Thursday, September 26, 2013

hahahahahahahahahahahahaha uuuuwwiiiiii

Sio kila anayeonekana Online kwenye Whatsap yuko interested kuchat..Hata kaa ni mpenzi wako...Yaani hamna kitu nalaani kwenye Whatsap kama hii kitu inaitwa 'Last Seen at' imekaa kimbea kweli,sometimes mtu umeboreka,hauko kwenye mood ya mahaba,ila ukionekana uko online na hujamtumia SMS laaziz eti anawaka,''anhaaa unachat na mahawara zako eeh,uko online hata hunitext''
Kwani kuwa online lazima nikutext??Sina watu wengine wa kuchat nao hadi na wewe uwemo??Mbona mapenzi yanakuwa magumu hivi jamani??
Nikikutana na owner wa Whatsap,sijui anaitwa Jimmy Balsamik ntamwambia atoe hii icon ya kimbea,inavunja sana ndoa..
Last seen my foot...Mtu unaaga sa4 umelala unaonekana last seen sa9 usiku,sikia hilo zogo lake,kumbe maskini ulishtuka kwenda kukojoa ukasoma msg ukalala,utajieleza kama katibu wa chama cha upinzani na hutaeleweka. Shikamoo Whatsap!

Imeandikwa na: Mosse Sakar

0 comments:

Post a Comment