Napenda kumshukuru MUNGU kwa siku ya jana, na wanawake wote waliokuja kufundwa hata baada ya kubadilisha ukumbi dakika za mwisho lakini waliweza kufika kwakweli nimefarijika na kuzidi kujuwa kwamba wanawake wakiamua wanaweza na ninajuwa wanawake kweli hawataki kuachwa nyuma wanapenda kujifunza wanapopata muda, mapenzi na mwaswala ya chumbani hayana mjuaji wote tunajifunza na kuendelea kujifunza kila leo ili turidhike na tuithamini miili yetu na ya wenza wetu..Napenda kuwashukuru wote waliokuja na biashara zao siku hiyo na kidogo ama kikubwa mlichopata ni njia tu ya kuinuana kiuchumi wanawake kama leo hujapata basi kesho utapata zaidi cha muhimu ni kumshukuru MUNGU...na pia MUNGU akipenda tukutane tena mwezi wa kumi na mbili katika mafundo mengine ya wanawake na haya yana madera...ahsanteni sana