Wednesday, September 18, 2013

MKE ANA IBA AU ANACHUKUA......

kuna kitu kimoja ambacho nadhani nilishawahi kugusia siku za nyuma aua kama sio humu basi ni kwenye facebook groups, hivi katika maisha yetu sisi wanandoa wewe mwanaume mkeo akichukuwa hela kwenye wallet yako unaichukuliaje????

Jamani kuna wanaume wengine yani hilo ni kosa kubwa sana na wanakuwa na hasira sana kwanini mkewe KAIBA hela zake, tena kuna mmoja mkewe aliwahi kunihadithia mumewe siku hizi akirudi nyumbani anaweka wallet chini ya mto ndio analala na asubuhi kwelnda kuoga anaenda nayo bafuni ebooooo huu si wenda wa zimu...

Sasa wewe mwanaume unafanya kazi ili iwaje naamini ili familia yako ikae vizuri wale, wavae, waende shule, mkae kwenye nyumba nzuri na mkeo apendeze au unataka apendezeshwe barabarani kwasababu jamani wanaume mtambue kuna wanaume hodari kwa kupendezesha wake za watu tena wenyewe wanakwambia mpaka nikimalizana na wewe mumeo atatia akili, na mpaka amalizane na mkeo basi mkeo atakuwa ameshachanganyikiwa kwa huyo mwanaume.

Sisi wanawake tunapenda mtu anayejuwa kutuhudumia, tupendeze yani ukipita kila mtu ajue yule mke wa fulani, sasa wewe mume unaenda kuoga na wallet siku ndio umeisahau bahati mbaya mkeo anachukuwa hela halafu unamkasirikia...hahahaha 

Wapendeni wake zenu jamani mpendezeshe na uhakikishe unahudumia vyema familia yako watoto waende shule na mambo yote nyumbani yawe sawa..

Nimegundua wanaume wengi kwakuwa wake zao wanafanya kazi basi anaona jukumu la kumpendezesha mke wake sio lake tena, au kwakuwa mkewe anafanya kazi basi nyumbani hatoi tena hela, hapana jamani hata vitabu vya dini vinasema mwanaume ndio kichwa cha familia hudumia tu familia yako hata kama mkeo ana kipato naamini sio kwamba hela yake uioni ipo tu sehemu ambapo mkeo anakusaidia haiwezekani mwanamke anafanya kazi na kupata hela halafu asihudumie familia yake hata kidogo...hamana kitu kama hicho

Ukimpa mkeo hela kamwe hata chukua bila ruhusa yako, ila ukiwa mbinafsi na mchoyo ndio unampelekea yeye kuchukuwa hela zenu kinguvu...

Reactions:

0 comments:

Post a Comment