mtoto wa watu ataeseke nje akose huduma muhimu  kwasababu ya umalaya wako...

Msonyooooooooooooooooooooooooooooooooooooo kwako wewe mume wa mtu kama na wewe unavitu vyako unavyomicha mkeo haswa kama ni WATOTO..Reactions:

0 comments:

Post a Comment