Shalom
Tukisoma habari za Sarah katika biblia tunaona kuwa alipoona umri unaenda na hajapata mtoto alikata tamaa na kuvunjika moyo. Kukata tamaa huku kukampelekea kumshauri mumewe jambo alilokuja kulijutia baadaye. Mumewe alimwamini sana na alikuwa tayari kumsikiliza, Sarah alitumia nafasi hiyo vibaya ikaleta majuto ulimwenguni kote.
Mwanamke una nafasi kubwa sana ya kumshauri mume wako, tumia nafasi hiyo vizuri kwa kuomba uongozi wa Roho mtakatifu. Usitoe ushauri ukisukumwa na hasira, kukata tamaa, chuki au hata wivu. Toa ushauri ambao matokeo yake unaweza kuishi nayo na hayatasababisha maumivu au madhara kwa mtu yoyote.
Ubarikiwe na Bwana Yesu.
Source:Woman of Christ