Friday, July 12, 2013

Hongera Dida...

 HUKU akiwa na umri wa miaka 28 tu, mtangazaji kiwango wa Kituo cha Radio Times FM cha jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’, ameibua mazito baada ya kufunga ndoa kwa mara ya tatu, Ijumaa Wikienda lina stori kamili.

Dida alifunga ndoa hiyo na mtangazaji Ezden Jumanne Ntambi (27), ambapo ‘kigodoro’ (muziki) kilifunga mtaa maeneo hayo.
Ndoa hiyo ya Kiislamu ilifungwa usiku ambapo mastaa kadhaa hasa mashosti wa Dida walijitokeza huku wengine wakiguna, eti iweje akiwa na umri wa miaka 28 afunge ndoa tatu?


Baadhi ya mashuhuda ambao muda mwingi walikuwa wakimwaga vigelegele ni pamoja na mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima, mtangazaji wa Radio One, Bi. Hindu na mwanamitindo Khadija Mwanamboka hasa kaka wa Dida, Hussein Shahibu alipokuwa akimuozesha dada yake.

BI. HINDU ARUSHA VIJEMBE
Wakati shamrashamra zikiendelea, Bi. Hindu alikamata kipaza sauti na kuanza kuwapiga vijembe watu wasiojulikana huku akisema wenye wivu wajinyonge na wenye husda watajiju.
Katika tukio hilo ulifika muda wa bwanaharusi kuingia chumbani kumuona mkewe ambapo mvulana mtanashati aliyeonekana kuwa mcha Mungu alijongea kwa Dida na kumshika kichwa wakati akimuombea dua.

DOTNATA AWAPA SOMO MAHARUSI
Baada ya Ezden kuungana na mkewe, msanii ambaye ni mdau mkubwa wa burudani Bongo, Husna Poshi ‘Dotnata’ aliwaweka chini maharusi na kuwapa somo la jinsi ya kuimarisha ndoa yao.

WATOTO WA USWAZI WAVAMIA SHUGHULI
Uswazi ni uswazi tu, watu hawana dogo, licha ya maharusi kualika watu wachache lakini Dida alionekana kuushangaa umati uliofurika hasa watoto wa uswazi, waliokuwa wakipigia misele ‘bufee’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Dida alisema anafurahi kufunga ndoa na Ezden na kuahidi kufuatana naye katika maisha ambayo yatampendeza Mungu.
“Namshukuru Mungu nimempata mwenzangu ambaye nadhani Mungu ataibariki ndoa yetu... ikitokea nikiachika sitaweza kukubali kuolewa tena,” alisema Dida.
Baada ya kutimiza umri wa miaka 18 hadi sasa akiwa na miaka 28, ndani ya kipindi cha miaka 10, tayari ameshafunga ndoa mara tatu, jambo linalozua manenomaneno mjini.
Kabla ya Ezden, Dida aliwahi kufunga ndoa na Mchops akaachana naye kisha akaolewa tena na Gervas Mbwiga ambaye waliachana mwaka jana.


Source: Global Publishers