Thursday, July 25, 2013

Mke mwema...

Mwanamke, ili ndoa yako ilete mafanikio lazima utafute kwa bidii kuwa na sifa zifuatazo
1. Muombaji
Simama kama mlinzi kwa ajili ya familia yako. Maombi yataisimamisha ndoa yako na kuwavusha katika vipindi vigumu.

2. Mtii
Hii haina upinzani, biblia imemwagiza mwanamke kuwa mtii kwa mume wake katika Bwana. Usishindane na mume wako, mtii na pale anapokuwa mgumu kumtii maombi ndiyo silaha yako.

3. Mshauri
Wewe ni mshauri namba moja kwa mume wako hivyo tumia nafasi hiyo vizuri umshauri kwa busara na hekima na sio kwa kusukumwa na hasira, chuki, kukata tamaa au uchungu. Biblia inamifano ya wanawake walio washauri waume zao vibaya na matokeo yake yakawa majuto; Sarah, hawa, mke wa ahabu na lingine mingi.

4. Mkarimu
Ukarimu kwa watu wote wanaokuzunguka bila kubagua au kuangalia wao wanakupa nini. Onyesha ukarimu kwa moyo uliochangamka. Nyumba inaonekana yenye ukarimu kwa kipimo cha ukarimu wa mke.

5. Msiri
Tunza siri za nyumbani kwako. Usipende kusema kila kinachotokea nyumbani kwako. Sio tu kila unapopishana kauli na mume wako unawaambia ndugu na marafiki zako au pale mume anapoyumba kiuchumi unawaambia watu. Hii sio sawa, mstahi mume wako kwa kutunza siri za ndoa yako.

Source: Woman of Christ

Reactions: