Wednesday, July 31, 2013

Makala kutoka kwa dada yangu Irene kwenda kwa wanawake...


Mwanamke una haki, mwanamke na wewe ni binadamu, una moyo, una damu, una kila kitu cha kibinadamu, kama mwanaume akichanjwa anatoka damu na wewe u natoka damu, kama mwanaume akipigwa na jiwe anaumia na wewe utumia, tena wewe zaidi kwani mwili wako hauna masozi za kuhimili mamboo mazito na magumu.
Mungu alipomummba mwanamke alimuumba kwa upendeleo, akampa ulaini, akampa kumvutia mwanaume, akampa kumtamanisha mwanauma kuanzia nje mpaka ndani, kwa asili kabisa mwanamke ni Pambo/ kivutio.

Swali je kivutio/ pambo linachukiza?
Hili ndilo swali la kujiuliza na kulifanyia kazi,, je wewe sio pambo? je wewe sio kivutio?
Pengine jibu unalo ambalo ungesema tu, MIMI NI PAMBO NA MIMI NI KIVUTIO.
Swali lingine ningekuuliza kazi ya kivutio na pambo ni nini? Najua utanijibu kirahisi sana kwamba ni KUFURAHISHA NA KULIWAZA NA KUPENDEZESHA. Sawa umepata.

Sasa tuje hapa kwenye swali lingine kabla hatujaja kwenye kilichopelekea niandike makala hiii.'
,Je ni kivutio kwa mtu special ama kwa mtu yeyote ama kwa watu wengi(wanaume) Nijuavyo mimi kivutio kinaweza kuwa kwa watu wengi ama mtu mmoja, ila tunapokuja kwa wanaume basi bila shaka utanisapoti kwa kukubali kwamba kivutio kwa mumeo tu kama sio mpenzi ama mchumba anayetarajiwa kukumiliki.
Na inapoleta kivutio na mvuto halisi na pambo basi ni kwa mwanaume mmoja, inapokuwa zaidi ya mwaname mmoja sasa sio kivutio tena ila ni neno jengine bovu singependa kulitumia hapa kwani huwa sipendi kabisa mwanamke adhalilike na awe wa namna hiyo.

Swali kuu hapa ni hili,, Je wewe ni kivutio, pambo.... sawa kabisa kulingana na maswali hapo juu yaliyojibu , kivutio hutunzwa, kivutio hupendezesha na huthaminiwa,, je kwa nini wanaume hawatuthamini? kwa nini wanatutesa? kwa nini wanatuumiza? Je hatuvutiii? je sisi sio mapambo?
Jibu hapa kila mmoja ana jibu lake kulingana na mahusiano yake, huyu atasema hivi na huyu atasema hivi,
Lakini tatizo lingine linakuja pale unapokuwa na hali ya kutoheshimiwa, kuthaminiwa na kupenda na mwenza wako,, yule ambaye anakumiliki kihalali kabisa anapokufanyia mambo ambayo huyapendi unaanza kuwaza kwa nini? je umepoteza uthamani wako, umepoteza mvuto wako umepoteza nini hasa kipelekeacho wewe kutothaminiwa?

Unapokosa kuheshimiwa, kupendwa na kuthaminiwa maana yake ni kwamba UMESHUKA THAMANI... Hii ndiyo maana halisi, katika kila kitu ambacho kinakosa uthamani na kuvutia maana yake halisi ni kwamba THAMANI IMESHUKA, Hivi ni kweli hata kwa binadamu (mwanamke na mwanaume ) (hapa naongelea zaidi mwanamke,,,) Mwanamke naye thamani hushuka? Na inashukaje shukaje? Unaona tunapata maswali mengi ya kujiuliza kila saa kila siku, kila dakika... Nini maana yake basi? Huenda kuna tatizo pengine unalifahamu ama nalifahamu maana utajiuliza, mpenzi huyu niliyempenda aliyenipenda, aliyenithamini inakuaje sasa anaiumiza? hanithamini? hanipendi? ananidharau nk? UTAJIULIZA SANA MASWALI MENGI MNO AMBAYO KUNA UTAPATA MAJIBU NA MENGINE HUTAPATA MAJIBU.

Ni lazima sasa kabla hatujaanza kulalamika juu ya kutothaminiwa, kupendwa na kufurahiwa na wapenzi wetu, wenza wetu waume zetu tuangalie uhalalisia wa jambo katika kuhakiki mvuto na upambo (pambo) kama upo na haujapotea ili sasa tunapopelekea shutuma moja kwa moja na kuwa na maamuzi mengine tuwe tunaamua katika hali ya halali ama kuipa miyoyo yetu fursa ya kufurahi katika maamuzi hayo na kuepusha maumivu, kwani wengi huamua lakini huwa na maumivu na kufikiri kwingi kurudia njie ile ile ambayo wameicha ndipo sa unajiuliza kama huku hakuwa pambo je huku atakuwa pambo? na je umejua ni kwa nini wewe sio pambo kule na kwa nini hukuthaminiwa kule ili sasa unapoingia katika HALI YA AWALI KWA MTU MWINGINE, ujue kama kosa ni lako ama sio lako?