Wednesday, October 2, 2013

HASIRA NDANI YA NDOA...

binadamu yeyote yule huwa anahasira hiki ni kitu cha kawaida katika maisha ya mwanadamu, sema tunatofautiana sana katika matumizi ya hizi hasira zetu...ukikuta tena ndio umechochea na pombe basi ndio balaa hasira mara mia zaidi..

mwanaume yeye katika maisha yake yote anajuwa kwamba ndio kichwa cha familia na ndio anayetakiwa kutawala maisha ya mwanamke kwa ujumla.

kwasababu ya hiyo mwanaume anataka maamuzi yake yeye ndiye yafwate na sio yako hapo ndio ukimkatalia na maamuzi yake unakuwa kama umempandisha jini la hasira anakuwa mbogo.

ndio na wanawake pia tunahaki ya kusikilizwa na kufanya maamuzi yetu, sio kwasababu umenioa au wewe ndio mpenzi wangu basi nifwate kila unachotaka.

lakini pia kumbukeni wanawake tumeambiwa tuwatii waume zetu...tutawatii vipi kama ndio mtu mwenye hasira mda wote.

 wewe mke ndiye unayemjua mumeo kuliko mwanamke yeyote ukiacha mama yake, akija leo unajuwa huyu kavurugwa, amejivuruga ama nimemvuruga...

ndio hivyo ni vitu vitatu tofauti...tuchambue sasa


KAVURUGWA: inawezekana ikawa kazini, familia yake, au katika vijiwe vyake anavyokaa kabla hajarudi nyumbani


AMEJIVURUGA: inawezekana kagombana na wewe kabla hajaondoka ama kabla hajafika nyumbani, au ni mwanaume mwenye mwanamke nje na ameshagombana na huyo mwanamke wake nje ndio karudi kwako.

NIMEMVURUGA: ndio kero na maneno yetu sisi ndio yanamfanya kumpandisha hasira..hapa sababu ya hasira yake ni wewe ndio umemsababisha

lakini majumuisho hayo yote hasira zake zinakuishia kwako wewe MKE au MPENZI hapa haswa kwa wanaokaa nyumba moja iwe kwa ndoa au bila ndoa

ndio ni kweli kabisa, kupandisha na kutuliza hasira ya mwanaume wako ipo mikononi mwako wewe mwanamke

unapomuona mwenzio kaja na hasira mpokee na ongea vitu vinavyohusu kula, kuoga na kulala tu kwa usiku huo usianze mada zisizokuwa na msingi...haswa zile za kuchokonoachokonoa

muache mtoto wa watu alale kwa amani asubuhi akiamka ndio uanze kumuuliza tena kwa upole na upendo kama mkewe mume wangu mbona jana nilikuona haupo sawa ulikuwa kama umekasirika hivi kuna tatizo mpenzi???

mwanaume mwengine atakaposikia umemuuliza kwa upole vile utayeyusha moyo na hasira zote zilizokuwa kiporo na atakueleza yote.

lakini pia kuna mambo yaliyomsababishia hasira ambayo wewe hutakiwi kuyajua wenyewe vinaitwa MEN'S STUFF..sio kwamba hakupendi hataki kukwambia lakini anajua akikwambia utakasirika utaanza mzozo maneno matusi mwishoe mtaishia kugombana wenyewe kwa wenyewe na wanaume wengine hasira zipo mikononi mara umemtukana na kugombana akakupiga..inakuwa haipendezi.

asipotaka kukwambia akikujibu tu hamna nipo sawa basi wewe kama mke kaa kimya usizidi kuchokonoa liache lipite kwa amani.

zaidi jitahidi tu kuwa karibu naye kumbembeleza kwenye msg, kumpigia simu na akirudi onyesha kwa zitendo kisses, kumkumbatia zinasaidia sana kumfanya mwanaume aone kwako ndio kimbilio lake.

sasa wewe nenda kajifanye mjuaji arudi na mahasira na wewe jana usiku ushachukua simu yake umepekenyua ukagundua anahawara basi unajisemea leo akirudi huyu bwana atanikoma.

mtoto wa watu kavurugwa kazini kaja na mihasira unaanza kupayuka wewe kama umemeza tepu maneno kibao ya kashfa matusi hayakuishi bibi wanaume hawapendi kuzozana atafungua mlango ataondoka zake kwenda kupata pumziko kwengine iwe gesti tu analipia alale au amtafute yule msichana anayependa kujichekesha akimuona au ndio akimbilie kwa hawara.

sasa wewe umefaidika nini hapo zaidi ya kutia ndoa yenu mibalaa inayoweza kuzuilika..

tatizo wanawake siku hizi mnachukulia ndoa kirahisirahisi nyieeeeee ukipata bwana unataka kuolewa halafu unaolewa hata kufundwa hujafundwa unaondoka na mitabia yako ya ugalfriend ya huko kichochoroni kwenu unampelekea mumeo unadhani ndoa itadumu...

nitawafunda nyie mpaka mkae sawa na mameno na misuto ni tawapa japo ya kuandika wote ninao wafunda inbox wanajua wanayoyaoga huko wakikosea...mfyuuuuuuuuu


Reactions:

0 comments:

Post a Comment