Umekataliwa. Umeonekana hufai. Hakuna mtu anayetaka kuwa karibu na wewe. Hujui mapenzi ya baba. Hakuna aliyewahi kukuambia wewe ni mzuri. Hakuna aliyewahi kukuambia anakupenda. Sasa umekata tamaa, unajiona huna thamani, unaona kama Mungu amekuacha. Ukipitia jambo mojawapo kati ya haya ni rahisi sana kuingia kwenye mahusiano ambayo sio sahihi. Moyo wako unahitaji kubwa la kupendwa na hakuna akiyelitimiza, hivyo mtu akikuambia anakupenda, akakuambia maneno mazuri, na zawadi kidogo sio rahisi akili yako ifikiri vizuri.
Sasa kabla haujaingia huko na kuja kujuta, nakupa habari njema. Yupo rafiki wa kweli ambaye upendo wake washinda vyote. Ukimpata huyo ataondoa ukiwa wako wote na kukupa furaha na tunaini la milele. Yeye huganga mioyo iliyopondeka na kukuponya jeraha za kukataliwa, naye hukupa mapenzi ya mzazi ambayo hujayapata na unayatafuta mahali si sahihi. Rafiki huyu ni Bwana Yesu Kristo.
ZAB. 147:3
"Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao."
Hakuna sababu ya kutafuta upendo mahali ambapo si sahihi, mtafute Yesu na huyo kijana unayetaka akupende atakukuta chini ya uvuli wa mbawa za Yesu, mahali pa salama. Itambidi kwanza ampate Yesu ndipo akupate wewe.
Source:Women of Christ