Wednesday, July 31, 2013

Word


Ndio upo busy sana. Kuanzia form one umesoma boarding hadi degree na baada ya hapo umepata kazi unatoka nyumbani sa12 unarudi sa 2 usiku. Lakini hii sio sababu ya kukufanya usijue kupika. Haipendezi msichana wa zaidi ya miaka 15 akiwa hajui kupika chakula kizuri watu wakala wakafurahi. Hauolewi ili uende kupika lakini kumbuka kila siku inawapasa kula. Kila msichana lazima ahakikishe anajifunza kupika, hakuna anayezaliwa anajua kupika ila ni kujifunza na kupika mara kwa mara. Usimtegemee tu dada wa kazi ndiye akupikie, hata akipika vibaya hutakuwa na ujasiri wa kumkosoa. Watoto na mume hujisikia vizuri wakipikiwa chakula mama/mke. 

Kwa wale walioolewa hakikisha kila wiki kuna siku ambazo unapika wewe mwenyewe kwa ajili ya familia yako. Sio kila siku kila wiki kila mwezi ni dada wa kazi tu ndiye anayepika. Yani ufanye bidii uwe unajua kupika zaidi ya dada uliyenaye hadi ifike mahali ukipika chakula wote wajue mama leo aliingia jikoni na wakati mwingine wakuombe uwapikie kitu fulani maana wanajua wewe ndiwe mtaalamu.

Source:Global Publishers

Reactions: