Thursday, September 19, 2013

MENGINE HAYA...

BAADA YA KUTOA MADA YA YULE DADA ALIYEFICHWA MENGI NA MUMEWE KUNA MWENGINE NA YEYE AKANIANDIKIA HII BADO NAONGEA NAYE JINSI YA KUMSAIDIA KAMA NA WEWE UNAWAZO UNAKARIBISHWA TATIZO LA KWANINI COMMENTS ZA WENGINE HAZIFIKI NA WENGINE ZINAFIKA HATA SIJUI NILIFANYAJE TENA MAANA NI JANGA LA TAIFA...


Habari Dada,

Mimi ni mfatiliaji sana wa blog yako, mara nyingi nasoma mada unazoweka ila kucomment ndo nashindwa.

Leo nimekuandikia kwa sababu kuna mada umeweka imenigusa sana tena sana. Nimejifunza kitu ambacho kina ukweli ndani yake.
Natarajia baada ya kujifungua ndo nitoe maamuzi, Nimevumilia sana nahisi natumika kama daraja la kuwajulisha wa karibu/ndugu zake kuwa yeye ni mwanaume.

Mwanzo kipindi tunaanza mahusiano alinificha hajaoa ila baadae, tena kwa kumbana ndo akakubali, akasema wanamatatizo ya kindoa ( hawana mtoto) ila hawajaacha wanaishi wote hapo nikiwa tayari mjamzito mtoto wa kwanza, Tumezidiana 10yrs.

Mambo yanayonichanganya ni haya:-

# Ukimpigia cm yupo busy na anaweza asipige mpaka kesho yake tena mida ya kuanzia saa mbili asubuhi mwisho saa mbili au tatu usiku.
#Matumizi ya mtoto mpaka  niombe.
# Hajibu sms, zinaweza pita hata siku mbili au mpaka umpigie kuuliza.
# Anajali marafiki zaidi.
# Hakutambulishi kwa ndugu mpaka kuwe na tatizo ndo atakuunganisha nao tena kwa cmu.
# Akiwa nje ya mkoa kikazi ndo atakupigia sana cm hata usiku wa manane.


Naumia sana kwani tayari ni mjamzito tena ila ndo hivyo navumilia kwa sababu ni mwajiriwa kampuni binafsi nimejenga kijumba cha vyumba viwili maisha yanaenda.

JINA KAPUNI

Reactions:

0 comments:

Post a Comment