Wednesday, July 24, 2013

MMhhhhh...Hatareee

Ladies... Usiruhusu mtu kumsema na kumchambua mke wake vibaya mbele zako. Haifai kabisa kumsikiliza mtu akimsema vibaya mke wake tena mkiwa wawili tu naye hayupo kujitetea. Mara nyingi wanaume wa aina hii huwasema wake zao vibaya mbele ya wasichana wasioolewa wakijidai wanawafundisha wasiwe kama wake zao wakati ukweli ni kwamba wanawataka. Anatafuta kuonekana victim kwa mkewe ili apate sympathy kwa binti huyo na hatimaye amkubali.

Jiweke kwenye nafasi ya huyo mke, kwanini unakubali kusikiliza mazungumzo kama hayo? Mtu wa aina hiyo mkemee na usijenge mazoea naye kabisa. Wewe hujaolewa, utawezaje kumshauri wakati huna experience yoyote kuhusu ndoa? Kukaa kumsikiliza mtu wa aina hii na kuendelea kumsikiliza ni kumvunjia heshima mke wake na haipendezi mbele za Mungu. Kama anamatatizo mweleze aende kwa mchungaji wake au mtu mwenye ndoa tena akiwa na mke wake. Usi entertain mazungumzo yasiyofaa na mume wa mtu maana mnaweza kujikuta mmeshakuwa na uhusiano wa kihisia bila kutarajia.


Source:Woman of Christ