Sunday, July 14, 2013

Uswahilini kwetu...

Uswahilini kwetu kuna msiba wa mkaka tu masikini alikuwa hajaoa ila anamwanamke ambaye kila mtu mtaani alijuwa ni mwanamke wake.

Tatizo wanawake wa siku hizi jamani wengi hawana aibu wala adabu hawana wanawake siku hizi wengi hawajiheshimu yani miili yao hawaithamini wanaichukulia tu poapoa ili mradi wapate kitu kidogo kutoka kwa wanaume.

Sitaki kumuhukumu huyu mwanamke labda ni kwasababu ya ugumu wa maisha walio nayo kwao ndio maana akaamua kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, ama labda ni tamaa za kupenda mteremko ndio maana akaamua kuwa anachuma huko na kule au ni hulka tu ya umalaya aliokuwa nao ukamtia aibu na balaa.

Huyu dada wakati anamwanaume huyu ambaye kila mtu mtaani anamjuwa kumbe pembeni alikuwa na mwanaume mwengine ambaye na yeye huyo mwanaume alijiamini kwamba yupo peke yake katika maisha ya huyo mwanamke, kumbe haikuwa hivyo na cha kushangaza mwanamke alivyowaajabu yani kaenda kuchukuwa mwanaume mwengine mtaa wa tatu kutoka mtaa anaoishi na huyo bwana yake.

Jamani wanawake/wanaume kama unaona inakubidi wewe kuwa na kidumu basi katafute huko wa mbali sio karibu mkaanza kutiana aibu, wengine vidumu wanachukuwa marafiki wa mabwana zao au marafiki wa wanawake zao bibi inahusu...

Back to the story, basi juzi ijumaa kulikuwa kuna harusi mtaani kwetu nyumba kama ya tatu na siye tena wanawake na wanamtaa lazima ndio kwenda tena shoga bwana sikaenda na bwana yake huyo ambaye kila mtu mtaani anamjuwa, jamani harusi za uswahilini likipigwa goma tu mpaka watu wa mtaa wa nne watakuja yani haina waalikwa hiyo mtu yoyote ndani, sasa katika hiyo sherehe kulikuwa na rafiki mmoja wa kile kidumu cha yule dada kumuona yule mwanamke ana mwanaume mwengine ndio kumpigia jamaa na kumpa umbea (jamani kumbe hata wanaume ni wambea, siye kusutwa sunna nyie je)..

Bwana kupata habari huko tena ndio kuja na washikaji zake hasira zimembana kufika pale hajataka story a wala b yeye shika yule bwana shindilia ngumi za haja harusi tena ya watu ikawa vurugu watu wanapigana huku na kule ndio kutolewa nje wakaenda tena kupigania nje yule mwenye mwanamke sasa akapigwa akawa kashindwa na kidumu.

Akaondoka akaenda kwao kumbuka sio mbali na hapo huku nyuma akamuacha kidumu anazozana na mwanamke wake mara ghafla kaja na kisu mkononi anataka kumchuma kidumu jamani yule kaka ni MUNGU tu yani wakaanza kupigana tena mara bwana kamkata kidumu kwenye mkono damu zikaanza kutoka kidumu naona hasira zikampanda mara kumi akampiga sana yule bwana na akafanikiwa kumpokonya kisu na akamchoma mwenzake zaidi ya mara moja watu ndio kelele na vilio wakamchukuwa kumpeleka hospital lakini akafia njiani.

Kile kidumu kikambia mpaka sasa kinasakwa na polisi ili wamemkamata mama yake kwenda kutoa maelezo labda wakimbana anaweza kusema mtoto kakimbilia wapi....

MAJANGA: mwanamke wake mwenyewe, kuhudumua ahudumie yeye kuumiziwa aumiziwe yeye na kuuliwa auliwe yeye...inauma sana

Na nyie wanaume kweli jamani mpaka unagombana na mwanamme mwenzio kisa mwanamke mnapigana na kutoana roho inahusu jamani au ndio kupenda kupenda gani huko kwa ujinga simnamalizana kimyamkimya kwa kuonyana ila akiwa hasikii unachukuwa uwamuzi mwengine ambao lazima ataacha lakini sio kuuana...au kama vipi si unampotezea tu kwani mwanamke yupo mmoja,au ndio mara yako ya kwanza kupenda...mfyuuuuuuuu

Reactions: